Ripoti ya CAG: Mapungufu katika ukusanyaji wa mapato

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Ripoti ya CAG inaonesha makusanyo ya Mapato ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuongezeka kwa 11%, kutoka Tsh. Bilioni 639.4 mwaka 2018/19 hadi Tsh. Bilioni 703.9 mwaka 2019/20

Licha ya kuongezeka kwa ukusanyaji wa Mapato, kumekuwepo changamoto mbalimbali. Mapato ya Tsh. Bilioni 23.88 yaliyokusanywa na Mawakala kupitia Mfumo wa LGRCIS katika Halmashauri 59 hayakupelekwa Benki

Mapato ya Tsh. Bilioni 60.80 katika Halmashauri 42 kushindwa kukusanywa kutoka vyanzo mbalimbali vya Mapato ya ndani

ATHARI
Mapungufu yaliyoainishwa yanaashiria upotevu au ubadhirifu wa mapato ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa ambayo yangeweza kutumika katika kuboresha huduma za kijamii na kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri husika.

Mfano, Kama mapato ya TZS 113.24 bilioni yaliyohusishwa na kasoro zilizobainishwa yangekusanywa, yangechangia TZS 11.59 bilioni katika Mfuko wa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.

USHAURI


WAJIBU inashauri Ofisi ya Rais - TAMISEMI ifanye yafuatayo;

1. Isimamie maelekezo yote yaliyotolewa kwenye Memoranda ya Fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 2009 pamoja na Randama zake, ili kuhakikisha mapato yanakusanywa na kutumika kwa mujibu wa Sheria

2. limarishe Vitengo vya Ukaguzi wa Ndani na Kamati za Ukaguzi (Audit Committees) za Halmashauri ili viweze kusimamia kikamilifu mapato ya Halmashauri,

3. Pale ambapo kuna viashiria vya rushwa na ubadhirifu wa mapato ya Halmashauri, Mabaraza ya Madiwani yachukue hatua stahiki ikiwemo kuwafikisha kwenye vyombo vya dola wahusika wa vitendo hivyo

4. Kuhakikisha kuwa inakagua mara kwa mara mifumo ya kielektroniki kwenye ukusanyaji mapato ya ndani ya Halmashauri ili kuongeza ufanisi wa mifumo hiyo, na

5. Kuhakikisha Halmashauri zinahuisha na kutunga Sheria ndogo (by-laws) za kukusanya mapato ili kuongeza wigo wa vyanzo vya mapato ya ndani na kuendana na wakati.

WAJIBU INSTITUTE
 
Back
Top Bottom