tremendous
JF-Expert Member
- Aug 12, 2016
- 3,237
- 5,327
Hebu malizia kwanini 4.58 haikujumuishwa?
Ala wasitufanyie hivyo!Ni Mtanzania hawa Mkuu sijui kwanini wanaandika habari nusu nusu, labda ni katika mbinu za kuongeza mauzo yao.
Hebu malizia kwanini 4.58 haikujumuishwa?
Hatukopesheki, huo ndiyo ukweli.
Ukitaka uone hatari la hili deni ni kujaribu kukisia kiasi gani tunalipa kwa mwaka kama marejesho.
Kama kwa mwaka TRA inakusanya net ya trilioni 12, basi asilimia 25 mpaka 30 inaishia kulipa principle na riba ya deni hilo. Hapo hatujaongelea mikopo inayotafutwa sasa kwani "tunakopesheka".
Kutoka tunachokusanya tunabakiwa na asilimia 75 mpaka 70. Gharama za uendeshaji wa Serikali, Bunge na Mahakama si chini ya asilimia 30 ya kile tunachokusanya. Na hapo ni baada ya kubana sana.
Hapo tunabaki na asilimia 40 tu kufanya nayo shughuli nyingine za maendeleo. Hiyo asilimia 40 ni kama trilioni 5 tu!
Kwanza, inaonyesha bila misaada kutoka kwa washirika wetu wa maendeleo nchi inasimama! Kauli za kusema hatutaki misaada ni kutokujua tu hali halisi.
Pili, inaonyesha hatari kwani asilimia 70 hivi ya deni ni deni la nje. Deni la nje lazima ni kwa fedha ya kigeni. Ikitokea shilingi imeporomoka, tuseme ifike 2500 kwa dola, basi tutalia njaa na nchi itaumia sana!
Tatu, kwa kiasi kilichobaki na miradi inayofanywa na pesa za Serikali kama kununua ndege, SGR, airport Chatto n.k. Ipo siku watu watalaani hayo matumizi kama hayataleta faida!
Nne, wabunge wapo wapi kuuliza maswali magumu? Waziri au CAG akitamka deni ni kiasi fulani, inapaswa aeleze ni kiasi gani tunatumia kwa mwaka kulipa hilo deni.
Tano, inabidi tuonyeshe sura nzuri duniani ya kupambana na ufisadi, kufuata utawala bora, n.k. ili hata tuombe kupunguziwa au kufutiwa deni.
Mwisho, hawa wanaotukopesha (waChina wanafurahi kuona maskini anamkopa) kuna siku sisi wenyewe ili kuweza kulipa tutapitisha sheria za kuwapa rasilimali zetu.
Nzi JokaKuu Kiranga
Wakati Bunge linamuita Pascla na Mhariri wa Gazeti la Raia Mwema, tunataka kuona linachukia hatua gani dhidi ya matumuzi haya ambayo hayakuizinishwa na Bunge.
Mimi kama mwananchi na kama mlipa kodi,nashauri Bunge liunde kamati teule kuchunguza matumizi haya.
Pia narudia ushauri wangu kuwa sasa wakati umefika sheria iliyounda Ofisi ya CAG ifanyiwe marekebisho ili iweze kumruhusu CAG kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha za umma na kumuwezesha kumshitaki mtu yoyote yule mahakamani bila kusubiri kibali cha DPP vinginevyo haya mambo kamwe hayawezi kwisha.
Asante sana kwa kutomungunya maneno mkuu..Hatukopesheki, huo ndiyo ukweli.
Wakati Bunge linamuita Pascla na Mhariri wa Gazeti la Raia Mwema, tunataka kuona linachukia hatua gani dhidi ya matumuzi haya ambayo hayakuizinishwa na Bunge.
Mimi kama mwananchi na kama mlipa kodi,nashauri Bunge liunde kamati teule kuchunguza matumizi haya.
Pia narudia ushauri wangu kuwa sasa wakati umefika sheria iliyounda Ofisi ya CAG ifanyiwe marekebisho ili iweze kumruhusu CAG kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha za umma na kumuwezesha kumshitaki mtu yoyote yule mahakamani bila kusubiri kibali cha DPP vinginevyo haya mambo kamwe hayawezi kwisha.
Asante sana kwa kutomungunya maneno mkuu..
Nchi IMEFILISIKA..HATUKOPESHIKI.
Alafu kutwa kufukuza wengine wakati nae anafanya madudu kama haya!!No one can rise the voice except you n me!huyo CAG mwenyewe juzi aliomba msamaha kwa kueleza ukweli:bunge halina uwezo wa kuhoji issues za maana kwa taifa hili watawahoji kina pascal mayala tu na sii kuhoji pesa zimetumikaje..utahoji vipi wakati aliyetumia ni uke muhimili mkuubwa kuliko mingine?utamhoji nani wakati sheria zimemlinda aliyetumia?wee unafikiri hadi anachukua hatua ya kutumia hakujua kama kuna bunge?no alijua bunge lipo ila siii lolote wala chochote kwake..wee huoni wapiga piga kelele kuhusu makonda lakini hakuna anaesubutu kumzuia japo hawapendi anachofanya?wanataka kunzuia lakini hawawezi..by the way huenda hata hizo pesa zilizotumika nje ya bunge walihongwa wwbunge wa ccm sasa niulize watahoji vipi wakati miongoni mwa hizo hela ni zile zikizotumika kuwahonga wao ili sheria ya kudhibiti habari ipite bila kuhongwa?acha kututania mkuu..kwa kifupi awamu hii watu hawaibi ila wanachukua kwa nguvu maana hakuna atakaethubutu kufungua mdomo wake kusema nywee..bora kikwete alikua muoga kidogo
Wakati Bunge linamuita Pascal na Mhariri wa Gazeti la Raia Mwema, tunataka kuona linachukia hatua gani dhidi ya matumuzi haya ambayo hayakuizinishwa na Bunge.
Na mimi kama mwananchi na kama mlipa kodi wa nchi hii,nashauri Bunge liunde kamati teule kuchunguza matumizi haya.
Pia, narudia ushauri wangu kuwa sasa wakati umefika sheria iliyounda Ofisi ya CAG ifanyiwe marekebisho ili iweze kumruhusu CAG kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha za umma na pia kumuwezesha kumshitaki mtu yoyote yule mahakamani bila kusubiri kibali cha DPP vinginevyo haya mambo kamwe hayawezi kwisha.
Tusijikite kujadili tu matatizo ambayo ni matokeo ya mifumo mibovu katika nchi yetu bali tujikite zaidi katika kutafuta suluhisho la vyanzo vya matatizo(madudu) haya.