MakinikiA
JF-Expert Member
- Jun 7, 2017
- 5,698
- 7,884
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema Serikali iko tayari kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kiongozi au mtumishi yeyote wa umma atakayebainika kufanya matumizi mabaya ya rasilimali za taifa, lakini amesisitiza kuwa hatua hizo haziwezi kuchukuliwa kwa msingi wa tuhuma zisizo na ushahidi, hivyo mwenye vielelezo awasilishe.
Msigwa ametoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la mwandishi wa habari aliyeomba ufafanuzi kuhusu kauli ya aliyekuwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Profesa Mussa Assad.
Profesa Assad aliyedai kuwa kuna waziri mmoja ambaye ndani ya kipindi cha miaka mitano amekuwa akimiliki magari ya kifahari, yakiwemo Toyota Land Cruiser LC300 matatu na Range Rover, huku akiishi maisha ya gharama kubwa, hali inayozua maswali kuhusu chanzo cha utajiri huo.
"Kama kuna mtu anafanya makosa katika matumizi ya rasilimali za taifa, anafikishwa mbele ya vyombo vya sheria na anachukuliwa hatua.
-
"Tuhuma hazikuwa na uthibitisho. Mtu yeyote mwenye ushahidi wa kiongozi yeyote wa Serikali ama mtumishi wa Serikali aliyefanya matumizi mabaya ya fedha za umma atoe taarifa na aweke uthibitisho, hatua zitachukuliwa," amesema Msigwa.