Ripoti ya CAG kwa mwaka ulioishia 30 Juni, 2017 imejaa madudu

Ripoti ya CAG kwa mwaka ulioishia 30 Juni, 2017 imejaa madudu

Tulipe deni ili kuepuka tatizo ikitokea dharura, dharura ya nani, Spika Ndugai akizidiwa akumbizwe India?

Kwa nini Watanzania tunakubali kutoa kodi zetu zikatibu watu nje ya nchi watu ambao wana mishahara na mavumba makubwa kuliko sisi raia ? Kwa nini mtu unathamini maisha ya kiongozi kuliko ya kwako?

Asituzingue huyu CAG na aache undumilakuwili, juzi kasema deni linastahimilika.

MKE wa Magufuli anatibiwa Muhimbili, huyu CAG anataka zilipwe hela za kwenda kuwatibu wao kina CAG India, Mzee Magu mtumbue huyu mtu fasta!

Umesoma taarifa ya CAG au umecomment tu?
 
Mkuu usicheze na jiwe!!! Jiwe lilishajaribu kumtumbua CAG lilipoingia tu Ikulu lakini vikaragosi vyake humu vikaja na hoja MUFILISI vikapigwa chini na kuukimbia uzi wao.

CAG hatumbuliki Mkuu. Hakuna mwenye mamlaka hayo labda Mungu peke yake.
 
Deni la supika ndio deni kubwa la nje kuliko yote,kutibu sukari na marukanga huwa ni gharama
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Prof. Mussa Assad amesema sheria mpya ya Madini haimpi ruhusa ya kufanya ukaguzi katika migodi. Aisihi Serikali ifanyie marekebisho.

Aidha, amesema mpaka sasa kuna vyama vya siasa 7 havikuwasilisha taarifa za mahesabu yao.

Pia, CAG amesema madeni ya matibabu nje ya nchi yamekuwa kubwa na yanatishia kusitishwa kwa huduma hiyo, hivyo ameishauri serikali kulipa haraka madeni hayo ili kuepuka matatizo ikitokea dharura..


===

YALIYOJIRI.. ​

"Mapendekezo 201 ya mamlaka za serikali za mitaa yalitolewa na CAG katika ripoti zilizopita lakini ni 43 tu yaliotelekezwa.. Ofisi yangu inaona kuna utekelezaji duni wa mapendekezo yangu"- CAG Profesa Mussa Assad

"Tumetoa hati 527 mwaka 2016/17, hati chafu ziko 42... Kati yake 1 ya saba ni vya vyama vya siasa" CAG Profesa Mussa Assad

"Bado kuna tatizo kwenye mafuta yanayoingizwa nchini kwa kupewa msamaha wa kodi kwa ajili ya uchimbaji wa madini.. Hali hii inaikosesha serikali mabilioni ya shilingi" CAG Profesa Mussa Assad

"Kuna ongezeko la deni la matibabu ya ughaibuni la asilimia 60.2 kwa kipindi cha mwaka mmoja.. Serikali ilipe deni hili kwa hospitali za India" CAG Profesa Mussa Assad

"Kuna ongezeko la trilioni 5/- kwenye Deni la Taifa kutoka Juni 30,2016 hadi Juni 30,2017" CAG Profesa Mussa Assad

"Vyama tisa havikuwasilisha kabisa taarifa za hesabu zake kwa ajili ua ukaguzi" CAG Profesa Mussa Assad

"Kuna madeni ya watumishi, 4.6 ya madeni hayo hayakulipwa licha ya kuwa stahiki zao kutokana na kupandishwa daraja na sababu nyinginezo...Maoni ya ofisi yangu ni kwamba madeni yote yaingizwe katika bajeti ya mwaka mmoja na kulipwa yote" CAG Profesa Mussa Assad

"Kuna fedha zilikusanywa kwenye balozi za Tanzania ughaibuni lakini hazikufikishwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali kinyume cha taratibu" CAG Profesa Mussa Assad

"Serikali za mitaa hazikupeleka fedha za maendeleo kwa asilimia kubwa...Zaidi ya Sh. Bilioni 320 hazikupelekwa ikiwa ni zaidi ya nusu ya bajeti ya maendeleo ya serikali za mitaa" CAG Prosefa Mussa Assad

"Serikali ilikusanya fedha kwa asilimia 94.2, sasa inakuwaje bajeti haijatekelezwa? ..Wabunge wanapaswa kuhiji hili kwa sababu makusanyo yalipaswa kuakisi utekelezaji wa miradi' CAG Profesa Mussa Assad

"Tumebaini kampuni za Bima hazijalipa MNH Sh. Bilioni 1.4" CAG Profesa Mussa Assad

"Sheria mpya ya madini haimpi mamlaka CAG kuingia na kufanya ukaguzi wa migodi. Tunaona kuna udhaifu wa kisheria hapo" CAG Profesa Mussa Assad

"Tumefanya ukaguzi maalum baada ya kuombwa kwenye Chama cha walimu na kubaini kuna malipo ya mabilioni ya shilingi yamefanyika kinyume cha taratibu" CAG Profesa Mussa Assad

"Tumebaini @NIDA_Tanzania kuna ubadhilifu kwa kughushi ukubwa wa eneo lililokodishwa...Mamlaka vilevile ilikuwa inatumia viwango vya kubadilisha fedha kwa hesabu za benki za biashara badala ya BoT" CAG Profesa Mussa Assad

"Ukaguzi wetu TBC ulibaini vifaa vilivyoingizwa na StarTimes kwa msamaha wa kodi havikufungwa mahali popote nchini.. Huenda vimepelekwa mahali pengine ndani ya nchi au nje ya nchi" CAG Profesa Mussa Assad

"Udhaifu mwingine ni StarTimes kupata hasara kwa miaka yote na haikuchagia gaharama za ushirikiano wa mtaji unaofikia Dola 600,000" CAG Profesa Mussa Assad

"Kuna usimamizi duni katika uwekezaji wa alama za barabarani" CAG Profesa Mussa Assad

"Majengo mengi ya umma si salama kutokana na kutokuwa na vifaa vya uokoaji likiwamo jengo hili la Bunge" CAG Profesa Mussa Assad

"Kuna udhaifu katika kutathimini maeneo ya miradi kabla ya kutekelezwa kwa miradi husika..Mfano, kituo cha mabasi ya mwendokasi Dar kinafurika maji wakati wa masika" CAG Profesa Mussa Assad

"Tumebaini kuna udhaifu katika utekelezaji wa taka za kielekroniki nchini.. Hakuna mkakati wala bajeti ya udhibiti wa taka hizo nchini" CAG Profesa Mussa Assad

"Kazi ya CAG ina lawama. Tutazipitia taarifa zote na kutoa taarifa kwa Bunge zima.. CAG ametaja kila sehemu upotevu wa fedha. PAC tumejipanga kuhakikisha halitaachwa jiwe.Kipindi hiki tutatoa mapendekezo mazito zaidi" Mwenyekiti wa PAC Naghenjwa Kaboyoka

Mh. Abdallah Mtolea (Kwa niaba ya Mwenyekiti wa LAAC)

"Tutaanza kuziita Halmashauri mara moja zikiwamo zile zilizomficha CAG vitabu vya risiti"

"Kamati ya Bajeti ya Bunge ijibu au ihoji kwanini fedha zimekusanywa lakini hazionekani zilikokwenda" CAG Profesa Mussa Assad

"Vyama ambavyo havikuwasilisha hesabu zake kwa CAG ni pamoja na ACT-Wazalendo, CUF, Tadea, NCCR na UPDP" CAG Profesa Mussa Assad

Pesa yote inayokusanywa anpewa bwana pombe nayeye ndiye anayeamua ifanye nini. Ndio maana utasikia natoa bilion 10 nk. Ufadi mkubwa unafanyika awamu hii kwa ngongo wa uzalendo na kupiga vita 'ufisadi'
 
Kwa mujibu wa katiba Rais akishamteua CAG hawezi mtumbua kama anavyomtumbua Kitwanga!! Ts a big process tena kwa tume ya kijaji

Mkuu ni kweli hayo usemayo, lakini hiyo ni nadharia na sheria za kwenye makaratasi kwani kwani anayemlipa CAG ni rais.
 
hii hapa safi, nainukuu..

"Serikali ilikusanya fedha kwa asilimia 94.2, sasa inakuwaje bajeti haijatekelezwa? ..Wabunge wanapaswa kuhoji hili kwa sababu makusanyo yalipaswa kuakisi utekelezaji wa miradi' CAG Profesa Mussa Assad
Hili ni swali la msingi kabisa. Inapaswa wale wabunge kama Kibajaj wawe wanapigwa mawe kwa vile badala ya kutumia wajibu wao wa kuhoji wanakuwa wasemaji wa serikali kuwajibu wenzao wanao hoji.
 
Mbona madhaifu yapo mengi sana...

Mipango siyo matumizi...

Kweli CAG ni kazi ya lawama...

Fedha zimekusanywa lakini hazionekani kwa sababu hapangiwi nini cha kufanya...


Cc: mahondaw
 
upload_2018-4-12_9-29-59.png
 
Umesoma taarifa ya CAG au umecomment tu?


Nime comment nilichokiona kimebandikwa hapa. Kama una la nyongeza ambalo wewe umeliona kwenye ripoti kalilete basi ufafanue kilichowekwa humu au unisahihishe.

FOR ALL WE KNOW, Mkaguzi kasema tulipe deni la hospitali India kuepuka kukwama siku ya dharura. Siku ya dharura ya nani akitaka kufa, Spika Ndugai?

Tumechoka, tumeamka, tumekataa! Hatutaki kusikia Mtanzania anaejiona yeye afya yake yeye bora kuliko ya wengine tutoe kodi akatibiwe yeye!

JANET MAGUFULI anatibiwa Muhimbili, hela za kupeleka watu India tulipe ili mumpeleke nani, WASTARA JUMA?
 
Jamaa wanachota tu! Si huyu jiwe aliudanganya umma kwamba matibabu ya nje yamesitishwa? Kumbe ulikuwa uongo mwingine!
Deni hili ka matibabu ni cumulative, limetoka miaka ya nyuma na serikali haijalipa deni hilo. Kama kuna deni la matibau nje ya nchi kwa fiscal year 2016/17 basi ni kidogo sana ambalo litakuwa limetokana na doctoral referrals kwa wagonjwa ambao wameshindikana kutibiwa MNH kama ilivyokuwa kwa yule super tall wa Songea. Siyo matibabu kwa ajili ya viongozi au jamaa zao kama ilivyokuwa zamani, enzi za JK. Let's be fair.
 
RIPOTI YA CAG YAZIDI KUANIKA MADUDU
Pg-4-1-300x172.jpg

Na FREDY AZZAH-Dodoma |


MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, amewasilisha bungeni ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka unaoishia Juni 2017, ambayo imeibua madudu zaidi na kuonyesha deni la taifa likiwa limefikia Sh trilioni 50.

Akitoa muhtasari wa ripoti yake kwa waandishi wa habari mjini hapa jana, alisema ukaguzi wake umejikita kwenye maeneo sita.

Aliyataja maeneo hayo ni ukaguzi katika Serikali kuu, mamlaka za Serikali za mitaa, mashirika ya umma, miradi ya maendeleo, ukaguzi wa ufanisi na ripoti 10 za ukaguzi wa ufanisi kwenye sekta mbalimbali.

Ripoti hiyo ya CAG imeonyesha uozo pia kwenye mafuta yaliyosamehwa kodi, udhibiti mizigo inayosafirishwa nje ya nchi, urejeshwaji mikopo, udhaifu katika usimamizi wa mikataba ya manunuzi, mapato kutowasilishwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali na mawakala kutowasilisha makusanyo kwenye mamlaka za Serikali za mitaa.

Uozo mwingine umeibuliwa kwenye Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Shirikisho la Serikali za Mitaa (ALAT) na Idara ya Uhamiaji.

Akizungumzia deni la taifa, Profesa Assad alisema limefikia Sh trilioni 50 na kwamba ni vyema kama nchi ikakopa kwa tahadhari ili isirudi nyuma miaka 20 ambako ilisamehewa sehemu ya deni.

Alisema hadi kufikia Juni 30, 2017, deni hilo lilikuwa Sh trilioni 46.08 kutoka Sh trilioni 41.03 za Juni 2016, ikiwa ni ongezeko la Sh trilioni 5.04 sawa na asilimia 12.

Profesa Assad alisema deni la ndani ni Sh trilioni 13.33 na deni la nje ni Sh trilioni 32.75.

Alisema katika deni hilo, kuna Sh trilioni 4.58 ambazo hazikujumuishwa kutokana na ….

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
 
Endelea mkuu wengine wako nnje ya nnchi watanufaika.

Hawataweza kupata gazeti la nipashe
 
Ni Mtanzania hawa Mkuu sijui kwanini wanaandika habari nusu nusu, labda ni katika mbinu za kuongeza mauzo yao.

Endelea mkuu wengine wako nnje ya nnchi watanufaika.

Hawataweza kupata gazeti la nipashe
 
Thursday April 12, 2018

The Guardian

We need to cut down on the borrowing, CAG says

Cautions that much as the current national debt of nearly 50 trillion/- remains tolerable, continuing in this way is bad for the nation


CONTROLLER and Auditor General (CAG) Prof Mussa Assad yesterday issued another strong warning to the government against continued external borrowing as the national debt now stands at close to 50 trillion/-.

Controller and Auditor General Prof Mussa Assad addresses a news conference in Dodoma yesterday after tabling his Annual General Audit Report for the year ended June 30, 2107 in the National Assembly. Left is Parliamentary Public Accounts Committee chairperson Naghenjwa Kaboyoka. Photo: Augusta Njoji

Speaking here after submitting the CAG’s annual general audit report for the year ended June 30, 2107 to parliament, Prof Assad asserted that much as the debt remains tolerable, continued borrowing is bad for the nation.

In his report, the CAG states that total public debt as at June 30 last year stood at 46,081.43 billion/-, of which the domestic debt stock was 13,335.65bn/- and external debt stock was valued at 32,745.78bn/-. Total arrears to public servants stood at 4.6 trillion/-.

This is an increase of 5,042.05bn/-, equivalent to 12 percent, compared to the 41,039.38bn/- debt stock reported as of June 30, 2016.

The report says the public debt is continuously on the rise, attributing this to persistence budget deficits, rollover of liquidity papers, new borrowings for various development projects, and foreign exchange loss arising from regular depreciation of the Tanzanian shilling against stronger currencies.

The external public debt portfolio includes loans from multilateral and bilateral institutions, along with development partners. The reported 32,745.78bn/- stock as of June 30 last year was equivalent to 71 per cent of total public debt, the report notes.

It adds that such debt stock increased by 2,899.78bn/-, equivalent to 10 per cent of the 29,846bn/- external debt reported at the end of 2015/16.

According to the CAG, although commercial borrowing appears to have become an economic necessity in recent years especially when the government embarks on major infrastructural projects, a sharp rise of external commercial credits in the country’s debt portfolio “is of concern”.

Such a trend calls for “a more cautious and prudence stance in managing its growth with a view to reduce potential liquidity and rollover risks going forward,” he states, adding:

“My analysis of maturity structure of government securities as at June 30, 2017 indicated that 72 per cent of securities mature within five years as compared to 59 percent reported at the end of 2015/16.”

He recommends the government to set aside part of its domestic revenue to settle some of the maturing domestic debt in order to reduce rolled-over balance, exert more efforts to rebalance the debt portfolio, and enhance the development of long-term government security markets.

“The smoothening of maturing obligations will front load debt repayments as the maturity profile of government security debt portfolio lengthen, save her financing costs, and offer better investment avenues for the long term investors in the country,” Prof Assad further asserts.

According to the report, the rise of external debt is mainly attributed to borrowings from multilateral sources such as IDA amounting to 995.7bn/-, to support various development and social projects including the Additional Financing for Productive Social Safety Net Project (205.9bn/-).

Others such projects are the Southern Africa Trade & Transport Facilitation Project (168.3bn/-), Strengthening Primary Health Care for Results Program (99bn/-), Urban Local Government Strengthening Program (95.2bn/-), Big Results Now in Education Program (52.3bn/-), and Tanzania Strategic Cities II Project (51.8bn/-).

In addition, the government received funds from bilateral sources like France, Saudi Arabia and Japan worth 181.3bn/-, plus External Non Concessional Borrowings (ENCB) in the form of Export Credit Arrangements amounting to 372.7bn/-.

Loan proceeds from ENCB mainly provided by Export–Import Banks of Korea, China and India were directed to projects such as the construction of a data centre for the National ID System (28.2bn/-), construction of the MUHAS Medical Centre Phase I (17.1bn/-), Tanzania National ICT Phase III Sub Phase 1 (41.3bn/-), Tanzania Mnazi Bay and Songosongo Natural Gas (15bn/-), and Dar es Salaam and Chalinze Water Supply Scheme (61.4bn/-).

Furthermore, the government received funds from commercial banks amounting to 978bn/-, including 887.6bn from Credit Suisse AG (UK) as a Term Facility and 74.2bn/- from the Hong Kong Shanghai Bank-HSBC for construction of the Passengers Terminal III Project at the Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom