Ripoti: Tanzania yaongoza kwa wanywa pombe

kipindi cha mgao wa umeme nilipata sms ikitaka serikali isithubutu kuleta mgao wa bia maana patachimbika sasa naanza kuelewa kwanini...
 
Kwa taarifa yako, mlipa kodi namba moja Tanzania ni Kampuni ya bia TBL.Kama bado hunywi bia anza leo uongeze pato la taifa

halafu kipata cha taifa kikiongezeka nafaidika na nini? maana sioni la maana kila kukicha afadhali ya jana..
 
Tanzania imeshika nafasi ya kwanza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanywa pombe za viwandani barani Afrika, ripoti imesema. Idadi ya walevi wa bia imeongezeka kwa asilimia 35 katika kipindi cha miaka 20 iliyopita wakati ile ya watumiaji wa pombe kali imepanda kwa kiwango cha asilimia 25. Nchi zinazoifuatia Tanzania ni Zambia, Afrika Kusini, Malawi na Nigeria.
Bwana yesu asifiwe Mwita!
 
Ni sawa kabisa kwani wanapokunywa husahau machungu ya nchi yao inavyoliwa na wajanja. enadpo wasingekunywa vichwa vingepasuka kwa mawazo. biblia inasema mpe masikini kilevi asahau shida zake.
 
Vipi ripoti ya kunywa Maji Salama au Maziwa

Nahisi hapo tutakua nafasi za mwisho, kuna watu nawajua hawajawahi kununua maji ya kunywa wao ni soda tu
 
Ni sawa kabisa kwani wanapokunywa husahau machungu ya nchi yao inavyoliwa na wajanja. enadpo wasingekunywa vichwa vingepasuka kwa mawazo. biblia inasema mpe masikini kilevi asahau shida zake.

wanapata wapi hela?
 
Du kila kizuri wa mwisho tukija kwa mabaya yasiyokuwa na maendeleo kwa mtu m1 m1 tunaongoza JK na hili lilikuwa kwenye ilani yenu au imekuja kama bahati mbaya
 
kipindi cha mgao wa umeme nilipata sms ikitaka serikali isithubutu kuleta mgao wa bia maana patachimbika sasa naanza kuelewa kwanini...

hizi ni bad news kwa kina mama maana madhara ya pombe kwa kina baba ni janga la taifa.
 
Ivi mtu unavyotoa habari kama izi bila ata kuweka huo utafiti apa as if kuna mtihani tutafanya plagiarism.
Weka huo utafiti apa na umefanywa na akina nani isije ikawa Synovate?
 
Back
Top Bottom