Tanzania imeshika nafasi ya 10 katika nchi za Afrika zenye Passport zenye nguvu zaidi huku ikiwa nafasi ya 74 duniani na uwezo wa kuingia katika maeneo 72 kwa Viza au bila Viza. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Henley Passport Index, kupitia Mamlaka ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (IATA) Orodha hiyo inajumuisha Hati za Kusafiria 199 tofauti na maeneo 227 tofauti ya kusafiri.
Ripoti ya utaiti huu inatolewa kila robo ya mwaka.
1. Seychelles (Nafasi ya 29 Duniani, Maeneo 153 ya kuingia)
2. Mauritius (Nafasi ya 34 Duniani, Maeneo 146 ya kuingia)
3. Afrika Kusini (Nafasi ya 53 Duniani, Maeneo 106 ya kuingia)
4. Botswana (Nafasi ya 63 Duniani, Maeneo 87 ya kuingia)
5. Namibia (Nafasi ya 67 Duniani, Maeneo 79 ya kuingia)
6. Lesotho (Nafasi ya 69 Duniani, Maeneo 77 ya kuingia)
7. Eswatini (Nafasi ya 71 Duniani, Maeneo 75 ya kuingia)
8. Malawi (Nafasi ya 72 Duniani, Maeneo 74 ya kuingia)
9. Kenya (Nafasi ya 73 Duniani, Maeneo 73 ya kuingia)
10. Tanzania (Nafasi ya 74 Duniani, Maeneo 72 ya kuingia)