TANZIA RIP Mwalimu John Lusungu Nusurupia Myavilwa wa Kwaya Kuu Habari Njema Arusha

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
31,868
33,279
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mwalimu Mstaafu wa Kwaya Kuu Habari Njema Arusha Mjini Kati Ndugu John Lusungu Nusurupia Myavilwa.

Atakumbukwa kwa kazi ya kutunga na kufundisha nyimbo za Injili Kwaya mbalimbali nchini ikiwemo Kwaya ya Vijana Makorora Tanga miaka ya 1970+, baadaye akahamia Arusha ambako alitumikia kama Mwalimu wa Kwaya Kuu Arusha Mjini hadi kustaafu kwake miaka ya hivi karibuni,

Pamoja na kuimbia Kwaya Kuu Arusha pia alifundisha baadhi ya wanamuziki walioipigia na kuimbia kwaya mbalimbali nje na ndani ya KKKT, miongoni mwa kanda za miaka hiyo zenye utunzi wake akiwa Kwaya Kuu Habari Njema Arusha ni pamoja na;
  1. Nampenda Bwana Yesu
  2. Jibidishe
  3. Panda Mbegu Njema
  4. Nitakwenda Mbinguni kwenye raha njema
  5. Tutaimba Milele
  6. Wapendeni Adui Zenu
  7. Mko Tayari
  8. Sikiliza ni Sauti ya Mtu
  9. Njia ya Msalaba
  10. Mtafuteni Bwana
  11. Tumo Safarini
Na nyingine nyingi ziliimbwa, kurekodiwa na kupigwa Sauti ya Injili Moshi, Radio Habari Maalum, RTD Sauti ya Kenya na Tamasha Nairobi Kenya.

Mungu Aiweke Roho yake Mahali Pema, mbele yetu wewe na nyuma yako ni sisi

Amin

Untitled.png


Mwalimu John Lusungu Myavilwa aagwa rasmi 28.08.2022 mjini Arusha na kusafirishwa kwenda kupumzishwa kwao 29.08.2022 Ramadhani mjini, Njombe

1662218183141.png


1662218220940.png
 
Back
Top Bottom