Hawa watu wanajua kujipanga sana kwa yanayokuja..wamepanga kujilinda.
Let me break this down kuonyesha vipi hawa watu ni wapuuzi wa kutupwa myopic na hawaangalii kesho; Ni miaka kama kumi au zaidi sasa huwa nina msemo wangu kwamba hawa walamba asali hawajui kula na vipofu, na nilishasema yakitokea ya French Revolution unadhani ni mali za nani watu wataanza kuzichoma ? Hata kama sio hawa basi ni wajukuu wao - Ni kama wametarnish jina la Ukoo.....
Nina uhakika hata kipindi cha Mwinyi sio Mama Sitti pekee alikuwa kibaka; ingawa hatukuwasikia watoto wa Mwinyi kama huyu jamaa, (hio ndio hekima) ; Kipindi cha Mkapa alikuwepo limbukeni mwingine mama Anna Mkapa... kila mtu aliona kwamba huyu ni kibaka, na wizi wa Mkapa ungesikika sana huenda watu wangelia na kusaga meno....
Sasa kama mpaka wewe unaona kwamba hawa wanajipanga huoni kwamba sio wajanja na hawajui kujipanga ? Joe Kennedy alikuwa na ndoto ya kumuweka mtoto wake Ikulu ingawa yule aliyepanga alipata ajali ila bado aliendeleza na mpango wake na kupanga mikakati kufanya JFK akawa Rais (kwa kutumia media na propaganda kumfanya kama an angel on earth, na kutumia mlungula mpaka connection za Mafia) - Ila watu walijua ?
Kama mtu unaweza kuteua yoyote wakati wowote kwanini usiweke mtu ambaye kwa macho ya mbali hajulikani kama ni mtu wako ? After all akizingua si unafukuza ?
Kumbuka Demokrasia kwa ukubwa wake ni illusion ili watu waone kwamba wameshirikishwa wakishaona hivyo basi wataridhika na mambo yatakwenda (hata kama ni usanii) Sasa kama unadanganya watu wanaojua kwamba wanadanganywa what is the flipping point (to put it mildly); Kwahio mimi kama mlipa Kodi kama hii Demokrasia wala haiwapi watu ile Illusion (feel good factor) kwamba nimemuweka mtu Ikulu - basi haina maana; na waliofanya hayo ni hawa unaodhani wanajua kujipanga - Mjanja ni yule ambaye hujui kama yupo lakini yupo - sababu huyu ataendelea kupeta bila shida yoyote.... The Greatest Trick the Devil ever Pulled was to Convice the World he did not Exist....
Nakumbushia niliyowahi kusema kabla
Tukumbushane tu...,
Sisemi kwamba hili linatokea Sasa lakini Kutumika kwa Rasilimali Fedha na Muda kwenye Maigizo ya Demokrasia au Kutumia Pesa kwa Propaganda, ni bora Muda na Pesa hizo zikatumika kuleta maendeleo kwa Wananchi wanaojua Demokrasia haipo (Maigizo yana Gharama isiyo na Tija, Hususan pale yule unayemuigizia anajua ni Maigizo)
He is not deceived who knows himself to be deceived.