mkulimamwema
Senior Member
- Apr 14, 2011
- 153
- 18
Mtoto wa nyoka ni nyoka tu
Ngoja broda,me hua nashangaa sana manake kama mtu ananjijua kua yupo safi wala hakuna hato sita hata kidogo
kwenda huko mahakamani.
sasa we utuhumiwe/uchafuliwe hivi, af unajijua kua upo safi kweli utakaa kimya.
we riz ni mwizi na ndo sababu unasita sna kwenda mahakamani.
Kama hii issue inahusu maisha yake binafsi mboma alikurupuka kwenda kwenye vyombo vya habari kuwapa waliosema notisi ya siku saba? It doesn't make any sense to me.
Hivi kweli wandugu wapenzi hii sio EPA No2???? Maana huyu Rais wetu alisema fedha za EPA wale wezi wamerudisha Tshs 70,000,000,000/= bilion sabini. Ikasemekana fedha hizo zimepelekwa TIB benki ya rasilimali ya taifa zote.Baadae tukasikia hizo fedha zimepelekwa kilimo kwanza na Mhs Rais Tshs 20,000,000,000/= Twenty billion. Sasa ebu tuulize swali hizo Fifty Billion zilizobaki zilikwenda wapi???????? Au bado zipo, na kama zipo ziko wapi na zinatumika kufanya nini????? Majibu tafadhari watu wa TIB au serikali na kilimo kwanza, Waziri mkuu au vipi???? Hizo ni fedha zetu lazima tujue vinginevyo ni EPA No2!!!!!!!Mtoto wa Rais Kikwete angaka
MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani, amesema hataki kufuatiliwa maisha yake na wanasiasa hasa wanaomtuhumu kuwa ni bilionea huku akisisitiza kuwashughulikia waolimchafua.
Ridhiwani, alisema hayo jana alipozungumza na Tanzania Daima akitakiwa kueleza hatua atakazochukua baada ya muda wa siku saba aliowapa Mwenyekiti wa Demokratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbrod Slaa kupita.
Awali, mtoto huyo wa Rais aliwataka wanasiasa hao wamwombe radhi katika kipindi cha siku saba vinginevyo angewapeleka mahakamani kwa kuwa wamemchafua pamoja na familia yake.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa njia ya simu, ili kujua lini angekwenda mahakamani kuwafungulia mashtaka viongozi hao, alijibu kwa jazba kwamba jambo hilo linahusu maisha yake hivyo haoni sababu ya kufuatiliwa na vyombo vya habari.
Jambo la kuwafikisha wanasiasa hao mahakamani si jambo lenu, hilo ni jambo linalonihusu mimi na maisha yangu hivyo nitachokifanya nakijua mwenyewe, alisema Ridhiwani huku akisisitiza kwamba hata alipozungumza na waandishi wa habari juma lililopita alisema lengo lake ni kuueleza umma na sio kufuatiliwa maisha yake.
Kwa nyakati tofauti Mchungaji Mtikila na Dk. Slaa, walimtuhumu Ridhiwani kwa ukwasi huku wakiitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kumchunguza.
Mchungaji Mtikila pamoja na Dr Slaa tafadhari anzeni na huyu kijana RIZ 1, apelekwe mahakamani aeleze alipataje hiyo mifedha. Kama alifikiri mahakama ni mchezo aone moto yeye ni lawyer atatokea mbele. Nia hasa ni kuzuia kwa muda malengo ya wizi wa mali za wananchi kama vile ni shamba la bibi!!!! Wengine watafuata baada ya kumaliza muda wao hapo Magogoni!!!!!!!Mtoto wa Rais Kikwete angaka