familia nzima yaani hawaeleweki..kuanzia baba hadi watoto.......
Mtoto wa Rais Kikwete angaka
MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani, amesema hataki kufuatiliwa maisha yake na wanasiasa hasa wanaomtuhumu kuwa ni bilionea huku akisisitiza kuwashughulikia waolimchafua.
Ridhiwani, alisema hayo jana alipozungumza na Tanzania Daima akitakiwa kueleza hatua atakazochukua baada ya muda wa siku saba aliowapa Mwenyekiti wa Demokratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbrod Slaa kupita.
Awali, mtoto huyo wa Rais aliwataka wanasiasa hao wamwombe radhi katika kipindi cha siku saba vinginevyo angewapeleka mahakamani kwa kuwa wamemchafua pamoja na familia yake.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa njia ya simu, ili kujua lini angekwenda mahakamani kuwafungulia mashtaka viongozi hao, alijibu kwa jazba kwamba jambo hilo linahusu maisha yake hivyo haoni sababu ya kufuatiliwa na vyombo vya habari.
Jambo la kuwafikisha wanasiasa hao mahakamani si jambo lenu, hilo ni jambo linalonihusu mimi na maisha yangu hivyo nitachokifanya nakijua mwenyewe, alisema Ridhiwani huku akisisitiza kwamba hata alipozungumza na waandishi wa habari juma lililopita alisema lengo lake ni kuueleza umma na sio kufuatiliwa maisha yake.
Kwa nyakati tofauti Mchungaji Mtikila na Dk. Slaa, walimtuhumu Ridhiwani kwa ukwasi huku wakiitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kumchunguza.
Kasome Tanzania Daima. Mie nilisema katika thread nyengine huyu hana ubavu wa kuwapeleka mahakamani akina Dr Slaa. Anapambana na mlima mkubwa asiouelewa nao ni nguvu ya umma. Nadhani amepata ushauri mzuri na kuwajulisha watanganyika kumbe na yeye ni Bilioneaasante ndugu,chanzo cha habari??
Asante tupe chanzo cha habari.....