Ridhiwani Kikwete ang'aka tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ridhiwani Kikwete ang'aka tena

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Red one, May 9, 2011.

 1. R

  Red one Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mtoto wa Rais Kikwete ang’aka


  MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani, amesema hataki kufuatiliwa maisha yake na wanasiasa hasa wanaomtuhumu kuwa ni bilionea huku akisisitiza kuwashughulikia waolimchafua.

  Ridhiwani, alisema hayo jana alipozungumza na Tanzania Daima akitakiwa kueleza hatua atakazochukua baada ya muda wa siku saba aliowapa Mwenyekiti wa Demokratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbrod Slaa kupita.

  Awali, mtoto huyo wa Rais aliwataka wanasiasa hao wamwombe radhi katika kipindi cha siku saba vinginevyo angewapeleka mahakamani kwa kuwa wamemchafua pamoja na familia yake.

  Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa njia ya simu, ili kujua lini angekwenda mahakamani kuwafungulia mashtaka viongozi hao, alijibu kwa jazba kwamba jambo hilo linahusu maisha yake hivyo haoni sababu ya kufuatiliwa na vyombo vya habari.

  “Jambo la kuwafikisha wanasiasa hao mahakamani si jambo lenu, hilo ni jambo linalonihusu mimi na maisha yangu hivyo nitachokifanya nakijua mwenyewe,” alisema Ridhiwani huku akisisitiza kwamba hata alipozungumza na waandishi wa habari juma lililopita alisema lengo lake ni kuueleza umma na sio kufuatiliwa maisha yake.

  Kwa nyakati tofauti Mchungaji Mtikila na Dk. Slaa, walimtuhumu Ridhiwani kwa ukwasi huku wakiitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kumchunguza.
   
 2. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  tzs : 3, 800, 00/=
  shilingi: Shilingi milioni tatu na laki nane

  $300, 000
  usa dollars: Two hundred thousand
   
 3. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Anakula matapishi yake huyo mtoto. Alisema atawapeleka mahakamani Dr Slaa na Mtikila baada ya siku saba kupita kama hajaombwa msamaha, muda umefika na wananchi wanataka kuona ahadi aliyoitoa kama ataitimiza. Hiki kitoto kilikuwa kinatingisha kiberiti, sasa moto umeanza kumuunguza. Mahakamani atapelekwa yeye na lazima atueleze mabilioni hayo kayapata wapi, vinginevyo ni mwizi akanyee debe akakutane na akina papiii.
   
 4. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Namuonea huruma haswa atakapopelekwa yeye mahakamani na Mtikila .... maana alisema atampeleka huko yeye....
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  My hairs!
  Hii ni kali!
  Hapa hashitakiwi mtu hata ikiisha miaka 10!
  Dogo keshastuka, hataki matatizo!
  Kagundua kuwa kupima OIL kwa baadhi ya watu si jambo la mchezo!
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  swahiba... the only danger naiona hapa ni arrogance ya dogo while there are only 4 year left kwa baba kulinda familia, if it was me, i would be very careful with what i say to anyone

  Tanzania iko kwenye mapito makali sana na kauli yoyote ile ni muhimu sana hasa ukiwa kwenye limelight

  Nina story ya mtoto wa waziri wa siera leone ambaye ni rafiki yangu akisimulia yaliyomtokea, unaweza kupata kichaa... yeye amekimbilia UK

  mlio karibu, mshaurini dogo akae kimya au hata asijibu chochote kwa waandishi, silence can be the best noise one can make
   
 7. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kama hii issue inahusu maisha yake binafsi mboma alikurupuka kwenda kwenye vyombo vya habari kuwapa waliosema notisi ya siku saba? It doesn't make any sense to me.
   
 8. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,694
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hapa ndipo anaponishangaza! Aliwaita waandishi kwa moyo safi nao wakaitikia wito. Akapiga mikwara mbuzi yake na ahadi zake, waandishi wanafanya follow up, kwa nini anawakasirikia? Kama ni jambo lake na hakutaka kushirikisha watu angewafuata Dr Slaa na Mtikila awaeleze kimya kimya? Maji ukiyavulia nguo....
   
 9. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Hii kama ni kweli basi Ridhiwani kaogopa kwenda kuumbuka mahakamani, hivyo ni kweli yeye ni bilionea na wala si uongo
   
 10. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #10
  May 10, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,206
  Likes Received: 3,766
  Trophy Points: 280
  Ewe Dr Slaa na Mch Mtikila mnaongoza kundi la watz wenye uchungu na nchi hii tafadhari mfungulieni kesi huyu m.s.e.n.g.e R1 Kwani mali za watz zinaliwa na hii familia ya pale MSOGA BAGAMOYO huku baadhi ya watz wanaishi chini ya mstari wa kimataifa wa umasikini tsh 260!
   
 11. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,121
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Ha ha!so dogo alikuwa anatishia wazee wazima nyau.
   
 12. Nditu

  Nditu Member

  #12
  May 10, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumbe sasa nimegundua kwa nini familia nzima ilichangamkia kampeni za "Urahisi" wa Mzee wa kuchakachua a.k.a. Dr. wa kubumba wa chama cha Magamba! Kumbe walikuwa wakiulinda ulaji wa familia na si uchungu wa nchi.
   
 13. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Hivi inakuwaje mtoto baba yao ni rais na wewe unataka kuwa front line kwenye siasa. Kwa nini usifaidi mambo nyuma ya pazia tu . Watu wengine sijui hawana washauri.

  Sijui kwa nini huyu Riz alikimbilia kwenye mambo ya siasa. Anamuharibia baba yake na yeye mwenyewe.
  Timig yake ya kuingia kwenye siasa tena front line ni mbaya


  JK leo kawaambia mawaziri kuna mambo ukikubali kuwa waziri inabidi ukubali kuyakosa. Je hajamawambia rizwani na familia yake haya kama mtoto au familia ya wa rais kuna vitu vingine wavipotezee tu na waendele kufaidi mambo nyuma ya pazia
  bila kuwa front line
   
 14. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  mimi nilijua tu haya ndiyo yatatokea , siku saba ni kidogo sana kuchakachua mambo.
  nadhani mganga wake alimdanganya----ohoo kawambie wakuombe radhi!!!
  alikuwa naongea mpaka mate yanamtoka na misemo kibao ---makanjanja
  sasa hasubiri moto wa mtikila---- atakwenda kujifunza huo u-lawyer kwa vitendo kwa kushinda mahakamani na mtikila.
  yeye anajifnya rofa wakati hao wahandishi wa habari alikutana nao new africa hotel hiyo hela ya ukumbi nani alimlipia?
  au kawakopa.
  mwambie na mama hapo hela za hiyo saccos anayokwenda kuchangisha mabilioni USA na hatuone mahesabu yake sio muda naye hataanza kujikuna upupu
  sijui naye mkwara wake utakuwa siku ngapi?
   
 15. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 713
  Trophy Points: 280
  familia nzima yaani hawaeleweki..kuanzia baba hadi watoto.......
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  At least if he would have stayed quite it would have made more sense
   
 17. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #17
  May 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  He is still :A S-baby::A S-baby::A S-baby:....mpatieni PAMPAS
   
 18. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #18
  May 10, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni mtazamo wake lakini.
  Ni sawa tu na Rz1 alipowaita waandishi na kuwaambia kuwa anatoa siku 7 kwa Dr. Slaa na Mtikila, waandishi wanafanya follow up anawajia juu; hiyo nayo si kujishushia heshima yeye na ikulu.
   
 19. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #19
  May 10, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Alifanya kosa kubwa sana kuzungumza na wanahabari kuhusiana na swala hilo, sasa hana jinsi itabidi aende tu mahakamani na asipoenda swla hili litamtafuna yeye na familia yake.
   
 20. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Yote hiyo ni katika kuchanganyikiwa. Maji yamekuwa marefu. Like father like son....
   
Loading...