USHAURI WANGU KWA JOHN MNYIKA:
Nikiwa kama mkaazi wa Mbezi kimara ndani ya jimbo la John Mnyika, naona kuna matatizo mengi sana ambayo mengine yanaweza kutatuliwa na nguvu za mbunge wetu kwa nafasi yake. Maji ni taabu sana, katika eneo letu maji dumu la lita 2o hununuliwa na wanachi wa jimbo la Ubungo kwa Ths. 1000-1500, bei hizi pia unazikuta maeneo ya riverside ambako pia ni jimbo la ubungo, barabara mbovu, vibaka wa kutosha, vijana hawana ajira. Pia natambua na bado tunaikumbuka kampeni yake iliyokuwa imeongozwa na msemo wake wa "AMUA" yaani-Afya, Maji, Umeme, Ajira, hizi zilikuwa ahadi za Mnyika 2010. Hapa ktk jimbo la ubungo hakuna lililofanyiwa kazi na haya mnyika aliyahidi.
Nilitarajia kumskia mnyika ndani ya bunge anazungumzia mambo haya, badala yake anaenda kuzungumza mambo ambayo kwa uhakika hayagusi matatizo na ahadi zile alizokuwa anawahaidi wanaUbungo.