Ridhiwan Kikwete atikisa avuna wanachama 300 wapya Singida

Ridhiwan Kikwete atikisa avuna wanachama 300 wapya Singida

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
Ziara ya mjumbe Ridhiwani mkoa wa Singida imekuwa ya mafanikio na kuvuna wanachama 300 wapya,alivuna wanachama katika mikutano ya vijiji vya Gurungu, Sanjaranda na Itigi.

Amewaasa wanasingida kuhakikisha wanapata katiba mpya.
 
Ziara ya mjumbe ridhiwani itigi ; imekuwa ya mafanikio na kuvuna wanachama 300 wapya ;alivuna wanachama ktk mikutano ya vijiji vya gurungu, sanjaranda na itigi.

Amewaasa wana singida kuhakikisha wanapata katiba mpya
Yeye anatembelea sehemu ya kufungua vituo vya mafuta kupitia lake oil watu wanafikiri yupo kwenye ziara!!!! hana tofauti na jangili kinana anayetafuta sehemu ya kuwinda tembo
 
CCM kimekuwa chama cha vituko wanavunana wenyewe kwa wenyewe halafu wanajifanya wamevuna wanachama wapya wakati hao wanaodaiwa kuvunwa walikuwa ni wanachama wao tangu zamani ila walikuwa hawana kadi.Wanachokifanya ni kuwapa kadi ili waonekane kuwa wamevuna wanachama wapya wakati ni uwongo mtupu.
 
picture, picture othrewise mnatudanganya
 
yaani ukivalishwa kofia, kanga na fulana manake umevunwa, haya vuneni maana mmetengeneza maskini hadi wanaona bora wafaidi mavazi maana huu msimu wa baridi
 
Ameenda kutambika home, afike hadi kiomboi.....
 
Ziara ya mjumbe Ridhiwani mkoa wa Singida imekuwa ya mafanikio na kuvuna wanachama 300 wapya,alivuna wanachama katika mikutano ya vijiji vya Gurungu, Sanjaranda na Itigi.

Amewaasa wanasingida kuhakikisha wanapata katiba mpya.

Hadithi pumbaza ni kwa nufaa ya Ccm!
 
Ukitikisa mbuyu unajisifu, cha kushangaza vijana wa kileo hata wakitikisa kalio wanajisifu. Nazeeka vizuri.
 
hata kama baba yake ni wa chalinze bado ana upande wa mama yake pia


katika haraka za kujenga chama ana mfunika mshua kipindi akiwa kijana kama yeye
 
"avuna wanachama 300" kwanini isiwe 307 au 298.

Ila kwenye siasa lolote linawezekana.
 
kwa hiyo ameenda kusalimia ujombani nyie mnasema amevuna 300
 
  • Thanks
Reactions: ram
sema kavuna misukule! Chama kinakufa huku nyie mkiendekeza maigizo ya kuvunana. Tunataka daftari liandikwe upya tuwaoneshe mbivu na mbichi tu!
 
Hiyo ni technique tu za ccm,mtu ukizoea kudanganya kuna wakati unajidanganya mpaka mwenyewe .hukusikia kwamba katibu wa ccm wilaya fulani alikamatwa na kadi za chadema 200,jiulize za nini,huo ni ujanja ambao wanautumia kila anapokuja kiongozi wa ccm wa kitaifa zinachukuliwa hizo kadi wanapewa vijana ,akishaondoka zinakusanywa zinahifadhiwa vizuri ,kwa hiyo kawadanganye watoto wasiojua huo mchezo
 
Yeye anatembelea sehemu ya kufungua vituo vya mafuta kupitia lake oil watu wanafikiri yupo kwenye ziara!!!! hana tofauti na jangili kinana anayetafuta sehemu ya kuwinda tembo


Mtaishia hayo hayo.
Utafikiria mmechawikwa.
 
Yeye anatembelea sehemu ya kufungua vituo vya mafuta kupitia lake oil watu wanafikiri yupo kwenye ziara!!!! hana tofauti na jangili kinana anayetafuta sehemu ya kuwinda tembo

Mkuu naunga mkono hiyo hoja hana jipya zaidi ya vituo vyake vya mafuta kinana juz katoka singapore hajapata watu leo yeye kawatoa wapi,
N.b ndovu alivokuja huku kwetu alikimbilia pori moja ya Yaeda chini bdo nafuatilia alienda kufanyaje ma
ana kule
Wanaishi ndg zang wahazabe
 
Vijijini ni rahisi kuvuna watu nini? Mbona sijasikia mijini.
 
Back
Top Bottom