Mlata: Rais Samia ameniagiza matokeo

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
Julai 29 na 30, 2023 zilikuwa siku za fahari sana kwangu kisiasa. Nilialikwa kushiriki Ziara ya Siku mbili Wilayani Manyoni ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Bi. Martha Mlata, mwite "Mama wa Matokeo". Ahsante Mama Mlata kwa heshima hiyo.

Ziara hii ya Mwenyekiti Mlata aliyeambatana na Kamati za Siasa na Sekretarieti za Mkoa wa Singida na Wilaya ya Manyoni ambayo imenifunza mengi juu utendaji madhubuti wa kazi wa Chama chetu cha Mapinduzi, ilijikita katika maeneo makuu mawili; kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero mtambuka za wananchi katika Kata za Mwanagembe na Rungwa zilizopo Wilayani Manyoni.

Kupitia Mama Mlata nimeshuhudia Siasa mpya, zenye ubunifu na wala zisizo na chembe ya porojo bali kutoa majawabu halisi papo hapo ya kero za wananchi. Utu, busara na Upendo mithili ya mahusiano kati ya Mama kwa mwanae, ndivyo nilivyoviona kwa Bi. Mlata kwa wananchi wake. Kila kauli ya Mama Mlata ilisindikizwa na vigelegele na minong'ono ya "Mama unatosha" kutoka kwa wananchi.

Kama ambavyo Mama Mlata ziarani alivyotanguliza kauli ya kwamba ameagizwa na Mwenyekiti wake wa Taifa, Daktari Samia Suluhu Hassan kusikiliza kero na kukagua miradi, na kutolea ufumbuzi; zifuatazo ni kero zilizotolewa na wananchi na hatua alizochukua kama Chama simamizi cha Serikali iliyopo madarakani:-

KATA YA MWANAMAGEMBE - Julai 29, 2023.

1) UZINDUZI WA SHULE YA SEKONDARI
Bi. Mlata aliikagua Shule ya Sekondari ya Mwanagembe ambayo baada ya kupokea ripoti kwamba itafunguliwa mwaka kesho 2024, aliagiza Shule hiyo ifunguliwe mapema Agosti 15, 2023 kwani kwa maelezo yake haiwezekani Kata yenye wakazi elfu 18, iliyopo umbali wa Kilomita 157 kutoka Wilayani Manyoni ikose Sekondari. Aidha Bi Mlata aliongeza kwamba Shule hiyo itaepusha wanafunzi kuolewa mapema, kubakwa na hata kuliwa na wanyama wakali na pia kuepuka adha ya kusoma mbali katika Sekondari iliyopo Kata nyingine ya Rungwa iliyopo takribani kiliomita 70.

2) MGOGORO NA HIFADHI
Wananchi wamelalamika alama za mipaka ya Hifadhi ya Rungwa zimebadilishwa na kuingia katika makazi yao na pia kuwepo madini hifadhini ambayo wangependa wayatumie. Bi. Mlata ameagiza Serikali kwenda kurekebisha hiyo mipaka, na kufanya utafiti wa madini hayo ili yaanze kuchimbwa wananchi wafaidike maana ni raslimali zao.

3) MICHEZO
Vijana wameomba kuanzishwa Kombe. Bi. Mlata ameagiza Kombe kuanzishwa

haraka na liitwe "Mama Samia Cup" ambapo mshindi wa kwanza atapatiwa Shilingi laki 5 na Mbunge wa Manyoni Magharibi, Mhe. Masare, Mshindi pili atapatiwa laki 3 na Diwani Dule na mshindi wa Tatu ni laki moja na nusu ambayo Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mwanagembe atatoa.

Aidha Mwenyekiti CCM Wilaya ya Manyoni ndugu Jumanne atatoa kreti 5 za soda na yeye Mwenyekiti Mlata ataleta Kombe kwa Mshindi siku za Ukomo wa mashindano hayo .

4) MAJI
Maji yamelalamikiwa machafu kwamba hayawezi hata kuivisha maharage. Mwenyekiti Mlata amewaambia gari tayari lipo la kuchimba visima, na hivyo wananchi waondoe hofu punde utekelezaji utaanza.

5) UMEME
Wananchi wamelalamika Umeme kuwaka tu barabarani, pembezoni nguzo zipo ila Umeme hakuna. Mhe. Mlata ameagiza TANESCO waende kufanya "wiring" kabla ya wiki hii haijaisha na kuwasha Umeme.

6) AFYA
Bi. Martha amewaasa wananchi kuacha imani potofu wanaodai kwamba wauguzi wamezidi kwa "makusudi" kuwafanyia upasuaji wake zao kipindi cha kujifungua. Mlata amewaelimisha kwamba "Operation" hufanywa kwa sababu za kitabibu ikiwemo mama mjamzito kuwa na nyonga ndogo na kichanga tumboni kuzidi uzito wa kilo 3 na sio makusudi ya madaktari, hivyo wawaamini wauguzi.

7) KITUO CHA POLISI
Bi. Mlata ameahidi anafuatilia na kuhakikisha kinaletwa mapema iwezekanavyo.

KATA YA RUNGWA - Julai 30, 2023.

1) SHINA NAMBA MOJA RUNGWA
Katika Kata hii ya Rungwa, Mwenyekiti Mlata kabla ya kwenda kutembelea miradi na kuzungumza na wananchi kwenye Mkutano wa Hadhara alitembea Shina "namba moja" Rungwa ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza wanachama kuwa na kadi mpya za kieletroniki ambazo zina huduma lukuki na muhimu kwa maendeleo.

"Kadi ya kieletroniki ya Chama cha Mapinduzi inaweza kusababisha kupatiwa mkopo benki. Balozi wa Shina na wanachama hakikisheni mnazo na mnashawishi wanachama wapya wawe nazo." Alisema Mwenyekiti Mlata

2) KITUO CHA AFYA - RUNGWA
Mama Mlata baada ya kutembelea ujenzi wa Kituo cha afya cha Rungwa ameagiza kituo hicho kijengewe Fensi kukitofautisha na makazi ya watu, kupandwa miti na pia kuahidi anaenda kuisimamia Serikali kuongeza watumishi na kuwajengea nyumba za kuishi.

3) GARI LA WAGONJWA
Mlata ameagiza gari bovu la wagonjwa kuondolewa mara moja na badala yake kuletwa gari lingine zima wakati hilo bovu linatengenezwa ili kuhakikisha wananachi wanapata huduma za afya kwa wakati kwani Rungwe na mbali hadi kufika hospitali za Wilaya na Mkoa.

4) STENDI
Katika hatua nyingine Mwenyekiti Mlata amegoma kuzindua stendi ya magari ya Rungwa hadi pale ambapo huduma muhimu na ujenzi kukamilika wa stendi hiyo muhimu itakayoonganisha Kata za Wilaya ya Manyoni na Mkoa wa Mbeya.

5) BWAWA LA RUNGWA
Mwenyekiti baada ya kulitembelea Bwawa hili ambalo lina wanyama wengi aina ya vifaru, ameagiza Halmashauri ya Itigi kuona namna ya kuyatumia maji yake kwa matumizi ya kibindamu na kilimo cha umwagiliaji.

6) KILIMO
Wananchi wa Rungwa wamelalamika kukatazwa kulima mazao ya biashara ikiwemo pamba kwa kuhofia wadudu waitwao "wadudu wekundu" Licha ya kuwa na hamu ya kujihusisha na kilimo hicho.

"Naagiza Afisa Kilimo aje aongee nanyi kuhusu mazao gani ya biashara yanafaa katika Kata yenu, na pia naagiza Serikali kuchukua hatua za makusudi kudhibiti mdudu mwekundu." Mwenyekiti Mlata.

7) AJIRA
Mwenyekiti Mlata ametoa maelekezo kwa Halmashauri ya Itigi kuhakikisha kila fursa za ajira zikitolewa, vijana-wakazi wenye Sifa stahiki wawe kipaumbele na wazidi idadi kuliko wageni.

"Haiwezekani hata kazi za sensa, vijana wenyeji muwaache, muwaajiri vijana wa kutoka mbali".. Alihitimisha Mwenyekiti Mlata.

Kwa hakika Mama Mlata, ni Mama wa Matokeo.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

KAZI IENDELEE

Suphian Juma Nkuwi,

Kada-CCM

Singida

Julai 30, 2023

IMG_20230731_185355_192.jpg
DSC_0059.JPG
IMG_20230731_185429_382.jpg
IMG_20230731_185132_759.jpg
DSC_0068.JPG
 
View attachment 2704026View attachment 2704028View attachment 2704029View attachment 2704032View attachment 2704035
Kumbe Musiba alikuwa sahihi kusema wewe ni upinde, umekidhi vigezo vyote
JamiiForums1049284733.jpg
JamiiForums1438962745.jpg
 
We na huyo Mlata wako hebu mtupishe. Kwa hiyo kakuita kwenye safari hiyo ili uje uandike upupu huu humu JF?
Nenda kamwambie JF ni "Home of great thinkers" hivyo hakuna mwenye muda na hizo Sanaa zenu za 3rd grade
@suphian Juma ni Shoga kutoka Singida, alikuwa Mfuasi wa Kigenge cha Yuda (ACT)
Kwa sasa anajipendekeza Kwa Hangaya ili Amulikwe zaidi na Ma Basha huko Serikalini
 
Back
Top Bottom