Revealed: Operation Bomoa CHADEMA Mbeya, Mpango Mzima Episode 1.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Revealed: Operation Bomoa CHADEMA Mbeya, Mpango Mzima Episode 1..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdau, Apr 23, 2011.

 1. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  [FONT=&quot]Mambo yameanza kuwa hadharani kuhusu Shitambala, aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya…[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Mkakati ulisukwa na JK mwenyewe kupitia watu wanne ambapo watatu ni wakazi wa mkoa wa Mbeya na mmoja anatoka nje ya Mbeya, rafiki wa Shitambala wa muda mrefu…[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Mtu wa kwanza ni Mwaikela ambaye ni mfanyabiashara wa madini mkoani Mbeya…Mwaikela ni moja kati ya watu waliokua kwenye orodha ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya ambayo alikabidhiwa JK, surprisingly, Mwaikela kwa sasa ni rafiki mkubwa sana wa JK.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Mwaikela ndiye aliyemuunganisha Shitambala na JK, pia alimuunganisha na Jenerari Mboma, mtu wa pili katika hili gemu..[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Mboma aliweza kumshawishi Shitambala aharibu uchaguzi wa Mbeya vijijini, kwa ahadi ya kwamba atalichukua jimbo 2015 kupitia CCM…[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Baada ya hapo, JK akamuomba mtu wa tatu, Mwandosya ili akamfikishie ujumbe Shitambala pamoja na viongozi wengine wa CHADEMA mkoani Mbeya jambo ambalo walifanikwa kwani hata katibu wa mkoa wa CHADEMA nae ni miongoni mwa watu ambao wanaendelea kunufaika na pesa za hao mafisadi…Katibu wa mkoa wa CHADEMA ambae nae ni moja kati ya viongozi wanaoendelea kutumika; ataondoka au atabaki ndani ya chama lakini kwa ajili ya kazi maalumu…[/FONT]
  [FONT=&quot](CHADEMA SHOULD TAKE A NOTE ON THIS!!!). Mkakati mwingine walionao ni pamoja na kuwanunua vijana mkoani Mbeya ili kuvunja ngome ya CHADEMA ambayo imewekeza kwa kiasi kikubwa kwa vijana hao, hasa wa vyuo vikuu…[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Mtu wa nne katika huu mpango ni waziri kijana katika serikali ya JK, jina litafutia soon…[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]NB:[/FONT]
  [FONT=&quot]Mwaikela, mhitimu wa darasa la saba, ana mpango wa kugombea ubunge jimbo la Mbeya Mjini na anadai kufikia mwaka 2015 atakuwa amepata digrii!!! Pesa kutoka CCM zinapitia kwa Mwaikela na baadae kuwafikia viongozi wa CHADEMA.. Wengi wangekua tayari wamehama tatizo, Shitambala aliwazidi spidi ya kula hizo pesa...[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Duu!!! Mwasalipa holowane.
   
 3. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Tunasafari ndefu kuelekea Tanzania mpya......
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Apr 23, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280
  Mdau are you sure?

  Leteni ushabiki kwenye mambo mengine mengi tu ila siasa za Mbeya ni ngumu sana na ile dhana yangu ya siasa ni mchezo ndio inapaswa kuingilia kati

  Fanya assignment yako upya ( Hints

  1. Angalia historia ya jimbo la mbeya mjini na Wasafwa
  2. Angalia uhusiano wa JK na Mwandosya
  3. Angalia uhusioano wa JK na Mwakipesile
  4. Angalia nguvu ya Mwandosya kwenye siasa za Mbeya
  5. Angalia uadui wa Mwakyembe na Mwakipesile
  6. Angalia mwitikio hasi wa Sugu kuwa mbunge kwa jamii ya kisomi ya Mbeya

  Ukifanya assignment utagundu akuwa

  Nguvu ya chadema mbeya ni kubwa endapo tu watachea karata ; kwanza ni kutoonyesha uadui kwa mwandosya, pili ni kujikita kwa wasafwa!

  Ninaposema siasa za pale ngumu kwani zina ukabila sana, Wanyakyusa hawana nguvu na jimbo la mbeya mjini kama inavyodhaniwa, wasafwa wana nguvu na kulitokea uasi wa jamii yao na kuchokwa CCM.

  Chadema has only opportunity kuigawa CCM vipande vipande mbeya ila sio kwa siasa hizi za kukurupuka.

  Sugu hatakiwi Mbeya kwa sasa na ubunge wwake utakuwa wa shinda sana, wanaoweza kukuambia haya ni wale ambao mbeya mjini ni kwetu. Achaneni na Shitambala au Kitambala,

  Sugu you can smoothen your position kwa kuangalia na kukutana na wazee wa hapo mjini, ninajua ninachokisema.

  Ukabila unaiua Mbeya mjini ! aibu!
   
 5. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mkuu nahisi unakaa Mby,ulichoongea ni ukweli kwa 95%.mm ni mkazi wa Mby,na mwanachama wa Cdm,mpango mzima uko hivyo na wanaotakiwa ni zaid ya wa2 sita,ktk hao niwe wazi nna mashaka na katibu wa mkoa,mengine tunashindwa kuongea humu,MUNGU IBARIKI CDM,MUNGu ibariki Mby,
   
 6. V

  Vipaji Senior Member

  #6
  Apr 23, 2011
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana kabisa na Waberoya, siasa za Mbeya ni tofauti sana na Mikoa mingine ya Tanganyika. Jambo la Msingi ni Uongozi wa juu wa Chadema kupiga kambi Mara kwa mara jimbo la Mbeya Mjini na majimbo mengine mkoani Mbeya la kuwaelimisha wananchi kuhusu na sio kuhubiri jaziba. Na watu Kama Lema wanahitajika vyuoni Mbeya kutibu na kuibomoa CCM.
   
 7. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  1. Influence ya Mwandosya inatoka wapi kwenye jamii ya wasafwa? Nahisi you are not consistent.
  2. Bifu la Mwakyembe (imfact na Mwandosya kwa upande mmoja) dhidi ya Mwakipesile lina impact gani kwa siasa za Mbeya Mjini?
  3. Uhusiano wa JK na Mwandosya unasemwa kuwa unaimarika (kwakuwa Mwandosya anataka urais na hana njia nyingine bali kujipendekeza kwa Mwenyekiti) uhusiano huo unaotajwa kuimarika una nafasi gani kwa siasa za Mbeya hasa ukizingatia kuwa M/kiti wa CCM mkoa wa Mbeya hawaivi kabisa na Mwandosya?
  4. Shitambala ana mvuto gani kwa wana mbeya yeye kama yeye?
  5. Nini mwitikio wa wakazi wa Mbeya kwa Chadema?
  Maswali haya yakijibiwa kwa usahihi naamini yanaweza kuleta majibu kama ni kweli hiyo OBOCHA( Operation bomoa chadema) ipo na kama itafanikiwa
   
 8. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  usipo-comment kuhusu udini, basi uta-comment kuhusu ukabila.

  But despite all that, Chadema will prevail. We support Chadema, We love Chadema, We pray to God that Chadema goes through all these bumps, drifts and ditches.

  We Stay United.

  We stay Strong.

  My 2 year old boy is purely Chademalized. How do you say about that?

  P1100392.JPG
   
 9. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mwaka huu tutasikia mengi tena sana! Mimi nasubiri movie ya RA, EL na AC.
   
 10. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Safari ni ndefu kuifikia demokrasia ya kweli..huu ni umafia sasa. Lakini pia hizi njaa hizi..
   
 11. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kwani kuna mtu anafanya siasa Tanzania Zanzibar au Tanzania Tanganyika kwa nia njema ya Taifa? tusijidanganye, woooote pesa tu! maslahi ya ndo siri ya kweli ya sababu.
   
 12. E. J. Magarinza

  E. J. Magarinza Member

  #12
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tunaimani na CHADEMA oya..... oya........ oya..............!!! Tunakipenda chama na si mtu.
   
 13. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,963
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 180
  This is hanky panky stori za vikao vya kimpumu, kwamba jamaa wa darasa la saba wakarub shoulders na JK na Mwandosya? Tell it to the birds!
  Nilikuwa Mbeya majuzi na wengi wamesitukia mkoa kukosa mgawo wa viti maalum pamoja na kujitokeza kwa wingi kukishabikia chama wasichokifahau.
  THAT IS THE ISSUE na msipindishe nepotism iliyo kubuhu CDM.
   
 14. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu huwa unanichekesha sana pale ambapo uko tayari kuongea uongo ili kusisitiza hoja yako!!!!!!!!!!!!! You have contradicted urself several times.
   
 15. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mzito Kabwela maswali yako yanaonyesha wewe huzifahamu siasa za Mbeya kama Waberyoya na hata kama tutajibu maswali yako hayawezi kuiongezea CDM lolote. Lakini kama chama chochote kinataka kuandaa mkakati wa jimbo la Mbeya kwa 2015 basi mkakati huo lazima uhakikishe kuwa yote yaliyoandikwa na Waberyoya hapo juu yanajibiwa. Usichukue for granted kwamba eti Shitambala amekwisha kwa sababu ya kurudi CCM au ukaiamulia CCM ya 2015 kwa kaushindi ka Sugu ka mwaka 2010, utakuwa unajidanganya. Hao wakazi wa Mbeya mjini ambao ni wasafwa hata wakati wa chama kimoja kwenye miaka ya 1980 waliwahi kumnyima mbunge wa kabila lao Bwana Yilanga na kumpa Mwamfupe kutokana na kwamba Yilanga alikuwa amewakwaza. Kwa hiyo usidhani kuwa eti wanampenda Sugu, No bali walikuwa wamemchoka Mpesya that is all na ndiyo maana wakapiga kura za CHUKI
   
 16. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180


  [FONT=&quot][/FONT] [FONT=&quot]Waberoya,[/FONT]
  [FONT=&quot]CCM wamegundua ishu ya ukabila haina nguvu tena kwani Mbeya kwa sasa inakaliwa na makabila mengi na hata wengine ni viongozi wa kisiasa; mfano meya wa jiji la Mbeya ni Msangu. Kama ajenda ya ukabila ingekua na uzito basi meya angekua Mnyakyusa au Msafwa, Na hata madiwani wengine wengi ni wa kutoka makabila nje ya mkoa wa Mbeya, angalia hawa: Diwani wa kata ya Ruanda mzee Kilato ni mwenyeji wa Iringa/Njombe…pia marehemu Shayo alikua ni diwani kata ya Majengo, ambapo panasubiriwa uchaguzi mdogo, huyu alikua ni Mchaga…..orodha ni ndefu wanaofikiri suala la ukabila lina nguvu Mbeya wamepotea…..siasa za ukabila zimebaki kwa watu wasiokwenda shule na wanaCCM hasa wa nje ya Mbeya na viongozi wakuu ambao ukabila na udini ni mitaji yao ya kila siku……………..[/FONT]
  [FONT=&quot]Kama Mwandosya anakubalika kwanini na yeye alizomewa wakati anamsindikiza Shitambala au kama ulivyosema Kitambala pale Uyole; mahali ambapo anakotoka na alikozaliwa Shitambala…Bado nasisistiza ishu sio ukabila zaidi hapo kilichoangaliwa na Shitambala ni pesa na si zinatoka kwa nani, kwa sababu hata aliyemkabidhi ni Mnyakyusa…zaidi, katika hawa watu wane waliocheza hili gemu wote makabila tofauti, Mmoja ni Mmalila, UNAMJUA!!![/FONT]
  [FONT=&quot]Ushauri kwa CHADEMA si kuigawa CCM, waigawe kwa misingi ipi!!! Ya ukabila amabyo ni siasa za maji taka!!???…. CCM imeanguka Mbeya kwa sababu ya migawanyiko na mbinu kama hizo kwa upande wao wenyewe, NUKTA![/FONT]
  [FONT=&quot]CHADEMA endeleeni kusimamia masuala ya msingi ya nchi kama ambavo mmekua mkifanya siku zote mtazidi kuungwa mkono na umma wa Watanzania uliokwishachoka na CCM na serikali yake..……….[/FONT]
  [FONT=&quot]Ushauri wangu kwa Sugu pia, endelea kuimarisha nguvu ya chama chako mkoani Mbeya, na sio siasa za KIBONGO FLEVA, wameanza kuchoka, nadhani unanielewa… [/FONT]
   
 17. b

  buckreef JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtu anavuruga uchaguzi wa mwaka huu ambao anaweza akashinda ili ashinde jimbo hilo miaka mitano ijayo? I am lost, it doesn't make any sense.

  Waberoya kwa maandishi yako nafikiri unazifahamu vizuri siasa za Mbeya.

  Kuna mabadiliko makubwa sana kwenye siasa za Mbeya ambayo yanaweza kuisaidia CCM tofauti na mwaka 2010. Baadhi ya mabadiliko yaliyotokea ni:

  Ghafla kunaonekana ukaribu mkubwa kati ya Prof. Mwandosya na JK. Kumbuka huko nyuma kulikuwa na hisia ya kwamba JK anamchukia prof. Mwandosya.

  Dr. Mwakyembe kuteuliwa kuwa naibu waziri. Kulikuwa na hisia kubwa Mbeya kwamba Dr. Mwakyembe hapendwi na JK na anakwamishwa na Mwakipesile. Baada ya kuteuliwa hawezi tena kusema rais anamchukia au Mkuu wa mkoa anamkwamisha. Hii tayari inaondoa sababu moja wapo ya CCM kuchukiwa Mbeya.

  Uhusiano wa prof. Mwandosya na Dr. Mwakyembe ni kama unafifia. Kuna dalili wakawa makundi tofauti kwenye urais CCM 2015. Inaonekana Dr. Mwakyembe yuko karibu zaidi na Sitta kuliko prof. Mwandosya. Hili Mwandosya analifahamu na tayari mmomonyoko unaanza hapo.

  Dr. Mwakyembe yuko karibu sana na CHADEMA taifa ila hakuwa na uhusiano mzuri na CHADEMA mkoa; alikuwa haelewani na Shitambala na Makata. Prof. Mwandosya hana mpango na CHADEMA, anapingana na CCM ndani kwa ndani, hana plan B ya kwenda CHADEMA.

  Dr. Slaa alimsaliti Makata kwenye uchaguzi wa Kyela. Alimkaanga waziwazi jukwaani na hata hakuongozana naye kwenye msafara ndani ya helikopta na kumfanya Makata achelewe mkutanoni. Hivyo CCM wakimzengea tu Makata inaweza kuwa rahisi sana kumchukua.

  Makosa ya CHADEAM kutokuchagua hata mwanamke mmoja kutoka Mbeya kwenye viti maalum.

  Adui wa CCM kwa Mbeya kwasasa ni UFISADI. Wakifanikiwa kujivua gamba kama wanavyodai, CHADEMA imekwisha Mbeya. Labda waje na strategies zingine. Ni muhimu sana kwa Sugu kutokuonyesha chuki ya waziwazi kwa prof. Mwandosya. Kikubwa ashirikiane naye na hiyo itamjenga kwa wananchi wote Mbeya na akifanikiwa kufanya kazi nzuri basi ataweza kurudi. Ila akitengeneza uadui na prof. Mwandosya, atakuwa amejimaliza.
   
 18. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Shitambala hana ushawishi wowote kwa siasa za Mbeya mjini. Ni kweli kwamba siasa za Mbeya hazitabiriki na lolote linawezatokea kwa wakati wowote. Nina rafiki yangu ambae alikuwa ni mgombea udiwani kata mojawapo ya mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema na alikosa. Nilisafiri nae kwenye gari na kwa nia nzuri tu alizungumza mengi na pia aligusia tabia ya Sugu na mimi niligundua hilo linaweza kuwa tatizo. Alisema Sugu anahusudu sana kujitenga na hili analifanya ili apate nafasi ya kujirusha. Aliendelea kuwa tatizo kubwa kwa Sugu ni akiwa na cash mfukoni, kwani ikiwa kinyume chake ni mzuri sana kimahusiano na jamii. Na aliniambia saa hizi ni jioni ilikuwa kama saa moja na nusu akasema, nimpigie simu sasa kama hutamkuta baa kwenye makelele mengi? Sikumshauri apige simu ila nilijifunza jambo fulani. Pamoja na kwamba Chedema iko juu sana mbeya mjini na ni chama kinachopendwa na makundi yote, binafsi ningemshauri Sugu ajaribu kuwa karibu na watu kama kina mnyika na kujifunza kutoka kwao. Nimepita sehemu nyingi za Dar na hasa jimbo la ubongo, mnyika anazungumzwa kwa sifa nzuri hasa mahusiano yake binafsi na watu na makundi tofauti. Nilishangaa hata kundi la mjahidina kwenye maeneo yao wakimtulea mfano kwamba ni mtu anaejua kuongea na watu na kuwa sehemu katika shida zao.
  Ukiachana na Dar, Mbeya bana mtu asikudanganye wale watu wemekaa kimaslahi kuliko mkoa mwingine. Watauza ngozi za watu, vichwa vyenye upaa hata biashara ya mimba changa ipo ili tu wapate pesa. Hivyo kuambiwa kitambala kauza utu wake ili apewe chapaa, hiyo ni asili yao sawa na msemo 'jasiri haachi asili'
  .
   
 19. f

  fundimchundo Senior Member

  #19
  Apr 23, 2011
  Joined: Jul 23, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Watu wa Mbeya ya sasa, kama nchi nzima ilivyo, wamevuka hatua ya kupigia kura watu binafsi.
  Wanapigia kura elimu ya watoto wao.
  Wanapigia kura hali zao za kiuchumi.
  Wanapigia kura ubora wa huduma za afya zao.
  Kimsingi, wanapigia kura matumaini ya kuishi maisha bora na wala siyo majina na makabila.
  Mjadala wa ukabila kwa Tanzania ya sasa ambayo vijana hawana kazi wala matumaini ya maisha yao unashangaza!
   
 20. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,348
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  Ndaga fijo nkamu gwangu.
  Kuna thread nlishawahi kuiona hapa Jf zamani kuwa CCM imepandikiza vijana kumchafua Joseph Mbilinyi Sugu mbunge wa Mbeya mjini. Muda si muda mjinga Jafarai akaanza kudai eti Sugu kaivunja ndoa ya Jafarai na Shyrose
   
Loading...