Nimesoma kwa umakini posts zote zilizopita, nimebaini kuwa ''mdau'' anazijua na bila shaka anazishiriki siasa za Mbeya. Nazifahamu kiasi kikubwa sana siasa za Mbeya naungana 100% na hoja za mdau. Pamoja na hayo nataka nichangie kuhusu baadhi ya mambo kama ifuatavyo:
Mr. Mwaikela: Kuna watu wanashangaa eti std 7 kuwa karibu na JK. Mwaikela hajaanza ''kugusana mabega'' na JK- yeye ni mzoefu na marais alianza na Dr. Salmini Juma na mwanaye- mwisho wake wakamfunga jela huko ZNZ
Umaarufu wa Mwaikela ulianzia wakati wa Aden Mwamunyange- Ex msemaji wa polisi, pia alikuwa na mahusiano ya karibu sana na Mwansasu ex CFO wa jeshi la polisi. Kwa kutumia mwanya wa vigogo hao ameendelea kuwa karibu na viongozi hata wa polisi wa sasa- hivyo they guy is untouchable. Kimsingi yeye ndio hutake care family problems nyingi za viongozi wengi wa Mby walioko Dar kama misiba, harusi etc.
Sitashangaa sana yy kujiunga na Mwandosya, maana ni majirani sana kama CRDB Lumumba na CCM lumumba, pia Mwandosya kagundua ili apate urais lazima apige magoti kwa JK. Na kufanya hivyo lazima ajiunge na atumike na watu walio jirani na JK kama Mwaikela.
Mwaikela is a hard worker, mjasiliamali, hana majivuno anaongea na kila mtu - ia yeye yupo kibiashara zaidi, yupo tayari kufanya lolote (kumpiga bei Shitambala) kwa CCM ili mambo yake yawe sawa. Mwaikela ni bingwa wa kuuza dhahabu, na vijana wake siku za nyuma wakiiuza '' sana zile ''Kakumba'' hivyo haishangazi kuwauzia CCM shitambala (kakumba) kwa bei kubwa wakati hamna kitu pale.
Shitambala:
Unaweza kurejea posts zangu za nyuma baada ya ule uchaguzi wa mwanzo kujaza nafasi ya Nyaulawa, niliwatahadharisha CDM kuwa Shita ni ''malaya'' wa kisiasa hata umpe nini, umridhishe namna gani atatoka nje ya ndoa tu kwa visenti kidogo kuliko utakavyompa na mwishowe atakuacha. Yeye mwenyewe hajawahi kukanusha kuuza ushindi, ila ukimuuliza anasema alitumia pesa zake na kujitolea sana CDM. Kwahiyo wale wanomtetea kuwa hakuuza ubunge hawamtendei haki Shita; maaana yeye hajawahi kukanusha.
Shitambala aliuza ubunge mara mbili hiyo hata nafsi yake inamsuta- kama wewe ni great thinker huna hana haja ya kujiuliza- unataka ushahidi upi? angalia circumstancial evidence kama huamini tunachosema.
Kimsingi siasa za Mbeya mjini ni sawa na Kyela na Chunya. Mbeya mjini kwa asili wanapenda upinzani bila kujali mgombea ni nani. Uchaguzi uliopita yule mzee Kisonga sio maarufu kabisa Mby lakini alitoa upinzani mkubwa sana kwa Mpesya ingawa aligombea kwa ''moribund party'' TLP. Rejea vuguvugu la Mrema Mbeya 1995 hadi NCCR wakashinda Mbeya mjini. Ukiacha uchaguzi wa mwaka 2010, wapinzani wamekuwa wakishinda majimbo ya Chunya na Kyela isingekuwa kuchakachua.
CDM bado wana nafasi kama chama watamua kuelekeza nguvu Mbeya, sugu bado hajakomaa katika kuendesha siasa baada ya uchaguzi ambapo mihemuko na hamasa zinakuwa zimepoa. CDM taifa lazima wahakikishe wanatupia jicho Mbeya mara kwa mara. Ikiwezekana mikakati ya kina Lema (kuhusu Elimu) akajaribu kuikopi na kupesti.
Mwandosya na Mwakyembe kwa sasa hawezi kuiva maana'' the friend of your enemy is your enemy. Ukaribu wa Prof na JK unampa mashaka DR ambaye kimsingi ni paka na panya na JK. Mbaya mkubwa wa Prof. kimsingi hakuwa JK bali Lowasa kwa sababu ya Urais. isitoshe Prof na Dr wote wanajiona ni president material
The NEXT time bomb kwa CDM ni Prof Safari, huyu kajiunga akiwa na TORs kabisa- kumbuka haya maneno yangu Mungu akitupa uhai