Revealed: Operation Bomoa CHADEMA Mbeya, Mpango Mzima Episode 1..

Mambo yote hayo ndiyo yanayomaanisha siasa. Pamoja na mambo yote hayo, CHADEMA wanaonekana kuzichanga vizuri karata zao tofauti na CCM ambao wamekalia kujiaminisha kuwa wao ni chama kinachopendwa na watu wengi bila wao kuonyesha kuwa wako karibu na wananchi na wanawapenda watu masikini (90% ya watanzania). Ubinafsi na unafiki wa viongozi wa CCM ndiyo chanzo cha kukiua chama chao taratibu (Killing the party slowly but surely).

Mkuu mtu ukiwa muflisi wa mawazo ndo una ongea kama ulivyopost.
10% ya hao unawainisha kuwa si masikini(matajiri) wanatoka chama kipi? Na kama Chadema ilipanga karata zake vizuri inakuwaje basi bado wako upinzani.
 
Duh...............

Mwaikela(George) anauza dawa za kulevya!!!!!!............hii kali...

Thought George ana mpango wa kugombea jimbo la Songwe.............kumbe Mbeya mjini!!!!!

Hivi Songwe ndio kwa huyu naibu waziri wa Elimu>>>>>>
 
  1. Shitambala alivuruga uchaguzi makusudi kwa sababu zifuatazo.......
(i) Tayari alikua ameanza kusaliti CHADEMA tangu awali, kwa mipango ya chinichini na baadhi ya vigogo wa CCM...

(ii) Uchaguzi wa 2010 alipewa pesa, milioni 17 cash si millioni 600 kama ilivyodhaniwa...aliyemkabidhi ni bwana Mwaikela, baada ya Mboma kumuomba ampishe mbunge wa sasa Mwanjale aendelee, mbunge huyu pia ni binamu wa Shitambala, kumbuka yaliyotokea 2008..(UMEWAHI KUSIKIA MWANASHERIA ANAJIAPISHA MWENYEWE!!??)
]


Hivi mkuu inakuingia akilini Shitambala,Wakili wa Kujitegema, ahongwe Million 17 tu na akubali kuyaacha marupurupu ya Ubunge?hivi unadhani Shitambala hakujua kuwa kuna Million 90 zitakazopatikana soon baada ya kwenda Bungeni?ongeza na mishahara kwa miaka 5 yote??think..

Pili hivi inakuingia akilini G.Mboma aliyedondoshwa na kuaibishwa kwenye kura za maoni na Mch Mwanjale atoe fedha mfukoni mwake kwa ajili ya kuulinda ulaji wa Mwanjale??think..

Tatu, suala la kutosimamisha wagombea kwenye baadhi ya kata ambazo waliopo wanamuunga mkono ni technics tu za kisiasa,ili linafanyika sana sehemu nyingi,ata Mpanda Arfi aligoma kabisa Chadema kuweka mgombea mbunge kwenye jimbo la Waziri Mkuu Pinda,alisema yupo tayari kurudisha kadi kuliko kushuhudia hilo likifanyika na hili lilimsaidia kisiasa.

Nne,kwa geographia ya Mbeya Vijijini na ukizingatia kuwa Chadema hakikuwa na fungu la kutosha kwa ajili ya kuwalipa wasimamizi wa Uchaguzi,ilikuwa ni vigumu sana kwa Shitambala kuweka wasimamizi kwenye vijiji vyote,aliitaji awe supported na mtu kama Rostam ili aweze kufanikisha hilo,ata Mbeya Mjini watu wengi walijitolea kufanya na maeneo ya karibu kama Mbalizi bila kulipwa,muamko wa watu wa vijijini vya ndani sio mkubwa na ukiongeza na umaskini,na hivyo kuwasafirisha watu kwa malori kwenda vijiji vyote vya Wilaya ya Mbeya Vijijini,kuwalisha na kuwapa posho sio shughuli ndogo.
 
Mkuu mtu ukiwa muflisi wa mawazo ndo una ongea kama ulivyopost.
10% ya hao unawainisha kuwa si masikini(matajiri) wanatoka chama kipi? Na kama Chadema ilipanga karata zake vizuri inakuwaje basi bado wako upinzani.

Upo sahihi kabisa mkuu...asilimia 90% ya Watanzania [ikiwa ni pamoja na wewe] wapo CCM...wanasumbuliwa na shida, tabu na umaskini uliotopea wa kiuchumi na kiakili, kwao wao hali hii ngumu inayowakabili ni mpango tu wa mwenyezi Mungu!!! Asilimia 10% ndio wapo CHADEMA [kwa mujibu wa uelewa wako]......hawa ni matajiri wa kihali na mali, na ni wachache ndio maana CCM bado ipo madarakani...NADHANI NIPO SAHIHI!!
 
Hivi mkuu inakuingia akilini Shitambala,Wakili wa Kujitegema ahongwe Million 17 tu na akubali kuyaacha marupurupu ya Ubunge??unadhani Shitambala hakujua kuwa kuna Million 90 zitakazopatikana soon baada ya kwenda Bungeni?think..

Pili inakuingia akilini Mboma aliyedondoshwa na kuaibishwa na Mwanjala atoe fedha mfukoni mwake kwa ajili ya kuulinda ulaji wa Mwanjala??think..

1. Haiingii akilini kabisa mkuu....inayoingia akilini KWAKO ni kitendo cha Shitambala, LLM, mwanasheria maarufu wa kujitegemea KUJIAPISHA MWENYEWE katika uchaguzi mdogo wa 2008....

2. Read btn the lines, Mboma hakutoa fedha mfukoni mwake, alikua ni mmoja wa facilitators....
 
ndaga fijo nkamu gwangu.
Kuna thread nlishawahi kuiona hapa jf zamani kuwa ccm imepandikiza vijana kumchafua joseph mbilinyi sugu mbunge wa mbeya mjini. Muda si muda mjinga jafarai akaanza kudai eti sugu kaivunja ndoa ya jafarai na shyrose
kumbe walifunga ndoa!!!!!!!!
 
1. Haiingii akilini kabisa mkuu....inayoingia akilini KWAKO ni kitendo cha Shitambala, LLM, mwanasheria maarufu wa kujitegemea KUJIAPISHA MWENYEWE katika uchaguzi mdogo wa 2008....

2. Read btn the lines, Mboma hakutoa fedha mfukoni mwake, alikua ni mmoja wa facilitators....

Taratibu Mkuu!!

1.Kwa taarifa yako, Sambwee Shitambala HAKUJIAPISHA MWENYEWE bali aliapishwa na WAKILI EVARIST MARTIN MASHIBA, nakushauri zihakiki kwanza data zako kabla ya kuzipost humu.

2. G.Mboma afacilitate fedha za kulinda kitumbua cha mtu aliyemuabisha nyumbani kwake?hivi unaifahamu ego ya G.Mboma?hivi unadhani Million 17 ni fedha ya kumfanya mtu kama Shitambala akubali kuyaacha mafao yoote ambayo angeyapata kwenye Ubunge kwa miaka mitano?

Nikwambie tu, Shitambala aliutafuta Ubunge kwa nguvu zake zote,alijitahidi kadri alivyoweza,lakini mwamko wa wananchi wa jimbo la Mbeya Vijijni kwenye siasa bado ni mdogo sana ukiondoa maeneo ya yaliyopo kwenye Highway, hivyo pamoja na kushinda maeneo ya mijini,CCM wakammaliza maeneo ya vijijini.

Hivyo baada ya kushindwa na kutafakari mazingira yanayomkabili kisiasa na gharama zake,akaona ni rahisi kwake kufanikisha malengo yake ya kisiasa ndani ya CCM kuliko ndani ya CDM.
 
Cha kufanya,Joseph aka Sugu asijiingize katika mgogoro wowote na wale wazee wa mbeya,sanasana azingatie ahadi alizozitoa na kuzitekeleza.vilevile ajitahidi kuondoa ukabila.akifanya hivyo 2015 hana mpizani yoyote bila kujali chama kikuu cha upinzani mbeya ccm.mimi naamini shitambala siyo kila kitu mbeya.
 
Taratibu Mkuu!!

Kwa taarifa yako, Sambwee Shitambala HAKUJIAPISHA MWENYEWE bali aliapishwa na WAKILI EVARIST MARTIN MASHIBA, nakushauri zihakiki kwanza data kabla ya kuzipost humu.

G.Mboma afacilitate fedha za kulinda kitumbua cha mtu aliyemuabisha nyumbani kwake?hivi unaifahamu ego ya G.Mboma?

Hizi siasa za majitaka mbaya sana. Mtu anaandika utafikiri anajua ukweli kumbe ni maneno ya vijiweni. Suala la Shitambala lilishajadiliwa sana hapa. Jamaa aliangushwa na ujuaji wa wanasheria kwamba wanajua maana ya kiapo na hakimu au mwanasheia mwingine anaweza kumwapisha.

Kweli mgombea ataachia ubunge ili aje awe mbunge miaka mitano ijayo?

Ndio maana Shitambala amewakimbia maana walianza kumchafua mno.
 
Yap.............Wazazi wa Mwaikela wapo Mkwajuni,ndiko kakulia na kusomea hapo japo anafanya shughuli zake Mbeya,Dar na Makongolosi

Balantanda,

Inaelekea unamfahamu vizuri huyo Mwaikela, tusaidie kutufafanulia zaidi ili tumfahamu maana hii ya kupakana matope imekuwa mbaya sana.

Si ajabu anafanya biashara zake, tayari watu wengine wanamwita muuza unga.

Hivi lini tutaanza kuongelea sera badala ya majitaka?
 
&lt;font face=&quot;&amp;amp;quot&quot;&gt;Do not spin issues hapa....&lt;/font&gt;&lt;br /&gt;<br />
&lt;font face=&quot;&amp;amp;quot&quot;&gt;&lt;br /&gt;<br />
1. Unafahamu level ya elimu ya Naibu Waziri wa Elimu?? Unajua ana-rub shoulders na kina nani???&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
2. Kwenye kikao cha mwisho, opposite na eneo la Airport ilipo ofisi ya Mwaikela (jamaa wa darasa la 7), ali-rub shoulders na wasomi 3 toka TEKU; ndugu Shitambala (ambae pia ni msomi LLM)...aliye-confirm kikao hiki kwa JK kwamba ni kweli kimefanyika ni Ngeleja, ambae ni rafiki wa Shitambala...huyu ndiye mtu wa nne katika hili gemu...&lt;/font&gt;
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
Naomba nikujibu kuhusu Elimu ya Mh.Phillip Augustino Mulugo-Naibu Waziri wa Elimu kwa kuwa nimesoma naye na ni mtu wa karibu kwa muda mrefu.Mheshimiwa Waziri ana Bachelor ya Education kama kuna una taarifa tofauti na hii utakuwa umelishwa kasa!
 
Upo sahihi kabisa mkuu...asilimia 90% ya Watanzania [ikiwa ni pamoja na wewe] wapo CCM...wanasumbuliwa na shida, tabu na umaskini uliotopea wa kiuchumi na kiakili, kwao wao hali hii ngumu inayowakabili ni mpango tu wa mwenyezi Mungu!!! Asilimia 10% ndio wapo CHADEMA ......hawa ni matajiri wa kihali na mali, na ni wachache ndio maana CCM bado ipo madarakani...NADHANI NIPO SAHIHI!!
Hongera mzee kwa kuwa na uzoefu mzuri wa kuibiwa na kuridhika!
Sisi masikini bado tupo hiki chama cha makabwela, na sisi tukisema CHADEMA haioni ndani na ndo mwisha wa mchezo.We ridhika na kuandamana and in the mean time siye makabwela tunajijenga.
Wish you all the best
 
Balantanda,

Inaelekea unamfahamu vizuri huyo Mwaikela, tusaidie kutufafanulia zaidi ili tumfahamu maana hii ya kupakana matope imekuwa mbaya sana.

Si ajabu anafanya biashara zake, tayari watu wengine wanamwita muuza unga.

Hivi lini tutaanza kuongelea sera badala ya majitaka?

Namfahamu vizuri sana mkuu...........

George hafanyi biashara ya drugs,namfahamu tangu udogo wake....Alianzia kwenye Udigala(ununuzi wa dhahabu) taratibu akawa anakua katika biashara yake hiyo kiasi cha kuanzisha kampuni yake ya Two Drums G&C Company ambayo inajihusisha na ununuaji wa madini.....Baadaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha wachimbaji wadogowadogo wa mkoa wa Mbeya(MBEREMA)...

Hayo mengine ni uzushi tu a.k.a MAJITAKA
 
Mdau are you sure?

Leteni ushabiki kwenye mambo mengine mengi tu ila siasa za Mbeya ni ngumu sana na ile dhana yangu ya siasa ni mchezo ndio inapaswa kuingilia kati

Fanya assignment yako upya ( Hints

1. Angalia historia ya jimbo la mbeya mjini na Wasafwa
2. Angalia uhusiano wa JK na Mwandosya
3. Angalia uhusioano wa JK na Mwakipesile
4. Angalia nguvu ya Mwandosya kwenye siasa za Mbeya
5. Angalia uadui wa Mwakyembe na Mwakipesile
6. Angalia mwitikio hasi wa Sugu kuwa mbunge kwa jamii ya kisomi ya Mbeya

Ukifanya assignment utagundu akuwa

Nguvu ya chadema mbeya ni kubwa endapo tu watachea karata ; kwanza ni kutoonyesha uadui kwa mwandosya, pili ni kujikita kwa wasafwa!

Ninaposema siasa za pale ngumu kwani zina ukabila sana, Wanyakyusa hawana nguvu na jimbo la mbeya mjini kama inavyodhaniwa, wasafwa wana nguvu na kulitokea uasi wa jamii yao na kuchokwa CCM.

Chadema has only opportunity kuigawa CCM vipande vipande mbeya ila sio kwa siasa hizi za kukurupuka.

Sugu hatakiwi Mbeya kwa sasa na ubunge wwake utakuwa wa shinda sana, wanaoweza kukuambia haya ni wale ambao mbeya mjini ni kwetu. Achaneni na Shitambala au Kitambala,

Sugu you can smoothen your position kwa kuangalia na kukutana na wazee wa hapo mjini, ninajua ninachokisema.

Ukabila unaiua Mbeya mjini ! aibu!

hii stori hapo juu inahusishwa na mbeya ipi??

mbeya hii hii tunayoijua wote, au??
 
Pamoja na kumchoka Mpesya lakini bado kampeni ya Sugu haikuweza kupenya kwenye maeneo ya Wasafwa mpaka Shitambala alipoingilia kati na kwenda kuongea nao lugha wanayoifahamu,its very complicated!!
Acha uongo,Shitambala alikuwepo kwenye uzinduzi wa kampeni tu,kata zote za wenyeji alienda Sugu na mw/kit wa wilaya,ckumbuki mkutano mwingine alihutubia,bali ss wa mjini tulipotaka kwenda kumpiga tafu Mby vijijini,alikataa,pia alikataa mawakala zaid ya 40,tuliomwambia aweke sehemu korofi,mwache Mdau ndiye anajua siasa zetu wa Mby.
 
Shitambala hana ushawishi wowote kwa siasa za Mbeya mjini. Ni kweli kwamba siasa za Mbeya hazitabiriki na lolote linawezatokea kwa wakati wowote. Nina rafiki yangu ambae alikuwa ni mgombea udiwani kata mojawapo ya mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema na alikosa. Nilisafiri nae kwenye gari na kwa nia nzuri tu alizungumza mengi na pia aligusia tabia ya Sugu na mimi niligundua hilo linaweza kuwa tatizo. Alisema Sugu anahusudu sana kujitenga na hili analifanya ili apate nafasi ya kujirusha. Aliendelea kuwa tatizo kubwa kwa Sugu ni akiwa na cash mfukoni, kwani ikiwa kinyume chake ni mzuri sana kimahusiano na jamii. Na aliniambia saa hizi ni jioni ilikuwa kama saa moja na nusu akasema, nimpigie simu sasa kama hutamkuta baa kwenye makelele mengi? Sikumshauri apige simu ila nilijifunza jambo fulani. Pamoja na kwamba Chedema iko juu sana mbeya mjini na ni chama kinachopendwa na makundi yote, binafsi ningemshauri Sugu ajaribu kuwa karibu na watu kama kina mnyika na kujifunza kutoka kwao. Nimepita sehemu nyingi za Dar na hasa jimbo la ubongo, mnyika anazungumzwa kwa sifa nzuri hasa mahusiano yake binafsi na watu na makundi tofauti. Nilishangaa hata kundi la mjahidina kwenye maeneo yao wakimtulea mfano kwamba ni mtu anaejua kuongea na watu na kuwa sehemu katika shida zao.
Ukiachana na Dar, Mbeya bana mtu asikudanganye wale watu wemekaa kimaslahi kuliko mkoa mwingine. Watauza ngozi za watu, vichwa vyenye upaa hata biashara ya mimba changa ipo ili tu wapate pesa. Hivyo kuambiwa kitambala kauza utu wake ili apewe chapaa, hiyo ni asili yao sawa na msemo 'jasiri haachi asili'
.

Umeeleza vizuri kidogo juu mwisho umeishia kuwatukana watu wa Mbeya kwamba ni wabinafsi wanajari pesa,hapo ndiyo umeniacha hoyi kweli kwa hiyo hata chadema wanashabikiwa sababu ya pesa? wanahonga kuliko CCM eeee? Unamawazo mepesi sana!Mbaguzi mkubwa sana wewe! uwezo wako wa kufanya analysis unatia shaka sana! au kiwango chako cha Elimu ni kidogo Mno.
 
Namfahamu vizuri sana mkuu...........

George hafanyi biashara ya drugs,namfahamu tangu udogo wake....Alianzia kwenye Udigala(ununuzi wa dhahabu) taratibu akawa anakua katika biashara yake hiyo kiasi cha kuanzisha kampuni yake ya Two Drums G&C Company ambayo inajihusisha na ununuaji wa madini.....Baadaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha wachimbaji wadogowadogo wa mkoa wa Mbeya(MBEREMA)...

Hayo mengine ni uzushi tu a.k.a MAJITAKA
Asante sana Balantanda,

Haya mambo ya kuchafua kwasababu tu ni siasa yana bore sana.

Inaelekea mambo mengi aliyoyaandika Mdau watu mbalimbali wameyakanusha hapa.

Siasa za majitaka ni balaa na mwaka 2015 zitakuwa hata zaidi.
 
Sina comment yoyote maana Mbeya naijua lakini hali ikoje huko kwa sasa kisiasa nitaju judge mwenyewe kulingana na jinsi hoja zinavyokwenda.
 
Taratibu Mkuu!!

1.Kwa taarifa yako, Sambwee Shitambala HAKUJIAPISHA MWENYEWE bali aliapishwa na WAKILI EVARIST MARTIN MASHIBA, nakushauri zihakiki kwanza data zako kabla ya kuzipost humu.

2. G.Mboma afacilitate fedha za kulinda kitumbua cha mtu aliyemuabisha nyumbani kwake?hivi unaifahamu ego ya G.Mboma?hivi unadhani Million 17 ni fedha ya kumfanya mtu kama Shitambala akubali kuyaacha mafao yoote ambayo angeyapata kwenye Ubunge kwa miaka mitano?

Nikwambie tu, Shitambala aliutafuta Ubunge kwa nguvu zake zote,alijitahidi kadri alivyoweza,lakini mwamko wa wananchi wa jimbo la Mbeya Vijijni kwenye siasa bado ni mdogo sana ukiondoa maeneo ya yaliyopo kwenye Highway, hivyo pamoja na kushinda maeneo ya mijini,CCM wakammaliza maeneo ya vijijini.

Hivyo baada ya kushindwa na kutafakari mazingira yanayomkabili kisiasa na gharama zake,akaona ni rahisi kwake kufanikisha malengo yake ya kisiasa ndani ya CCM kuliko ndani ya CDM.

Ndugu Butola, changamsha ubongo utambue kwamba;

1. Shitambala, LL.M "ALIJIAPISHA" mwenyewe kwa sababu aliyemuapisha ni WAKILI kama yeye, wakati sheria haitamki hivyo, that means alifanya makusudi!!...WANASHERIA wanaweza kutusaidia kwenye hili...

2. Gen Mboma ni fisadi tu kama walivyo mafisadi wengine, ego yake haiwezi kumzuia kushiriki kwenye uchafu kama huu...kashashiriki kwenye ufisadi mwingi tu...

Shitambala hajatafuta UBUNGE kwa jitihada zake, zilitosha sana ndio maana alikataa MAWAKALA!!????

Malengo ya kisiasa atakayoyatimiza CCM na si CDM ni yapi?? Acha poor reasoning, kama ni malengo ya dhati alitakiwa ayatimilize akiwa CDM, nani yupo CCM kwa maslahi ya Taifa??
 
Back
Top Bottom