Rev Mtikila aachiwa baada ya kulipa deni

Rev Mtikila aachiwa baada ya kulipa deni

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,667
Reaction score
37,834
Kwa mlioona taarifa ya habari ya tbc; pastor/rev/appostle wetu machachari ambae majuzi chombo cha sheria kilimhukumu miezi sita kabla ya kukamatwa kwenye street ametoka na kurudi tena uraiani baada ya kulipa hela za watu mil 9 na ushee. Hata hivyo alipoachiwa alikiri atakata rufaa, anasubiri uchaguzi uishe arudi mahakamani.
Hongera mpambanuaji
 
Jamaa wapenda amani na uchaguzi wamelipa hela. Wamefikiria kuwa bila Mtikila uchaguzi hauwezi kuwa wenyewe. Hongera mzee wa kesi mahakamani
 
Mi huyu mtu namwogopa kwanza wapi umeona mtu anahukumiwa alafu analipa akiwa ndani anatoka jamani hii sheria ipo ...mmhh siwezi kujua...rev...chriss we noma yaani nakupa kumi mikono yote huko mahakamani najua mahakimu wakikuona wanaomba kwenda toilet kwanza
 
Kuna wakati huwa namhusudu sana huyu jamaa ingawa kuna wakati huwa sikubaliani na mambo au maneno yake,kiukweli Mtikila anajua sana kucheza na akili za watu kiasi kwamba umaarufu wake katika vyombo vya habari haushuki zaidi ya kuongezeka,tusubiri vimbwanga zaidi baada ya leo kwani natumai ataongea tu na waandishi wa habari
 
Probably the most controversial and flamboyant politician in Tanzania history. Politics is never the same without this fella in this country.
 
Kuna wakati huwa namhusudu sana huyu jamaa ingawa kuna wakati huwa sikubaliani na mambo au maneno yake,kiukweli Mtikila anajua sana kucheza na akili za watu kiasi kwamba umaarufu wake katika vyombo vya habari haushuki zaidi ya kuongezeka,tusubiri vimbwanga zaidi baada ya leo kwani natumai ataongea tu na waandishi wa habari

Huwa napenda sana jinsi anavyojenga hoja, lakini vituko vyake kama vya madeni ambavyo wanaweza malizana tu huko mtaani sivifagilii kabisa. Inaonesha si mstaarabu, ndiyo! si mstaarabu, kama siyo kwanini mpaka wapelekani lupango kama ni mtu wanaaminiana? Kwa maana hataki kulipa madeni ya watu. Ajifunze na astaaribike.
 
Huyu ni msanii tu, hajashindwa kulipa hiyo hela. kuna wakati huwa naona kama anatumiwa na ccm ili kupumbanza na kutufanya watz tusahau mada motomoto zinazoendelea vile....huyu jamaa ni ccm kabisa.
Pili, hoja zake za kidini, zinakera, analitukana hata jina la Mungu kwa kutuletea porojo zake za ajabu....huwa sipendi hata kusikiliza akianza udini wake....anahitaji msaada. however, huwa namfagilia sana kwenye hoja zake zingine...natumaini Mwalimu Mhozya naye atakuwa pacha wake....huyu naye ni maarufu kwa umtikilaumtikila..
 
Welcome back uswaz Rev Kris,
Never took him seriously..japo kuna mahala anajenga hoja zenye mashiko...
Ningem-miss Uchaguzi huu..
 
Nakumbuka mambo mawili tu ambayo yananifanya siku hizo kumpuuza kabisa huyu mchungaji.

1. Alipolamba pesa ya fisadi. Alikwisha ingia katika mtego wa RA, kamwe siwezi kumwamini.

2. Alipokiri hadharani kutumiwa na ccm kuimaliza Chadema Tarime, kwa kuzua madai ya uongo. Hata kama aliomba radhi lakini si mtu wa kuaminika tena.

Mimi ningependekeza watanzania wampuuze, kwanza hana mvuto tena wa kisiasa, si mwanamageuzi tena, ameishiwa.
 
Mi huyu mtu namwogopa kwanza wapi umeona mtu anahukumiwa alafu analipa akiwa ndani anatoka jamani hii sheria ipo ...mmhh siwezi kujua...rev...chriss we noma yaani nakupa kumi mikono yote huko mahakamani najua mahakimu wakikuona wanaomba kwenda toilet kwanza
Kuna tetesi kuwa aliyekuwa anamdai ni mkewe, i wonder whether that is true.
 
Mtikila kapata wapi pesa hizi zote kwa kipindi kifupi hivi?

Amepata kule alikopata za kumsumbua Sumaye lakini this time hatafanikiwa. Pia CHadema ni lazima watu kama mtikila na Mrema wawe kwenye defensive mode muda wote ili wasifanye offensive yoyote, you know what i'm saying!!!!
 
Nakumbuka mambo mawili tu ambayo yananifanya siku hizo kumpuuza kabisa huyu mchungaji.

1. Alipolamba pesa ya fisadi. Alikwisha ingia katika mtego wa RA, kamwe siwezi kumwamini.

2. Alipokiri hadharani kutumiwa na ccm kuimaliza Chadema Tarime, kwa kuzua madai ya uongo. Hata kama aliomba radhi lakini si mtu wa kuaminika tena.

Mimi ningependekeza watanzania wampuuze, kwanza hana mvuto tena wa kisiasa, si mwanamageuzi tena, ameishiwa.

Ni kweli unayosema -- Mtikila ni mtu asiye na maadili wala msimamo wowote wa kisiasa na amekuwa anatumiwa kila mara. Mwaka 2000 aliwahi kukipigia kampeni CUF. Pia mapema 2006 aliwahi kutumiwa na Mengi katika sakata lake na Manji kuhusu Ubungo godowns.

Hayo ya Tarime ndiyo yalikera sana kwa sababu alikuwa anakampeni kuonyesha kuwa akina Mbowe ndiyo wahusika wa kifo chs Chacha Wangwe. Alifanya hivyo bila aibu.

Mimi nina wasiwasi sana kwamba hizo hela alizolipa deni lake amepewa na wanasiasa -- na si kwa bure. Sintashangaa iwapo katika kampeni zake za kugombea urais akaanza kukampeni against Dr Slaa na Chadema -- badala ya kujikampenia yeye mwenyewe au dhidi ya chama anachotarajia kuking'oa madarakani -- yaani CCM. Ngojeni tu -- mtakuja kukubaliana nami.

Akifanya hivyo itakuwa ni rahisi kujua akina nani wamempa hela hizo kulipia deni.
 
Zak,
Unachohisi kuwa huyu Mtikila atakampeni against CHADEMA ndio mkakati wenyewe ulivyosukwa. Na si huyo tu, yumo na mtu aliyewahi kuwa mweka hazina wa CHADEMA taifa. This time CCM wako desperate kwelikweli.
 
nakumbuka mambo mawili tu ambayo yananifanya siku hizo kumpuuza kabisa huyu mchungaji.

1. Alipolamba pesa ya fisadi. Alikwisha ingia katika mtego wa ra, kamwe siwezi kumwamini.

2. Alipokiri hadharani kutumiwa na ccm kuimaliza chadema tarime, kwa kuzua madai ya uongo. Hata kama aliomba radhi lakini si mtu wa kuaminika tena.

Mimi ningependekeza watanzania wampuuze, kwanza hana mvuto tena wa kisiasa, si mwanamageuzi tena, ameishiwa.

mbona tunaambiwa pesa zao tulambe kura tusiwape sasa kama fisadi anajipendekeza ulitaaka amwache kweli babangu???
 
Back
Top Bottom