Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
- Thread starter
- #61
Tunaomba utuletee na ya Jerry Slaa....kwenye utaratibu kama huu
Atakuwa honeymoon!au zenji na jamaa ake wakila good time!
Halima Mdee atoweka jimboni Kawe na katika chama chao cha CHADEMA. Kuanzia mwishoni mwa mwaka 2011 mpaka sasa Mbunge wa Jimbo Kawe na mjumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho Halima Mdee haonekani kwenye kazi katika jimbo hilo na katika matukio yanayoandaliwa chama hicho.
Mbunge huyo kijana hakuonekana kabisa wakati wa maafa ya maafuriko yaliyotokea katika mkoa wa Dar es salaam mwishoni mwa mwaka 2011. Badala yake vyombo mbalimbali vya habari vilieleza kwamba mbunge wa jimbo jirani la Ubungo alitembelea maeneo yaliyopata maafa katika jimbo hilo ya Msasani na Boko.
Halima Mdee hakuwepo pia wakati ambapo wabunge wa Dar es salaam wakitoa tamko kuhusu pongezeko la nauli katika kivuko cha Kigamboni, ambapo Waziri Magufuli alimpongeza kwa kuacha kutoa tamko hilo pamoja na wenzake.
Mbunge huyo machachari hakusikika pia katika mkutano wa baraza la madiwani la jiji ambalo lilijadili mambo yenye kuvuta hisia hasa kuhusu UDA na pia wakati wa kikao cha bodi ya barabara ambapo vyombo vya habari vimedokeza kilikuwa na mjadala mkali.
Anaweza kuwa na personal issues, she is also human.