Reli ya DAR (Treni ya Mwakyembe) kubinafsishwa rasmi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1686832998000.png
Serikali imesema Reli ya Dar es Salaam (Dar -Commuter Rail) maarufu kama treni ya Mwakyembe ni moja ya miradi inayokusudiwa kuendeshwa na sekta binafsi ikiwa ni utaratibu wa kutekeleza Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amesema bungeni jiji Dodoma kuwa mradi huo ni miongoni mwa miradi 48 ambayo serikali inakusudia kuiendesha kwa ubia na sekta binafsi.

Benki ya Dunia na wadau wengine imebainisha jumla ya miradi 48 inayoweza kutekelezwa kwa utaratibu wa ubia na sekta binafsi.

Miradi mingine ni Reli ya Mtwara-Bamba Bay; Uendeshaji wa Reli (Rolling stocks); Uendeshaji wa Barabara ya haraka (expressway) kutoka Igawa-Tunduma; Barabara za 38 kupunguza msongamano katikati ya Jiji la Dar es Salaam (Inner and Outer Ring Roads); Barabara za haraka kutoka Kibaha Chalinze - Morogoro hadi Dodoma na kuunganisha Jiji la Dodoma na Dar es Salaam kwa barabara za haraka; Bandari kavu katika eneo la Kisiwa/Mgao – Mtwara; na Kuboresha na Upanuzi wa bandari katika Ziwa Victoria - Mwanza na Nansio - Ukerewe.

Mwigulu amesema utaratibu huo ni sehemu ya mpango wa kimkakati wa serikali kushirikisha sekta binafsi ambayo ilipewa jukumu la kugharamia asilimia 17 ya bajeti karibu Sh trilioni 21.
 
Mkuu BARD AI , ukiwa unamtaja Mwigulu, tafadhali anza na Mh., Dkt. then Mb, na kisha malizia kwa cheo chake cha uwaziri wa fedha. Jitahidi kuwa makini sana na uandishi wako.

NB: Ndipo sie tumekaribia huku mpakani kuhamia Burundi.
 
(Rolling stocks); Uendeshaji wa Barabara ya haraka (expressway) kutoka Igawa-Tunduma; Barabara za 38 kupunguza msongamano katikati ya Jiji la Dar es Salaam (Inner and Outer Ring Roads);
Hii misamiati ndiyo wanaitumia kutupiga
 
Hapo atapewa mtu wa genge la wenye nchi ili kusudi ahujumu mradi ufe ili malori yasikose kazi 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom