"Pascal Mayalla, tofauti ya matumizi ya nembo hizi mbili ni nini? Wapi Rais anatumia nembo ya taifa na kwa nini na wapi anatumia nembo ya Rais na kwa sababu gani..
Je, wananchi wananufaika nini na mabadiliko ya matumizi ya nembo pale zinapotumika tofauti..pse!
Kiukweli kuna vitu mimi sivijui, mfano tulipoungana na Zanzibar kuunda serikali ya JMT, tulikuwa na bendera moja ya JMT na wimbo mmoja wa taifa wa JMT, na JMT ina katiba moja ya JMT, inayosema Tanzania ni nchi moja ya JMT, yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar na kuielezea Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani. Mwaka 2010 kukafanyika mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kuitambulisha Zanzibar kuwa ni nchi, na ni moja ya nchi mbili zilizounda JMT, baadae kukatokea na wimbo wa taifa wa Zanzibar, baadae kukatokea na bendera ya Zanzibar, japo mabadiliko hayo ya katiba ya Zanzibar, katiba ya JMT haiyatambui lakini yapo!. Mpaka sasa bado siijui status ya Zanzibar ni nini?!.
Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete, walikuwa na bendera ya rais yenye nembo ya rais, lakini sikuwahigi kuona any public use ya nembo hiyo, ndio nimejua jana kupitia humu JF!.
Kiukweli kabisa elimu ya uraia inahitajika sana kuliko tunavyo kudhania. Kwa vile mimi ni mwanasheria, nina uhakika asilimia 100% ya 100%, mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ni batili!, lakini JMT na katiba ya JMT imeunyamazia ubatili huo kwasababu hautuhusu!.
Ndani ya katiba yetu wenyewe kuna ubatili mwingi tuu unaotuhusu na umenyamaziwa!, hivyo unaweza kukuta hata matumizi ya nembo ya rais kwenye shughuli za Kitaifa badala matumizi ya nembo ya taifa pia ni ubatili!
P