Bwana alitoa na bwana ametwaa sifa,shukrani na utukufu ni kwako muweza yote unaetuinua tunapojijwaa na kuanguka na alipoangukia Regia ndipo tunapoinukia kuelekea ukombozi wa mtanzania damu yako iwe maji ya kututia nguvu za mapambano sauti yako itaendelea kuwa filimbi ya vita hivi vya ukombozi unalala Regia nasi tutaamka kwa maelfu kuendeleza ukombozi tulitaka ubaki lakini hatukua na nguvu za kukubakisha RIP REGIA ALUTA CONTINUA CHADEMA!
Nimethibitisha kwa Mwenyekiti Mh.Mbowe.Hakika hili ni pigo kubwa kuliko maelezo haya, sina njia ya kulizungumzia.Huyu Dada yetu mpiganaji nilikuwa naye ana kwa ana yapata mwezi na siku kadhaa sasa katika moja ya Mikoa ya Nyanda za juu Kusini tukizungumzia mambo makubwa mengi sana.Sikujua kwamba hiyo Dinner pamoja naye ndio ilikuwa tunaagana, kwa kuwa aliondoka kesho yake kuelekea Moshi Machame kujiunga na Viongozi wengine katika Birth day ya Kamanda Mkuu Mh.Mbowe.
MWENYEZI MUNGU ni wa ajabu sana na ndio maana huwa hataki sisi wanadamu tumzoe, kwa kawaida yake anapofunga mlango mmoja hufungua mwingine.Nina hakika kuondoka mapema kiasi hiki kwa Dada yetu Mh.REGIA MTEMA ni kipimo tosha iwapo tunaweza kuthubutu kuvumilia na kukubaliana na machungu hata pale wapendwa wetu wanapoondoka katika umri ambao ndio nguvu kazi yake inahitajika sana.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA BWANA LIHIDIMIWE
The Good always die young,
Thanx God for giving us a short time with Regia,
Regia you lived your life so well,
you lived a short life, however you achieved a lot,
You fought well, for the benefit of all
We will fondly miss you.