Refa Anapokuwa Shabiki wa Brazil

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,739
155,433
Jana nilijionea tukio la kustaajabisha wakati Luis Fabiano akifunga goli la mkono.
Alishika mpira kwa mkono akawapiga kanzu mtu na kaka yake, mpira ukamzidi, akauvuta tena kwa mkono, kisha akausukuma mpira kimiani.
Baada ya hapo Refa akiwa ameongozana na Luis fabiano alionekana akimwambia kwa ishara kuwa goli lako ni la mkono, lakini nimelimezea kwa sababu tu naipenda Brazil.
Hivi refa kama yule anaweza akashitakiwa Fifa au ndio haki imeisha na dakika sitini zake?
 
Yaani yule refa hafai kabisa na anastahili kufungiwa. Maana kwenye slow motion wamemuonyesha vizuri kweli anavyocheka na Fabiano huku akimwonyesha kuwa umeunawa mpira kabla ya kufunga na Fabiano anakana kwa kuonyesha kuwa "nimeutuliza kifuani refa". Lol!
 
yaani marefa hawa sijui wanalewa chang'aa kwanza ndo wanaingia uwanjani?ni upumbavu mtupu.mi natamani atoke mchazaji amtwange vichwa basi kama walivofanya tp mazembe kwenye kagame cup.wanaudhi sana marefa
 
ma refa wa safar hii naona mgogoro .........marekani wamekataliwa goli bla ya maelezo ya msingi. Kuna wanaopewa redcards kwa faul za kipuuzi kabsa.....agggr
 
Jana nilijionea tukio la kustaajabisha wakati Luis Fabiano akifunga goli la mkono.
Alishika mpira kwa mkono akawapiga kanzu mtu na kaka yake, mpira ukamzidi, akauvuta tena kwa mkono, kisha akausukuma mpira kimiani.
Baada ya hapo Refa akiwa ameongozana na Luis fabiano alionekana akimwambia kwa ishara kuwa goli lako ni la mkono, lakini nimelimezea kwa sababu tu naipenda Brazil.
Hivi refa kama yule anaweza akashitakiwa Fifa au ndio haki imeisha na dakika sitini zake?

hahaha Bujibuji leo umenichekesha ulijuaje kama Refa kamwambia Luis F maneno hayo?
 
ma refa bogus bwana ..............kaka kapigwa yellow ya pili ile bla sababu ya msingi

ujerumani nayo inalia na refa .....

new zealand pia inala na refa ......penalty ya Italia haikuwa na sababu

Marekani inalia refa kawanyima goli

Fainali zinachezwa afrika basi tena kila kitu kinakwenda kiafrika afrika tu
 
Anaweza asimwambie hivyo exactly,kwanza hawaongei kiswahili,lakini it was obviously refa alikuwa anamaanisha hivyo.

Ni kweli Hassani nadhani refa alikuwa anajaribu kumwambia huu mpira umeshika na mkono jamaa anakataa ..
ila world cup ya 2010 sijui
 
Jamanimsameheni refa, kila mtu ameumbwa kupenda. Hata mimi kwa jinsi Fabiano alivyocontrol ule mpira in front of 3 defenders wawili kati yao wakiwa ndugu wa damu ni aibu kubwa sana kwa defenders.

Naamini refa na mshika kibendera wake walikuwa wanafurahia individual brilliance za Fabiano.......kuja kushtuka goli limeingia so akawa ana jinsi zaidi ya kurudi kati!!

Jamani tuache utani...Brazil wataaaaaaaamuuuuuuuuuuuu!!
 
wa-sauzi wanatuangusha kwa nini wasiwatwage risasi marefa kama hawa ili iwe fundisho! wanatuaribia woooooza yetu; washenzi hawa
 
ma refa bogus bwana ..............kaka kapigwa yellow ya pili ile bila sababu ya msingi

ujerumani nayo inalia na refa .....

new zealand pia inala na refa ......penalty ya Italia haikuwa na sababu

Marekani inalia refa kawanyima goli

Fainali zinachezwa afrika basi tena kila kitu kinakwenda kiafrika afrika tu

Mkuu hiyo niliyoweka kwenye nyekundu si sahii. Kaka alistahili kabisa hiyo njano ya pili maana alimpiga kipepsi yule mchezaji wa IvoryCoast kwa kukusudia kabisa. Hata asingekuwa na ile ya kwanza kwa kosa hilo alistahili kupata nyekundu moja kwa moja.
 
msiwalaumu marefa. wanazungukwa na msitu wa wachezaji 22, hapo unategemea nini? alishakubali goli bila na maamuzi ya refa yanatakiwa ndani ya nusu sekunde. yule wa marekani na slovenia si ndio kituko?
 
...Hakumpiga kiwiko chochote! Waligongana tu na yule mchezahi wa Ivory Coast akasema, hapa hapa...!:whistle:
 
1.kuna ball hand na hand ball.
2.inategemea wewe ndie ulieushika mpira au mpira umekugonga kwa bahati mbaya.
2.kosa kama hilo lipo chini ya sheria namba 12 ya mpira wa miguu...faul and misconducts
 
Jana nilijionea tukio la kustaajabisha wakati Luis Fabiano akifunga goli la mkono.
Alishika mpira kwa mkono akawapiga kanzu mtu na kaka yake, mpira ukamzidi, akauvuta tena kwa mkono, kisha akausukuma mpira kimiani.
Baada ya hapo Refa akiwa ameongozana na Luis fabiano alionekana akimwambia kwa ishara kuwa goli lako ni la mkono, lakini nimelimezea kwa sababu tu naipenda Brazil.
Hivi refa kama yule anaweza akashitakiwa Fifa au ndio haki imeisha na dakika sitini zake?
Kiongozi, nadhani hapo kwenye nyekundu ulitaka kuandika dakika tisini. For the sake of football
 
Back
Top Bottom