Refa anapofunga goli kwa bahati mbaya, wajua nini kinafanyika?

leadermoe

JF-Expert Member
Feb 15, 2017
1,392
4,573
Kuna vitu vinatokea uwanjani hasa kwenye mchezo wa soka, haijalishi mara ngapi inatokea, lakini vinakuwa sio vya kuchekesha. Vinabadili matokeo ya mchezo, na kuathiri matokeo ya ujumla. Lakini wakati mwingine kuvizuia kawaida ni ngumu kwa sababu vinatokea kwa bahati mbaya.

Miongoni mwa vitu adimu vya kuchekesha kwenye soka, ni mwamuzi kubadili muelekeo wa mpira bila malengo. Lakini nini kinatokea ikiwa muamuzi ama refa anabadili muelekeo na kufunga bao kwenye mpira wa miguu? Ni nini hufanyika ikiwa mwamuzi ataugusa mpira?

Hata swali la 'Je! Mwamuzi amewahi kufunga bao kwa bahati mbaya?' Linaonekana la kushangaza na kama halina maana. Wao ni waamuzi, baada ya yote, wanapaswa kuamua mchezo ili mshindi apatikane kihalali na magoli yafungwe kihalali kwa mujibu wa sheria 17 za mchezo wa soka. Lakini mwamuzi kufunga goli, ambalo ni faida kwa timu pinzani, maana yake nini?

Hii ni mifano michache ya mabao ya waamuzi
Ipo mifano michache hapa ya muamuzi kufunga bao katika mchezo wa soka. Mnamo Septemba 2001, Brian Savill alikuwa mwamjuzi wa mechi kubwa ya marudiano ya kombe la Bromley kati ya Earls Colne na Wimpole 2000, aliifungia bao Wimpole.

Hata hivyo bao hilo halikuwasaidia lolote Wimpole, kwani walichabangwa jumla ya mabao 20-2, lakini miezi minne baadae mwamuzi huyo alijiuzulu baada ya kuambiwa angesimamishwa na Chama cha Soka.

Mwezi Mei 2019, mwamuzi Maurice Paarhuis aliifungia bao timu ya HSV Hoek katika mchezo dhidi ya Harkemase Boys kwenye mchezo wa daraja la nne nchini Uholanzi. Goli hilo hata hivyo halikuwasaidia sana HSV waliochapwa 4-2.


Maelezo ya picha,
Waamuzi wa soka sasa wana haueni kutokana na uwepo wa sheria zinazowalinda inapotokea wamefunga goli kw abahati mbaya

Mwaka 1986, msiba ulimpata mwamuzi Ahmet Akçay alipojikuta akiunganisha kwa bahati mbaya mpira wa dakika ya mwisho kabisa wa mchezo uliowapa ushindi timu ya MKE Ankaragücü katika pambano la ligi ya Uturuki dhidi ya Besiktas. Mwamuzi huyo alisimamia goli hilo, likasalia na Ankaragücü iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

"Hii ni mara ya kwanza kufunga goli katika miaka yangu 17 katika mpira wa miguu," Akçay aliliambia gazeti la Milliyet baadaye. "Dhamiri yangu iko safi."

Pengine goli hilo lisingefungwa Besiktas ikitwa ubingwa wa ligi, kwani mwishoni mwa ligi Besiktas ilimaliza na alama sawa na bingwa Galatasaray lakini kwa tofauti ya bao moja tu. Wengi wanalikumbuka bao mwamuzi huyo limeleta tofauti hiyo.

Kabla ya mwaka huo, mwaka 1983 kuna mchezo wa ligi kuu ya Brazil kati ya Santos na Palmeiras, ambapo mwamuzi José de Assis Aragão alijikuta akifunga bao lililoisaidia Santos kupata ushindi wa mabao 3-1. Mpaka dakika ya 90, Santos ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1 , lakini dakika ya pili ya muda wa nyongeza mwamuzi huyo Aragão kwa bahati mbaya alifunga bao hilo na kuibua hasira kwa mashabiki wa Palmeiras.

Mabadiliko ya Sheria mwaka 2019
Refa

Mizozo huibuka mingi uwanjani kati ya muamuzi na wachezaji, inapotokea muamuzi kuingilia mchezo kwa namna yoyote ile, achilia mbali kufunga goli

Kupitia mifano ya matukio ya waamuzi Paarhuis, Akçay na Aragão, kila mmoja wao, kwa wakati huo walikuwa sahihi kuruhusu mabao waliyofunga na kuwa halali. Hadi sheria ilipobadilika mnamo Juni 2019, sheria ilikuwa inasema: "Mpira unakuwa kwenye mchezo wakato wote ikiwa ni pamoja na utakapomgusa muamuzi, kugonga mwamba au kibendera na kurudi uwanjani."

Sheria za mchezo

Wakati huo, muamuzi alionekana kama sehemu ya mchezo, sio kama kitu ambacho kiko nje ya uwanja, ndio maana mpira ukimgonga muamuizi, wakati wowote na kuzaa goli liliruhusiwa.

Lakini mwezi Juni, 2019, mambo yalibadilika; sheria nyingi kaytia vyama na mashirikio ya soka ulimwenguni yalifanya mabadiliko, ikiwa ni wiki moja tu baada ya Paarhuis kufunga goli kwa bahati mbaya. Lakini kwa sasa kuna sheria tofauti:

"Mpira utakuwa nje ya mchezo kama utamgusa muamuzi na kusalia uwanjani; na kusaidia timu kuanzisha shambulizi la hatari, au mpira ukaenda moja kwa moja golini, au umiliki wa mpira utapokwa na timu pinzani."

Nini kinatokea , kama muamuzi ataugusa mpira sasa na kuzaa bao?
Chini ya sheria mpya, kama muamuzi ataugusa moja kwa moja mpira na kuingilia mchezo, atapaswa kusimamisha mchezo na kuanzisha upya kwa kuudondosha mpira. Kwa sasa huenda kusiwe na magoli ya kufungwa na waamuzi, lakini itabaki tu uamuzi wa waamuzi pekee kuchangia matokeo lakini si wao kushiriki kwa kufunga moja kwa moja.
 
Mpira ukimgonga refa na kuingia golini ni goli kama ataweka kati na sio goli kama atawapa mpira waliofungwa wauanze.
 
Avatar nyingi humu zinaakisi mtu husika, kama huyu mwamba aliweka picha ya tatizo lililokuwa likimsumbua.

R.I.P!.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom