Tanzania Premier League 'TPL' Simba SC Vs Ndanda FC Uwanja wa Uhuru Dar Es Salaam

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania 'TPL' kuendelea kupigwa leo Mei 19, 2019 kunako uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ambapo Mabingwa watetezi Simba SC, Mnyama Mkali Mwituni, wakiwakaribisha Ndanda FC Wanakuchele kutoka Mtwara.

Ni mechi inayotarajiwa kuwa ngumu ya vuta nikuvute kwa muda wote wa dakika tisini, kwani katika mchezo wa mzunguko wa kwanza timu hizi zilitoka sare ya kutofungana.

Leo wanapambana tena Ndanda FC watawasimamisha Simba SC? Au Simba SC watapata matokeo chanya yatakayowasogeza kushikilia kombe kwa mkono mmoja? Usikose Ukaambiwa.

Kumbuka mchezo kuanzia saa 10:00 jioni na itakuwa mubashara na Azam Sports 2.


IMG_20190519_151428_340.jpeg
IMG_20190519_151748_347.jpeg


Wakati wowote Kabumbu litaanza uwanja wa Uhuru

Naaaaam mpira umeanza uwanja wa uhuru

00' Simba SC 0-0 Ndanda FC

05' Gooooooooooooaaaal goooooaal
Maddie Kagere anahesabu bao la kwanza upande wa Simba akipokea pasi ya Bocco

Simba SC 1-0 Ndanda FC

Simba wanatawala mchezo wa kwa pasi za hapa na pale.

Ni dhahir Simba wanataka kupata matokeo ya ushindi mapema ili kuweza kuimarisha uongozi wa ligi

10' Goooooooooooooooooooaaal Maddie Kagere anahesabu bao la pili upande wa Simba

Simba SC 2-0 Ndanda FC

15' Mpira unacheza upande wa Ndanda FC pamoja na kushambuliwa langoni mwao!

Bocco anakwenda, lakini anakosea wanachukua Ndanda wanakwenda mbele kujaribu kushambulia lakini Niyonzima anaharibu mipango

20' Simba SC 2-0 Ndanda FC

Ndanda wanapata faulo..Nahodha Makasi anapaisha na kuwa goal kick

25' bado matokeo Simba wako mbele kwa goli mbili bila majibu...

Zana anaonywa na mwamuzi baada ya kumfanyia madhambi

30' Simba SC 2-0 Ndanda FC,

Wachukua Simba kwake Mo Hussein anatokea golikipa anakuokoa

Kagere anakwenda na mpira mashariki ya uwanja, Ndanda wanajaribu kuondosha hatari ile...

Haya Ndanda wanaonana sasa kujaribu kulisogelea lango mchezaji anapiga ndefu lakini unatoka nje ya lango upande wa Simba

35' Simba SC 2-0 Ndanda FC

Kigi Makasi anaonyeshwa kadi ya Njano baada ya kumchezea faulo Zana Coulibaly

Mkopi anapiga ndefu..Lakini Aishi Manula anatokea na kudaka bila wasiwasi.

Mpaka sasa mpira umepungua ile kasi ya mwanzo

40' kuelekea kuwa mapumziko ambapo Simba wanaongoza kwa bao mbili

Hassan Dilunga anapiga shuti kali kwa umbali mrefu..Lakini unatoka nje kuwa goal kick

V. Manyanga anakwenda na anapiga chenga hata hivyo anaukosea..!

45+2' kipindi cha kwanza kimemalizika ambapo Simba wanatoka wakiwa mbele ya mabao mawili ya Maddie Kagere 05' 10

Simba SC 2-0 Ndanda FC


Naaaam..Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Uhuru

50' Matokea bado yale yale kwa Simba kuongoza mabao mawili bila majibu.

55' Mayanga anapapatuana na walinzi wa Simba, lakini simba wanamiliki.

60' Simba SC 2-0 Ndanda FC

Bocco anafinya kutaka kutoa pasi..Lakini wanapoteza

Magharibi ya uwanja Mo Hussein kwake Bocco, lakini mpira wanaunasa Ndanda

Muhilu amecheza vizuri hapa kujaribu kusaidia mashambulizi

65' Simba SC 2-0 Ndanda FC kipindi cha pili mtanange wa TPL

Beki wa Ndanda nusura afungishe, ila golikipa ametokea na kuuwahi mpira ule..

Hassan Maulidi anacheza pembeni..refa anasema ni faulo kuelekea Ndanda.

Simba wanakwenda langoni mwa Ndanda, anatokea beki wao na kulala kuokoa hatari.

70' Simba 2-0 Ndanda FC

Kotei anatoa pasi fupi, Inakataliwa wanachukua ndanda lakini unakuwa mwingi na kutoka nje..!

73' Anatoka Yusuf Mlipili anaingia Pascal Wawa

Hakuna matumaini ya Ndanda FC kusawazisha, wakati huohuo anatoka Makasi anaingia mchezaji Salum.

Niyonzima anatoa pasi safi..Maddie Kagere anakosa bao wazi..ilikuwa hatari.

Anatoka John Bocco..Anaingia Rashid Juma

Ndanda wasogea lango la Simba..Lakini wakaa vema mabeki wa Simba wakingozwa na Wawa.

87' Simba SC 2-0 Ndanda FC

Kagere anakosa nafasi ya kuandika bao last tatu dakika hizi za lala salama.

90+3' Wakati wowote mpira utakuwa umemalizika uwanja wa Uhuru

Naaaaaaam mpira umekwisha uwanja wa Uhuru ambapo Simba wamefanikiwa kutoka na ushindi wa mabao mawili bila majibu yakiwekwa kimiani na Maddie Kagere 05' 10

Simba SC 2-0 Ndanda FC
 
Back
Top Bottom