Redio inagonga nyimbo kali za zamani za injili balaa

Baba jayaron

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
4,008
5,446
Bwana asifiwe,

Wapenzi wa gospel songs Kuna redio inaitwa New life fm redio Moshi Ni balaa wanagonga nyimbo za injili za zamani mpaka unahisi Mbingu inakushukia.

Kwanza mtangazaji Yuko vizuri Hana maneno mengi na sauti iko vizuri kifupi jamaa anastahili kupata redip kubwaaa zaidi maana anajua Kila kitu. Jina lake sijalishika aliopo Moshi anikumbushe jina lake.

Kipindi nadhani kinaitwa KUIMBA ZAMANI Kila jpili kuanzia saa nane mpaka 11 jioni. Yaan hapa naiskiliza yaani nikasema siwezi barikiwa mwenyewe....

Jpili njema watu wa Mungu
 
kwenye app za redio inapatikana pia ili tulioko mbali na Moshi tuipate?
 
Ila kwaya za zamani walitimiza wajibu wao aisee.
° Msalato Dodoma - yupo Mungu
° Kwaya ya mabibo
° kuna kwaya moshi huko huko wimbo unaitwa machweo
° Makongorosi chunya nk
Ulikua unasikiliza na wewe???
Yaani walikua na ujumbe na beats nzuri saana
 
Itakuwa wewe ndo mtangazaji kwenye hicho kipindi unatafuta tension ya kujua je watu wanakusikiliza!!!! Sawa ujumbe umefika na mungu akubariki mtumishi
N.b,,, kama malebo haijapigwa hapo basi hiyo playlist fake
 
Itaachajwe kupigwa Mzee??? Mwamba Ni noma yule.

Anyway Kama yupo humu ajitokeze binafsi amenikosha saana
 
Itakuwa wewe ndo mtangazaji kwenye hicho kipindi unatafuta tension ya kujua je watu wanakusikiliza!!!! Sawa ujumbe umefika na mungu akubariki mtumishi
N.b,,, kama malebo haijapigwa hapo basi hiyo playlist fake
Radio inasikika bomangombe tu ata moshi mjini haifiki
 
Bwana asifiwe,
Amina!
Naomba nikusahihishe kidogo kwenye salaam yako kwa sababu haiko sahihi; hii siyo salaam ya waumini wanaomwanini Yesu; Bwana asifiwe, YUPI?

Salaam hii uliyoitumia hapa kwa uelewa wangu mimi mpaka muda hii ni salaam special ambayo huwa inatumiwa na watu ambao huwa wanaingia Kanisani nia yao ikiwa ni kuja kurusha mapepo kanisani kwa ajili ya kuzima Ibada. Nina vimiaka kadhaa Kanisani na nimeshalithibitisha hili pasipo shaka yoyote

Salaam sahihi ni hii "Bwana Yesu Asifiwe", na maneno yote haya matatu yanaandikwa kwa herufi kubwa kwa sababu mawili ya kwanza ni "nomino" na hivyo lazima yaandikwe kwa herufi kubwa, na la tatu ni kiwakilishi cha nafsi ya MUNGU ambalo linabeba kiwakilishi cha nafsi "Yeye" "Asifiwe"; nani huyo; "Bwana Yesu" na hivyo ni lazima "A" inadikwe kwa herufi kubwa kwa sababu ni kiwakilishi cha nafsi ya MUNGU, na si ya binadamu

Ukimkuta mtu yupo kanisani amesimama mbele ya waumini halafu anasalimia kwa salaam ya "Bwana asifiwe"; huyo ni wa kuogopa kama ukoma. Ninaongea kutoka kwenye experience ya angalau miaka karibia kumi; na muda siyo mrefu nitakuja na post kuhusiana na salaamu hii ya "Bwana asifiwe"

The best alternative kwa salaam hii "Bwana Yesu Asifiwe";ni ile inayotumiwa na waumini wa RC. Hii salaam ndiyo the best kuzidi salaam zote za wakristo. Salaam inasema hivi: TUMSIFU YESU KRISTO; MILELE AMINA

Ningekuwa na mamlaka na Makanisa ya Walokole, ningeifuta salaam wanayotumia sasa; halafu ningewaambia watumie hii inayotumiwa na waumini wa RC. Salaam hii ya waumini wa RC ni ya pekee sana kwa sababu inasema ANAYESIFIWA NI YESU PEKEE, NA ANASIFIWA MILELE NA SI VINGINEVYO
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom