Kaka hata siku moja huwezi kuchenji lafudhi ya mtu,. Na ndo maana hata katika mada ya Asili ya kiswahili kuna mada ndogo iitwayo lafudhi. Inafahamika wazi kabisa kuwa kiswahili kimetokana lugha za kibantu. Hivo bas kiswahili cha mngoni na kiswahili cha mangi wa arachuga lazma viwe na lafudhi tofauti. Hebu angalia lafudhi ya kiswahili cha mzanzibar unaweza mfananisha na mswahili wa tarime? Ndo maana ktk kiswahili tunasema kuna sabab ambazo znamfanya mtu asiwe mahiri katka lugha ya kiswahili.; mfano, athari ya lugha mama, mfano ukikutana na mnyakusa aliyekulia unyakyusani badala ya kukwambia, Naomba viatu vyangu. Atakwambia, Naomba fiatu fyangu. Kwake yeye yuko sawa na kumrekebsha huwez sabab keshaathirika na lugha mama. Hivo bas naomba nihitimishe kwa kusema Christina Mbezi co anapenda kusema hvo bali ndivo alivo na kumbadilisha huwezi. Na hiyo haimaanishi lugha ya kiswahili haitakuwa,, bro kwani wewe unauhakika kuwa huwa unaongea kiswahili kwa ufasaha bila kuharibu sarufi ya kiswahili hata siku moja? Imposible.