Msongoru
JF-Expert Member
- Apr 16, 2008
- 306
- 24
Jamani! naamini sana katika ukimya lakini safari hii yamenishinda..... Katika kipindi chake cha asubuhi cha Watanzania tusikilize magazeti, sidhani kama uongozi wa redio hiyo unasikiliza kila siku ama la! Kuna mtangazaji mmoja anaitwa Christina Mbezi, kiswahili chake ni cha kupotosha...
Nisingelalamika sana kama angekuwa anazungumzia au anasoma magazeti hayo nyumbani kwake, ila kwa sababu ya jamii, nadhani hatutendewi haki mtu huyu kuendelea kupotosha lugha yetu kwa muda mrefu kiasi hicho. Amekua akipotosha maneno, mfano Mhariri anasoma mharili! Dalesaram, safali, laisi, uhulu, na maneno mengine mengi ambayo kwa hadhi ya chombo kama hicho sidhani kama ni sawa kulifumbia macho.....
Nimeandika haya nikijua moja kati ya dhima ya vyombo vya habari ni kukuza lugha yetu adhimu, la kama uongozi utaona ni sawa, pengine kwa kuwa hakuna chombo kinachosimamia hayo, basi waendelee. Hata hivyo lazima nikirikwamba ni kwa huyo mmoja tu, wengine wote wamekuwa wasomaji wazuri, wakiitumia lugha sawasawa!