SoC02 Jinsi lugha ya Kiswahili itakavyoondoa umasikini Afrika

Stories of Change - 2022 Competition

tenachew

Member
May 27, 2021
10
10
Hivi kweli Afrika ni masikini? Na kama ni kweli Afrika ni masikini kwanini Afrika ni masikini? Hili ni swali ambalo waafrika wengi na watanzania wamekuwa wakijiuliza, lakini je kwanza tujiulize ni kweli Afrika ni masikini?

Licha ya bara la Afrika kuwa na utajiri mwingi wa rasilimali na amali nyingi lakini ni kweli limekuwa nyuma Sana Kwa maendelea hata wengi wamediriki kusema Afrika ni bara masikini.Tukija kiuchumi Afrika iko nyuma,tukija kijeshi Afrika iko nyuma,tukija kiteknolojia Afrika iko nyuma, kwanini?

Ili tupate sababu ya Afrika kuwa masikini lazima kwanza tukubali Afrika imekuwa ikikutana na ugumu katika kutekeleza adhima yake ya kuondoa umasikini kwanini!? . Kiukweli lazima pawepo sababu Kama ilivyo Kila jambo Huwa na sababu yake na bara la Afrika limekuwa nyuma kimaendeleo Kwa sababu fulani mahususi na sababu hiyo ni kukosa lugha moja.

Afrika kukosa lugha Moja ndio sababu kuu ya Afrika kuwa nyuma Kwa maendeleo na kuwa hiyo ndio sababu ya Afrika kuwa masikini. Fuatana nami tuitafute Siri ya Afrika kuhitaji lugha Moja tu ambayo ni kiswahili katika kuondoa umasikini. Ifuatayo ni hoja inayoelezea kwa nini Afrika inahitaji kiswahili kuondoa umasikini na kuitisha Dunia Kwa mafanikio!.

AFRIKA INAHITAJI LUGHA MOJA.
Kwanza tukubali Afrika inahitaji lugha moja nayo ni kiswahili.
Lugha ni sauti zilizo katika mpangilio maalumu unaoeleweka baina ya wazungunzaji . Kutokuwa na lugha Moja Kwa bara la Afrika ni siri kubwa Sana ya Afrika kuwa masikini.
1662230382081~2.jpg

KWA NINI KUKOSA LUGHA MOJA AFRIKA IMEKUWA MASIKINI?
Hebu tutazame kwenye Moja ya vitabu vitakatifu mwanzo 11, Hapa tunaona watu wa dunia Kama ilivyo kuwa Afrika walikuwa na nguvu ya kutekeleza jambo kiasi hata Mungu alikili kuwa watalifikia wasipozuiliwa. Walikuwa na sauti Moja, walikuwa na lugha moja na siri iliyowatawanya na kuwamalizia nguvu ni kukosa lugha moja "Mwanzo 11:6 , Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. 7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao."

Ukiangalia hapa utagundua kuwa kumbe umoja, maelewano,amani na mwitikio chanya wa jamii kushiriki katika shughuli yoyote ni lugha. Hivyo siri ya kuwa wamoja,kushirikiana na kutimiza adhima na malengo ya Afrika ni Kwa kuwa na lugha moja .Hivyo siku Afrika ikiamua kutumia lugha Moja ndio siku tutaanza kuwatisha mataifa mengine Kwa nguvu na uwezo wa kutenda Kwa mafanikio na umasikini tutaukomesha. Pia hapa tumeona ukosefu wa lugha Moja Afrika ndio umeleta Hali Kama ilivyowapata hao watu walioungana kujenga mnara wa babeli.​

KWA NINI AFRIKA INAHITAJI LUGHA YA KISWAHILI?
Zipo sababu nyingi ambazo Afrika inayo haja ya kuzitumia kukipitisha kuwa lugha kuu. Lakini sababu kuu ya Afrika kutumia kiswahili ni;

Moja, Kiswahili ndio lugha rahisi kujifunza Kwa waafrika. Lugha ya kiswahili ndio lugha pekee na rahisi kujifunza Kwa nchi zote za Afrika kwa sababu Afrika ina makabila mengi ya kibantu na kiswahili kina falsafa ya Kibantu na muundo wa lugha ya Kiswahili ni kiwakilishi cha miundo ya lugha za makabila ya Afrika ya Kibantu. Utamaduni wa Kiswahili ndiyo unajitokeza katika jamii nyingi za Kiafrika. Mfumo wa familia, makuzi, misemo, nahau, methali na mengine mengi husadifu maisha ya waafrika kwa ujumla.Hivyo Afrika inayo sababu ya kukitumia kiswahili Kwa sababu watu wake ni rahisi kukielewa Kwa kuwa kimejaa tamaduni na zote za waafrika. Hii inafanya kuwa kujifunza kiswahili Kwa nchi za Afrika haitakuwa kitu kikeni kwao.

Mbili, Kiswahili tayari kimeonyesha mafanikio ya kuenea Afrika. Kiswahili ndio lugha pekee Afrika ambayo imeonyesha mafanikio makubwa na imevutia wazungumzaji wengi wanaongezeka Kwa Kasi kupindukia watumi million 200 Afrika huku Afrika mashariki ikiwa kitovu cha wazungumzaji . Ujuaji huu wa kiswahili unavutia kukipitisha kiswahili kuwa lugha ya Afrika.

Tatu, kiswahili kimepokelewa katika umoja wa mataifa. Tarehe 23 mwezi novemba mwaka 2021 shirika la umoja wa mataifa la elimu,sayansi na utamaduni UNESCO lilitangaza na kupitisha rasmi tarehe 7 ya julai kila mwaka kuwa siku ya kiswahili duniani.Siku hiyo ni kwaajili ya kukienzi na kukitangaza kiswahili. Hii ni hatua muhimu sana ya Afrika kuona sababu ya kukitumia kiswahili kama lugha kuu ya kiutendaji.

Nne, kiswahili kimepata sapoti na kuungwa mkono pakubwa kimataifa .Mfano katika azimio la umoja wa mataifa lenye kurasa tatu, inaelezwa kuwa uamuzi huo unatokana na uamuzi wa kikao cha 212 cha bodi ya utendaji ya UNESCO kwa kutumia misingi mikuu kumi ambayo imesaidia kuleta dhana na mwangaza Kwa ulimwengu wote kuwa Afrika lugha ni kiswahili. Misingi hiyo kumi inayokitangaza kiswahili ni;​

(I) Kiswahili ni mawasiliano.
(II) Wazungumzaji wa Kiswahili duniani.
(III) Kiswahili afrika mashariki, kati na kusini.
(IV) Kiswahili na kufanikisha SDGs(Sustainable Development Goals) na AcFTA(Africa Continental Free Trade Area)
(V) Kiswahili katika idhaa za umoja wa mataifa.
(VI) Umoja wa mataifa na matumizi ya lugha zaidi ya moja.
(VII) Kiswahili na utajiri katika utofauti wa kiisimu.
(VIII) Kiswahili ni lugha rasmi ya SADC (Southern African Development Community)
(IX) Kwa nini ni tarehe 7/7 na si tarehe nyingine. Tarehe 7/7/1954 nisiku ambayo chama cha ukombozi na upiganiaji uhuru (TANU) chini ya hayati mwalimu julias kambarage nyerere,rais wa kwanza wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kilipitisha Kiswahili kama lugha ya kuunganisha harakati za ukombozi, kuhamasisha umoja, kuhimiza maendeleo na kuhubiri amani.
(X) Maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani.
1662277057773.jpg

Tano, kiswahili kinatumika na vyombo vya habari Duniani kote. Kiswahili kimepata mafanikio makubwa pia kwenye vyombo vya habari kama televisheni,redio na hata magazeti mfano mzuri ni kutumika Kwa kiswahili Kwa mashirika ya utangazaji Kama BBC , sauti ya Amerika (VOA),Deutch Welle (DW) na baadhi ya magazeti ya ujerumani pia kiswahili kutumiwa na wasanii wakubwa duniani wanaotumia lugha ya Kiswahili kuwasilisha maudhui na kuwapa burudani mashariki na hadhira Duniani kote.

Sita , kiswahili kimerasimishwa na baadhi ya nchi za Afrika. Lugha ya kiswahili imepitishwa kuwa lugha ya mazungumzo na mawasiliano Kwa baadhi ya nchi na kanda za afrika kuwa ni lugha rasmi. Mfano ni Tanzania,Kenya na katika jumuiya ya afrika mashariki (EAC).
1662276811686~2.jpg

Saba, Kuanzishwa kwa tahasusi na kozi mbalimbali za Kiswahili katika nchi mbalimbali. Lugha ya kiswahili inatumika kufundishia tahasusi na kozi mbalimbali katika sekondari na vyuo vya elimu ya juu kitaifa na kimataifa mfano mzuri ni baadhi ya vyuo vikuu nchini Afrika kusini ambapo kiswahili kinafundishwa.

1662230277634.jpg


Hii ni mifano dhahiri kuwa lugha inaleta maelewano na lugha inaleta umoja .Afrika ikiwa na lugha Moja ambayo ni kiswahili basi itakuwa na umoja, itakuwa na maelewano na itakuwa na dira Moja, itakuwa na nia na dhamira moja na Kwa sababu hiyo basi itaweza kufanikiwa. Tuangalie mataifa au kanda zilizofanikiwa Kama umoja wa kiarabu, uchina, umoja wa Ulaya , marekani na wengineo wote wana sauti moja ya kutenda mambo yao. Mfano waarabu kiarabu , uchina kichina , marekani kiingereza na Ulaya licha Kila nchi kuwa na lugha zao lakini kiingereza ndio lugha ya kiutendaji hivyo Afrika nayo ikitumia kiswahili Kama lugha ya kiutendaji itafanikiwa.​

KWA NAMNA GANI KISWAHILI KITAONDOA UMASIKINI AFRIKA?
Sasa tuangalie baadhi ya sifa za lugha ya kiswahili Kwa namna gani kitachangia kuondoa umasikini Afrika?.

KISWAHILI NI LUGHA INAYOHUBIRI AMANI. Kiswahili ni lugha inayohubiri Amani ,tukiangalia bara la Afrika limeleemewa na kusongwa sana na migogoro, itikadi na ukabila mwingi kiasi cha watu kutojikita katika shughuli za kimaendeleo. Hivyo kutokana na asili ya kiswahili kuwa ni Tanzania , nchi ya amani na utulivu ,basi Kama kiswahili kitatumika Kama lugha kuu ya utendaji Afrika , kitaihubiri sifa hii njema ya kuwa na amani Tanzania kiasi kwamba maeneo ya mizozo kama Somalia, Ethiopia, Sudani, Afrika magharibi na kwingineko watafikiwa na sauti hii ya kuhubiri amani iliyobebwa na lugha adhimu ya kiswahili. Na watu wakiwa na amani basi watakuwa na muda wa kutosha kujikita kwenye shughuli za maendeleo na hivyo kuondoa kabisa umasikini na pia serikali za mataifa hayo na Afrika Kwa ujumla zitaelekeza nguvu zake kwenye shughuli za kuleta maendeleo na sio kutatua migogora .

KISWAHILI NI LUGHA INAYOHAMASISHA UMOJA. Kiswahili ni lugha inayohamasisha umoja. Lugha ya kiswahili Kwa muda mrefu Tanzania imetumuka kama chombo Cha kuhamasisha umoja baina ya makabila mbalimbali ya Tanzania. Hivyo Kama itatumiwa na bara la Afrika Kama lugha kuu basi itahamasisha umoja na ushirikiano baina ya mataifa ya Afrika na kama ilivyotumika Tanzania kuwaunganisha watanzania kuziacha tofauti zao na kutetea uhuru Kwa amani kipindi wakitetea uhuru basi hata Sasa Afrika itapata mafanikio Kwa kutumia kiswahili. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu na kiswahili ndicho chombo Cha kuleta umoja na nguvu ya umoja italeta maendeleo.

KISWAHILI NI LUGHA INAYOHAMASISHA MAENDELEO. Kiswahili ni lugha inayohamasisha maendeleo, Kiswahili ni lugha hai ambayo kila siku inakua na kuhamasisha uvumbuzi mpya unaoleta tija Kwa watumiaji. Ikiwa kiswahili kitatumika Afrika basi kunauwezekano kikaiunganisha Afrika na mwishoe Dunia yote kuwa kitu kimoja na kufanya Afrika kuwa kitovu kikuu cha ukuaji na uletaji maendeleo. Ukuaji huleta maendeleo na maendeleo huletwa na umoja , maendeleo na umoja vyote ni sifa za kiswahili. Kiswahili kikitumika basi kitaleta maendeleo.
KISWAHILI KIMEBEBA HADHI YA UTAMADUNI WA MWAFRIKA.
Kiswahili ni kibantu , hii ni kumaanisha kimebeba hadhi inayotukuza utamaduni wa watu wa Afrika ambao Kila mwafrika anaukubali na kutoa mwitikio wa kushiriki katika kuukuza na kuutukuza. Hii pia ni kumaanisha ikiwa kiswahili kitatumika Kama lugha kuu ya kiutendaji basi itakuwa ni mwanzo wa matumaini ya kuwapa heshima, ari na hamasa waafrika kushiriki katika shughuli za kimaendeleo Kama vile kiuchumi, kisiasa, kijamaa na kadhalika. Pia itawapa tumaini waafrika kujiona kitu kimoja na kuwa vyote vilivyo Afrika na Kwa ajili ya waafrika na hivyo watavitumia kuleta maendeleo Afrika bila ubaguzi wala utengano.


NINI KIFANYIKE KUKIKUZA KISWAHILI?.
Kama tulivyoweza kuona, Afrika imelemewa na umaskini na migogoro mingi inauohitaji kutatuliwa , pia kuwa Afrika inahitaji sauti Moja kuleta amani, umoja na maendeleo. Lugha ya kiswahili iliyobeba sifa na dhima ya kuhubiri amani, upendo, umoja na maendeleo ni suluhisho na tiba itakayotumiwa na viongozi wa mataifa ya kiafrika katika utendaji wa shughuli zote na hakika matokeo yake Afrika itapiga hatua na kusahau kabisa umasikini.

Natoa wito na kuwashauri viongozi wa mataifa ya kiafrika nikianzia na Tanzania ambapo kiswahili ndio chimbuko kuu na kuwa ndipo palipo na nguvu wa kukitangaza na kukieneza kiswahili, wawekeze nguvu kwa kuweka mikakati madhubuti ya kukieneza kiswahili ambacho Kwa Sasa kimeonesha mafanikio makubwa Kwa kuongeza watumiaji wengi katika nchi nyingi za Afrika . Afrika inahitaji lugha moja na kiswahili ndiyo lugha rahisi kujifunza na kuenea hivyo serikali ichukue hatua Kwa kuyaona hayo. Asanteni sana.
Jina: Emmanuel Samuel Shigela
Email:tenachewsamuel@gmail.com
Tel : +255621282979

Chanzo: Picha kutoka mtandaoni.
 
Kama hakuna uzalendo wa kweli, hofu ya Mungu kwa viongozi na watendaji wa umma na serikali, iwapo hakuna ubaninafsi (selflessness), bila shaka tutaendelea kuuimba wimbo mkuu wa ufukara Afrika hadi Kiama, licha ya rasilimali chungu nzima zilizosheheni kotekote.
 
Back
Top Bottom