Uchaguzi 2020 REDET: Uchaguzi ulikuwa Huru na wa Haki

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,780
141,667
Mtafiti Mkuu Tanzania kupitia taasisi ya Redet Prof Mukandara amesema uangalizi wa taasisi yake umegundua uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Prof Mukandara amesema 44% ya waangalizi wake wamesema uchaguzi ulikuwa huru na haki na haukuwa na hitilafu yoyote ile. Na 40% ya waangalizi wake wamesema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki lakini uligubikwa na hitilafu chache ambazo haziathiri matokeo kwa vyovyote vile.

1356CB6B-78B2-40F6-9CE2-23EDB1321D78.jpeg


Chanzo: Eatv habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Uchaguzi umeisha tugange yajayo
Prof. anaunga unga mno tumeshamchagua Magufuli tumeshakubaliana na hali
Mitano tena acha maisha yaendelee. Hizi findings ambazo ziko accelerated na Funds hazitusaidii
 
Sijui kushuhudia uongo kwa mambo ambayo yalikuwa wazi kiasi cha kutia aibu ya kitaifa yanalenga nini katika mustakbali wa taifa hili.

Morali ya wananchi kupiga kura itaendelea kushuka sana sana km kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwaka huu zitaendelna kupakwa rangi na kuonekana ni za kawaida. Madhara yake ni makubwa sana kwa chaguzi zijazo. i
 
Chama changu kinasikitisha, kila kitu kikiwa tofauti na wengi watakavyo basi kita nangwa. Kwa muono sahihi ni CHADEMA tuu?

Tutoe miwani ya mbao, ni silka kwa binadamu kukosea au kupishana muono na wengine na bado wewe au wenzako wakawa sawa.

Na ikitokea tukakubali ubora wa CCM, kama taasisi ya kisiasa bora Africa ndio siku ushindi utapatikana kwa kuwa tutatafuta silaha sawasawa zitakazo kumuangamiza adui CCM.

Hata Tume ya uchaguzi ikibadilishwa wakati sisi hatubadiliki matokeo yatabaki hivi hivi.

Kundi la Nyani lile lile kitakacho badilishwa ni msitu.

TUNA KAZI KUBWA MBELENI.
 
Wekeni michango yenu ili tupate utajiri wa maoni kutoka watu mbali mbali. Kukosoa tuu haitoshi andika na wewe yako tutajirike kielimu katika miono mbali mbali.
 
Uchaguzi umeisha tugange yajayo
Prof. anaunga unga mno tumeshamchagua Magufuli tumeshakubaliana na hali
Mitano tena acha maisha yaendelee. Hizi findings ambazo ziko accelerated na Funds hazitusaidii
Wakuuuu, hivi huyu Bia yetu yupo waapiii? Au anaonyesha UZALENDO kwa vitendo kwa kutotumia VNP?
Huu uzi lazima angeuparamia!
 
Prof. Mukandala

Amesahau muhadhara wake kuwa mazingira ya uchaguzi ukiwa wa haki, huru na halali 2020 hatma ya CCM Mpya mashakani na haijulikani:

.................................................................
Venue : Nkrumah Hall UDSM
Prof. Mukandala :Hatma ya CCM 2020 Haijulikani

Siasa na Utawala
Profesa Rwekaza Sympho Mukandala anazungumzia kigezo muhimu na kikubwa cha siasa na uongozi na kubaki madarakani kwa muda muafaka, Ni je wananchi wanafuraha?

Prof. Mukandala anasema haitoshi baba wa nyumba kuleta nyama, samaki na chakula kila siku nyumbani lakini familia yake inaishi bila furaha. Prof. Mukandala anataka utoe tathmini katika maeneo yao chini baada ya muhadhara wake na kutoa alama/ maksi juu ya utawala wa CCM


  • Kiongozi kuongoza kwa hiyari, kushawishi na siyo kushurutisha
  • Wakati wa janga kubwa kwa nchi, kiongozi kuwa mbele pamoja na wananchi kukabiliana na changamoto hiyo
  • Kukithiri kwa Umasikini wa watu
  • Maendeleo ya Vitu kuleta Umasikini ktk Maendeleo ya Watu
  • Ajira na Viwanda
  • Kilimo Kwanza na Masoko ya Kilimo , Mifugo, Uvuvi
  • Wananchi kukosa kushirikishwa ktk kipi ni kipau-mbele kwao maana serikali haitoi nafasi wananchi kusema
  • Sera za kiuchumi za serikali kukazania Maendeleo ya Vitu na kusahau kabisa Maendeleo ya Watu.
  • Utawala wa sheria
  • Uhuru wa Kujumuika na Kufanya Siasa
  • Kupiga vita rushwa
  • Kushindwa siasa za Ushawishi kubaki Siasa za Kushurutisha
  • Tanzania kuelewa diplomasia ya kujinafasi ki Geopolitics ktk majukumu kikanda / Kimataifa : SADC , EAC , Africa Union , United Nations, WHO, Benki ya Dunia World Bank, Fuko la Fedha IMF
  • Uwezo wa Mwenyekiti wa CCM kuzuia chama kisiwe na mpasuko si tu CCM Tanganyika na hata CCM Zanzibar kuelekea 2020

Kipimo cha kufanya vizuri CCM hakiwezi kupimwa kwa vile serikali yake imeweza kutengeneza miundombinu lukuki na kulazimisha watu waridhike wakati wananchi hawana furaha kutokana na ukata mifukoni mwao. Kipimo halisi ni hayo madokezo hapo juu.


Source :
25 Nov 2018
African Intellectuals : Prof. Rwekaza Mukandala - Hali ya Uchumi na Siasa Nchini Tanzania Miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano: "Tunatoka wapi, Tuko wapi na Tunakwenda wapi"
 
Huyu kaelezewa vyema kwenye kitabu cha Mkapa.

Maelezo na picha mle yanaeleza mengi kumhusu huyu Profesa na hiyo inayoitwa REDET.

Huyu akiinanga CCM, tegemea Chakubanga kuhamia ACT.
 
wamesema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki lakini uligubikwa na hitilafu chache ambazo haziathiri matokeo kwa vyovyote vile.
🤣🤣🤣. Shida hii. Sijui hao waandishi wamemuuliza ni hitilafu gani hizo na hao watafiti walitafiti nini kujua kwamba hitilafu haziathiri matokeo?

Hitilafu yoyote inaathiri matokeo somehow. Prof should not be this stupid.
 
Wapinzani walie na kusaga meno. Kasuku Zito Kabwe aliambiwa muda mrefu hata rudi Bungeni, leo hii anahaya na kutanga tanga kama taahira flani hivi kwa kuruka ruka kama kunguru.
 
Back
Top Bottom