"recipe" ya pilau

Deodat

JF-Expert Member
Sep 18, 2008
1,275
270
Wadau naomba msaada: Niko mbali na nyumbani kwa muda mrefu sasa, nimelikumbuka sana pilau na hapa ugenini hakuna restaurant/hotel wanayopika pilau. Please wenye kujua namna ya kupika pilau mnielekeze nipike mwenyewe, yaani ningejua ningekuwa naaangaliwa wakati mama au dada anapika kipindi kile niko nyumbani. Natumaini viungo nitapata kwenye Asian shops. Natakunguliza shukrani za awali.
 
Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
1,164
Unachukua mafuta unayakaanga then unachukua mdalasini unamimina kikaangoni. Baada ya hapo unachukua mpunga unachanganya na maji ya moto, hakikisha hutumii chumvi kama una presha. Then wakati mchele unakaribia kutoa rangi unachanganya na nyama ya mbuzi lakini hata ya bata fresh tu. Sasa pilau yako iko tayari kuliwa. Yafaa kuliwa na juice ya ukwaju au makomamanga utakavyopenda wewe mwenyewe
 
Thanx a million buddy!
 
Jestina

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
4,838
1,699
mnh lol.mie sijui kupika pilau ila huyo kaka hapo kakuingiza machakani,pilau ina viungo vingi kitunguu saumu,mdalasini,iliki etc
 
Deodat

JF-Expert Member
Sep 18, 2008
1,275
270
mmmh....hiyo recipe kiboko.....
mi nakushauri ugoogle au uingie kwenye blog ya chef issa au jaydee unaweza kutoka na chochote......

Thanx for the suggestion......!

mnh lol.mie sijui kupika pilau ila huyo kaka hapo kakuingiza machakani,pilau ina viungo vingi kitunguu saumu,mdalasini,iliki etc

Naona jamaa alinipa procedure ya fasta fasta! thanx for your comment!
 
Kimey

JF-Expert Member
Mar 25, 2009
4,117
827
mmmh....hiyo recipe kiboko.....
mi nakushauri ugoogle au uingie kwenye blog ya chef issa au jaydee unaweza kutoka na chochote......
Mkeku we unachojua ni kupika macharari tu lol
 
Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
1,164
mnh lol.mie sijui kupika pilau ila huyo kaka hapo kakuingiza machakani,pilau ina viungo vingi kitunguu saumu,mdalasini,iliki etc

acha kujichanganya wewe ooh sijui kupika pilau ooh huyo kaka kakuingiza machakani.
 
Shadya

Member
Sep 14, 2011
87
37
Jamani wali mmoja mapishi tofauti:...........................i wish anialike nionje hilo pilau lake la mafuta, mchele, mdalasini chumvi na maji tu mbona kaziiiiiiiii .
 
Shadya

Member
Sep 14, 2011
87
37
Dear, kuna website moja ya kizanzibar ukigoole tu, pishi lolote unalohitaji hapo utapata au wewe search tu kwenye google andika jinsi ya kupika pilau ( hapo utapata website nyingi/na njia za kupika pilau. Enjoy utafutaji wako.
 
Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
1,164
Jamani wali mmoja mapishi tofauti:...........................i wish anialike nionje hilo pilau lake la mafuta, mchele, mdalasini chumvi na maji tu mbona kaziiiiiiiii .

Nimesema unachanganya na nyama lakini lazime iwe mbuzi au bata. Wewe mbona mgumu sana kuolewa
 
FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,793
5,333
Hebu ingia kwa web hii ujipatie misosi bomba

Vipimo

Mchele wa basmati 3 vikombe

Kuku ½

Viazi 4

Vitunguu 2

Thomu iliyosagwa 2 vijiko vya supu

Binzari ya pilau nzima 1 Kijiko cha chakula

Binzari ya pilau ½ kijiko cha chai

Pilipili manga nzima ½ kijiko cha chai

Karafuu nzima 8

Iliki nzima 6

Mdalasini nzima 5 vijiti

Pilipili mbichi iliyosagwa 2

Chumvi kiasi

Mafuta ya kupikia ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele.
Kata kuku vipande upendavyo, safisha kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu na tangawizi.
Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria
Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi.
Tia thomu na tangawizi na binzari zote kaanga kidogo
Kisha tia viazi kanga kidogo kisha tia kisha tia vipande vyako vya kuku na supu acha ichemke kidogo kisha tia maji ukisie kutokana na mchele unaotumia.
mwisho tia mchele koroga uchanganye na vitu vyote acha ichemke kiasi kisha funika na punguza moto mpaka uive (huku ukiugeuzageuza)
Ukishakuwa tayari pakua kwenye sahani tayari kwa kula na salad na pilipili.

Pilau Ya Kuku | Alhidaaya.com
 
Tatizo siku hizi kitufe cha "THANKS" sikioni tena........but anyhow, senki yuu veri machi!
 
Deodat

JF-Expert Member
Sep 18, 2008
1,275
270
Sasa nitaunganisha comments zote halafu naenda kulipika pilau, likiiva nitawaonyesha picha!
 
Sigma

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
5,012
1,246
popular_afghani_dish_169.jpg
popular_afghani_dish_169.jpg
popular_afghani_dish_169.jpg
Qabeli%20Pilau%20-%20with%20chicken.JPG
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom