Cesar Caspar
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 3,096
- 5,164
Mkuu mbona unanikatisha tamaa kwa maneno andiko lako, ninaona umejitambulisha kama Madridista ila ilichokiandika hakiendani na u Madridista wako.,An
other mistake by our management, how can we sell Navas and leave players like Benzema and other flopps in the team?. Time will tell, I don't see any positive things ahead, funny enough Zizou doesn't appreciate young talents, to me Sergio regullon was far better than Mendy, why Kubo was loaned?. Let's keep on watching, I am a Madridista for life lose or win.
Kwa upande wangu sioni kosa la.Management kwenye suala la Navas kuondoka, ni.kweli alikuwa golikipa wetu mahiri sana na ametusaidia sana, ila hili la kuondoka aliomba mwenyew na club ikakubali, kwa upande wangu club ndio ilifanya jambo la busara kwani Navas alijulishwa tokea msimu unamalizika juu ya nafasi yake ndani ya kikosi akasema atabaki msimu huu, club ikamtoa Lunin kwa mkopo ili apate nafasi ya kucheza kwa kuwa angebaki isingewezekana kupata nafasi mbele ya Navas, ila dakika za Mwisho anaomba kuondoka huku tayari tumeshamtoa Lunin kwa mkopo, kwangu nilimuona kama kigeugeu, sababu angekubali toka awali kuondoka Lunin angebaki kama golikipa namba mbili.,
Ishu ya Benzema inaeleweka tokea siku nyingi kwamba anapwaya kwenye nafasi yake, kama club itafanikiwa kumsajili Mbape msimu unaokuja ndio ninadhani utakuwa Mwisho wa Benzema Real Madrid., hapa tuombee tu Jovic achangamane na wenzie mapema na aweze kuona goli vizur ili ampe Zidane changamoto kwenye kuchagua kikosi.
Regullion acha kwanza apate changamoto ya kutosha atarudi tu msimu ujao na mwezie Hakimi. Mendy yupo poa kiukweli, kama kila game atacheza kama alivyocheza juzi basi wale wapinzani waliozoea kupitia ule upande kwasasa wasahau hilo suala, Kijana yupo makini sana.
Mkuu unavyoona wewe unadhani Kubo anaweza kuchukua namba ya nani kwenye kikosi chetu kwasasa!? acha akapate experience. Sio rahisi hivyo kuchezea Real Madrid, Mwezie Odegaard licha kuwa na msimu mzuri zaidi kule Uholanzi bado ametolewa tena kwa mkopo huwezi kujiuliza imekuwaje !?