Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Leo kuna mabadiliko kidogo kwenye kikosi kitakachoanza, Nacho amechukua nafasi ya David Alaba, na Daniel Carvajal amerejea kikosini baada ya kutocheza game kadhaa juu ya majeraha.,
 
Kwenye game ya leo nitafurahi kuona battle ya Vinicius na Dani Alves, ninataka kuona Wabrazil hawa ni nani atamkalisha mwezie,
Ninakumbuka wakati Alves anacheza Sevilla, tulicheza nao, kwenye huo upande wake akakumbana na Mbrazil mwenzie Robinho ilikuwa ni battle ya aina yake, muda wote huo upande haukutulia hata kama hawana mpira refa akatoa kadi ya njano kwa wote ila bado, mwisho wa siku Robinho alifunga goli la ushindi akavua jezi akapigwa kadi ya pili ya njano na umeme juu.,
Licha ya utofauti mkubwa wa umri, ninadhani na Leo tuta enjoy.,
#HalaMadrid
 
Tumekuwa na kipindi cha kwanza kizuri japokuwa sio sana, kuna mapungufu kadhaa, haswa kwenye upande wa kulia, huu upande kwenye kulinda bado(Carvajal hajacheza kwa muda kido go) na kwenye kushambulia Asensio na yeye bado hayupo vizuri, ninadhani Ancelotti atayafanyia kazi haya mapungufu.
 
Upande wa kiungo, Kroos na Casemiro kama wanacheza nyuma sana, na hata team ikipanda kwenda kushambulia wanachelewa so tunakuwa na options chache sana tunapoingia kwenye eneo la adui
 
Back
Top Bottom