Nakubaliana na wewe. Kitendawili chenu kikubwa kiko pale katikati kwa Casemiro, Modric na Kroos. Sioni kama mnao vijana wanaoweza kudeliver kama wale jamaa. Itakua ngumu sana kufanya transition.
Sehemu nyingine hazina shida. Kijana wenu Vinicious amejielewa sana msimu huu. Amekua na utulivu ambao hakua nao kabisa kabla. I have a feeling, next season Laliga itarudi kutawala European football (UCL).
Maana mkimuongeza na Mbappe pale mbele itakua hatari sana. Sisi tunaweka vitabu sawa tumchukue Haaland. Maana naona hata Perez katulia, anajua umuhimu wa Barca kuwa kwenye form for the sake of Laliga. Msimu wenu huu, enjoy it while it lasts. Tutawapiga sana kuanzia next season!
Ni kweli kabisa, sehemu itakayotusumbua kufanya transition ni kwenye eneo la midfield, na kwa namna tunavyojenga team yetu, bado tunaijenga kwenye mfumo wa 4 3 3, hapo ina maana itabid tutafute mbadala wa Casemiro, Kroos na Modrić, japokuwa sio shida kupata wachezaji wa aina hiyo, ishu inakuja kama wataweza ku offer hao jamaa wanacho offer uwanjani ama itakuwaje!?
Tayari tuna vijana wa kufanya hiyo kazi, Blanco, Camavinga na Valverde., Hawa wana fit mfumo wa team bila shida yoyote, pia tuna vijana wengine ili wacheze vizuri itabid tubadili mfumo kwenda 4 4 2, mmoja akicheza nyuma ya forward, Hawa ni Brahim Diaz na Kubo, Hawa ili wacheze ni club iache kujenga team katika huo mfumo wa 4 3 3, ama mmoja wao awe na uwezo kama wa Modrić, yaani aweze kukaba na kutengeneza mashambulizi, kutu ambacho hao jamaa hawawezi kukifanya, mfumo huo ndio uliomnyima nafasi Isco, James Rodriguez na hata Martin Odegaard., kuna kazi ya kufanya ila ninaamini tutavuka salama kabisa.,
Kwenye suala ka kutufunga nyie msahau hilo kwasasa, bado mna safari ndefu.,