Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Mkuu madrid tuliwamiliki tukiwa kwao.

Na tumewamiliki tukiwa darajani.
Madrid ni timu kubwa yenye wachezaji ghali duniani na kocha mzoefu.

Goli moja la chelsea haliwezi kuwatoa mchezoni timu kubwa kama ile.

Ukweli ni kwamba tumewazidi uwezo uwanjani.

Walitutisha kwa majina nje ya uwanja,
Na dak90 tumeziona.
Tumewakosa goli zaidi ya saba .

This is new chelsea


Ngoja nifanye kazi sasa, kuongea kwa zamu. Huyo TT yuko na very tough season to come. Game in game out kila wiki. Mungu ambariki abebe hii ndoo ili muongeze volume JF. La sivyo mtakuja kumkataa
 
Kadi nyekundu moja ni kitu gani kwa kocha mwenye mbinu? Mbona Ajax aligewa red moja akawasasambua ikabidi red nyingine iongezeke ili mshinde?

Na kwa Ajax hamkushinda tano ingawa ana red zaidi ya moja.

Nyinyi mna red moja mnakufa 5 mnasingizia red.
Red ndio iliyo ondoa utulivu hilo liko wazi kabisa wala haliitaji ubishi.


Usisahau Jmosi kuwaangalia Man City tunavyo wauwa... Na hii Jmosi hii game sisi tunaichukulia km ya kuisoma City vzr ili tarehe 29 tuje tuiwashe moto vibaya
 
Hazard hakuonyesha Ukubwa Wake na Wala Hakujitoa Alizingua Sana.
ila Agost Tufanye Usajili Wa Kutosha.
Nani alicheza vizuri hadi umlaum Hazard? Timu nzima ilikuwa slow kulinganisha na chelsea na bado hakuna mbinu yoyote ya kocha iliyoonekana labda tujifariji mbinu hazikufanya kazi.
 
Nashkuru timu yangu kwa kutolewa nusu ili historia yetu isivunjwe ya kutopoteza fainali zote tulizoingia.maana kwa mziki huu wa Guardiola ingekuwa balaa
 
Red ndio iliyo ondoa utulivu hilo liko wazi kabisa wala haliitaji ubishi.


Usisahau Jmosi kuwaangalia Man City tunavyo wauwa... Na hii Jmosi hii game sisi tunaichukulia km ya kuisoma City vzr ili tarehe 29 tuje tuiwashe moto vibaya
Game ya tarehe 8 ndiyo ikuonyeshe hiyo timu tarehe 29 itakuaje?

Game ya kesho kutwa itakua ni mind game. Kila mmoja atataka kumtrick mwingine
 
Game ya tarehe 8 ndiyo ikuonyeshe hiyo timu tarehe 29 itakuaje?

Game ya kesho kutwa itakua ni mind game. Kila mmoja atataka kumtrick mwingine
Sisi tarehe 8 tunakwenda kushinda ili kujihakikishia top four. Kz iishe tubaki tunasubiri kukusanya makombe yanayo zagaa zagaa
 
Red ndio iliyo ondoa utulivu hilo liko wazi kabisa wala haliitaji ubishi.


Usisahau Jmosi kuwaangalia Man City tunavyo wauwa... Na hii Jmosi hii game sisi tunaichukulia km ya kuisoma City vzr ili tarehe 29 tuje tuiwashe moto vibaya
Yeye city atakuwa hawasomi
 
Mkuu madrid tuliwamiliki tukiwa kwao.

Na tumewamiliki tukiwa darajani.
Madrid ni timu kubwa yenye wachezaji ghali duniani na kocha mzoefu.

Goli moja la chelsea haliwezi kuwatoa mchezoni timu kubwa kama ile.

Ukweli ni kwamba tumewazidi uwezo uwanjani.

Walitutisha kwa majina nje ya uwanja,
Na dak90 tumeziona.
Tumewakosa goli zaidi ya saba .

This is new chelsea
Kwa city kazi haitakuwa rahisi ki hivyo na wasiwasi wangu finishing ni mbovu isingekuwa mbovu Madrid alipaswa anywe mengi tu
 
HII NDIO INAITWA TEAM WORK

Hongera sana CHELSEA FOOTBALL CLUB, leo ngoja niongelee kile nilicho kiona kwenye mchezo wa jana kwa mchezaji mmoja mmoja.

THOMAS TUCHEL : Nikianza na kocha, aisee huyu jamaa yuko poa sana. Jana kaingia na mbinu tofauti kabisa ata Zidane alishangaa sana kuona tuko vile. TT alikubali Madrid wamiliki mpira vile watakavyo ila shida ilikuwa ni jinsi gani wanaweza kuzifungua beki za Chelsea na kupata goli. Unajua ni kwann TT hutumia mfumo wa 3-4-3? We kwenye akili yako ama kuona utaona ni mabeki 3 ndio wanazuia lakini ukweli wa mambo ni mabeki 6. Hii imekuwa ngumu sana kwa timu pinzani kupata goli ndio maana Chelsea mara nyingi wanaondoka na clean sheet, ama ikitokea akafugwa basi atafungwa goli chache tu. Jana TT kaingia kwa kuzuia na kushambulia kwa kushtukiza, pindi Chelsea akiwa na mpira alikuwa anafika kwenye lango la Madrid kwa upesi sana. Madrid wao waliona ni kheri kupiga pasi tu. Big up sana TT

EDOUARD MENDY : Huyu jamaa kadri siku zinavyo zidi kuja ndio anazidi kuwa bora zaidi, moja ya magolikipa bora kabisa Duniani. Zile saves alifanya jana na kwenye game ya Fulham unabaki unajiuliza huyu ni mtu kweli.! Mimi ndio maana huwa namuita JINI, kipa anajiamini sana huyu. Mendy ana kila sifa ya kuwa golikipa bora, ana 16 clean sheet za epl huku uefa akiwa na 8.

CHRISTENSEN : Huyu dogo kuna kipindi tuliona hafai ila now days kabadilika sana. Dogo anazuia vizuri sana huyu, kuna kipindi nisipo muona kwenye kikosi naumia kabisa. Jana kacheza poa sana, kuna kipindi alipokonya mpira kisha alie kuwa na mpira akabaki anavuta soksi tu aisee nilicheka. Dogo anakuja vizuri sana

SILVA : Daah! Wengi walitucheka sana kuhusu usajili huu ila huyu jamaa amewaacha midomo wazi wamebaki na aibu zao tu. Beki mmoja mtulivu asie na papara kwenye maamuzi, Benzema alishikwa vilivyo.

RUDIGER : What a Player.! Huyu jamaa kwa anacho kifanya kwa sasa unaweza kuamini yale maneno yalio kuwa yakizagaa mitaani kuwa alianzisha mgomo ili Lampard atoke. Rudiger amebadilika sana anazuia vizuri sana mbaya ama nzuri zaidi anashamhulia pia. Kinacho nifurahisha zaidi anaelewana sana na mabeki wenzake akipanda basi Silva na Christensen wako nyuma kuweka ulinzi. Huyu jamaa ndio injini pale nyuma kwe safu ya ulinzi. Jana Madrid hawakuweza kufurukuta kabisa.

AZPILICUETA : Siku zote ukiwa kiongozi basi inabidi uwe mfano kwa watu wako. Hicho ndio alikifanya jana Captain wetu, kacheza vizuri sana kunakipindi wapinzani walikuwa wakifika kwake wanaamua kurudi waliko toka maana kulikuwa hakupitiki kabisa, Hazard mpaka unamuonea huruma alivyo shikwa na Captain wetu.

KANTE : Huyu hana maelezo mengi kila mmoja anamjua. Pain killer naomba aje amuelezee kwa kina zaidi.

MOUNT : Huyu dogo ule u haraka wake kwenye kupokea mpira kisha kushambulia unaweza hisi mpira ni kazi rahis sana. Kila mmoja anamjua vizuri tu hana maelezo mengi huyu dogo.

WERNER : Naona kaanza kurudi kwenye ubora wake

KAI : Huyu dogo bado naona hajakaa sawa pamoja na kucheza false 9 lakin inapaswa atumie vizuri zile nafasi anapata. Fainali asilete uzembe wa namna ile

Yote kwa yote kwa sasa Chelsea ni timu tishio sana Duniani we bisha tu lakini ukweli ndio huo.
 
Hivi hamuoni hii hoja ni dhaifu?

Chelsea mlicheza na ajax. Ajax akapata red mbili, mlishinda ngapi?
Ndio maana kwenye jukwaa la chelsea nilikwambia, kuna siku unakuta tim nzima haiko vizuri au tactics siki hiyo zimekataa,
Guardiola msimu huu kafungwa 5 na leicestar je utasema ni mbovu
Vipi kuhus saf alivyofungwa 6 na city utasema ni mbovu???
 
Haswa casemiro,anatembea ndani kama father yaan...hataki tabu...akipata pass anarudisha nyuma,hawazi kwenda mbele...hii timu inahitaji reform kubwa sana...
Screenshot_20210506-064544_Twitter.jpg


Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
Ndio maana kwenye jukwaa la chelsea nilikwambia, kuna siku unakuta tim nzima haiko vizuri au tactics siki hiyo zimekataa,
Guardiola msimu huu kafungwa 5 na leicestar je utasema ni mbovu
Vipi kuhus saf alivyofungwa 6 na city utasema ni mbovu???
Anyway. Thom ana msimu mzima wa kuprove kwamba timu zitakua zinaogopa kukutana naye
 
Back
Top Bottom