RC wa Kilimanjaro, Meck Sadiki na Majaji wawili Wajiuzulu. Rais Magufuli aridhia...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa viongozi wafuatao;

1. Ndg. Saidi Meck Sadiki - Aliyekuwa Nlimu Wa Mkoa wa Kilimanjaro.

2. Ndg. Aloysius Kibuuka Mujulizi - Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

3. Ndg. Upendo Hillary Msuya - Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 16 Mei, 2017 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inaeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa viongozi hao kuanzia tarehe 15 Mei, 2017.

Mikurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU Dar es Salaam 16 Mei, 2017

Hili ni jambo zuri; kuliko kuendelea kufanya kazi wakati unaona ama huiitajiki au hauko unavyotakiwa kuwa ni bora uombe kujiuzulu ili angalau uondoke na tu maslahi twako.
 
huyo mmoja aliwahi kutuhumiwa kwa kuwaachia watuhumiwa wa madawa ya kulevya katika mazingira tatanishi na pia kuwapa dhamana hata pale sheria hairuhusu
 
washaona mbali mtaani kukavu sana kama nchi haina dira wala kiongozi
 
Majaji acheni tu kazi kweli mahakimu wanakula rushwa watu wanafungwa bila hatia

Azimio la Tano: Linasomeka; “Bunge linaazimia kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aunde Tume ya Kijaji ya Uchunguzi kuchunguza utovu wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania”
 
Naona baadhi yenu mmejaribu kudadavua sababu za kuachia ngazi kwa waheshimiwa hawa bila mafanikio. Nasubiri vumbi litue nije nimwage humu mbivu na mbichi za chanzo cha kujiuzuru kwao. Hii serikali yetu ya kimabavu inachuma dhambi kubwa sana.
 
Kwani Kilimanjaro na Arusha ni mbali ? Hivi unajua kuwa mkoa wa Kilimanjaro ndiyo ulikuwa umepoteza watoto wengi walikuwa 14 na Arusha 13 sasa unachoona uongo ni nn hapo? ...
Kwani Dar na Pwani ni mbali? Hoja sio ukaribu bali mkoa upi ulihodhi shughuli ya maombolezo ya kiserikali ya msiba ule? Na nani anaratibu au anapokea rambirambi kwa niaba ya serikali?
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa viongozi wafuatao;

1. Ndg. Saidi Meck Sadiki - Aliyekuwa Nlimu Wa Mkoa wa Kilimanjaro.

2. Ndg. Aloysius Kibuuka Mujulizi - Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

3. Ndg. Upendo Hillary Msuya - Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 16 Mei, 2017 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inaeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa viongozi hao kuanzia tarehe 15 Mei, 2017.

Mikurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU Dar es Salaam 16 Mei, 2017

Kuna mawili, pengine vyeti vyao havikukaa sawa, ama shamba la bibi limewekewa kufuli.
 
Picha ninayoipata hapa ni kuwa wapo wengi wanatamani kujisambaratisha kama kina Meki sema wanamuogopa Mkemia.. ila time will tell...
 
Kilimanjaro kuna nini mpaka aburuzwe?
Mzee anataka kuwa karibu na wajukuu zake hapa Dar!
Ngoja ipelekwe damu changa kilimanjaro akanyooshe mkoa, type ya Makonda, Gambo ndo watafiti ule mkoa.
Kilimanjaro ni mkoa ambao hata bila kuwa na RC unaweza kwenda kimaendeleo kwani wanajitambua. Hukumsikia Mwigulu bungeni? Kama ilivyo Arusha, speed ilikuwa 120 ila baada ya kuja Mr Rambirambi kaleta malumbano na speed imebadilika kwani kuna wakati anaweka gia ya reverse huku anataka kwenda mbele
 
Back
Top Bottom