RC wa Iringa kafanya madudu gani?

RC wa Iringa kafanya madudu gani?

Kwa lililotokea kwenye hiyo video,mimi nipo upande mmoja na Hapi...hata kama ni daktari bingwa haiwezekani awaumize ndugu zetu wakati serikali ilishatangaza matibabu bure kwa watoto chini ya miaka 5,wazee kuanzia miaka 60 na akina mama wajawazito afu mtu aje Awalaipishe hela,tena bila mganga mkuu wa hospital kushirikishwa,katibu mkuu wa wizara including waziri na boby ya hospital halafu mseme jamaa kakurupuka,hapana aisee,pia hajamfukuza kazi ili kamkataa ndani ya mkoa wake kutokana na utendaji wake mbovu,hata kama Hapi ana mapungufu mengine lakini sio kwenye hili aisee,tu`reason vitu bila chuki wakuu!
Kwa haraka haraka unaweza ukadhani hivyo...kumbuka yeye ni referal hospital na ana wagonjwa wengi kuliko uwezo wake.wagonjwa wenye magonjwa simple yakutibiwa hata level ya dispensary mtu anamleta hapo.tujifunze kutoka muhimbili...nenda bila referal na mtoto au mzazi uone utakavyolipishwa
 
Huyu Happy ajiangalie sana kama anabisha ajikumbushe tukio la 25.12.1971 pale ndugu Kreluu alivyopigwa shabaha na Mwamwindi
Duh nilipita eneo ambalo hayati mkuu wa mkoa aliingia choo cha kike na kula Shaba za kutosha hii Dodoma road. Shukrani kwa kunikimbusha tarehe!!
 
Kiki yake IMEBUMA!
Katikisa wasiotingishika, akarushwa yeye.
Siku zote, ogopa sana kutingisha watu wanaofanya kazi chini ya mwavuli uitwao UNIONS. Unaweza kupambana na mtu mmoja kumbe nyuma yake kuna maelfu. Utashangaa kujikuta unashambuliwa na maelfu wakati wewe ulitegemea unadeal na mtu mmoja.
Akamuulize JK anawajua sana madaktari jinsi walivyomhenyesha na migomo. Au awatafute Tuico na chama cha waalimu.
Sasa hivi kina Fatma Karume na chama chao cha wanasheria wanamtia stress Magu.
Union is a single most powerful entity.
Ukifanya kazi kwa kuogopa hutufai...gharama ya kutetea haki huwa ni kifo siku zote.

Na kifo kwa mpigania haki au masilahi ya wengi ni sawa na tunu au medali kwa mwanariadha.

Kuna watu wa kuwagomea sio Mheshimiwa Magufuli. Huyu jamaa ana maamuzi magumu sana in short hayumbishwi linapokuja suala linalohitaji uhadilifu.

UKIOGOPA KUFA HUTUFAI!!!!

ASANTE
 
Kwa hali jinsi ilivyo mikoani kila mtu anataka kwenda kutibiwa hospitali ya mkoa
Sasa kupunguza utitiri wa wa watu serikali yenyewe imeweka utaratibu kuwa (kwa mfano morogoro) ukienda hospitali ya mkoa bila kupita hospitali ya kata ukapata rufaa kuandikishwa tu ni elfu10, lakini ukipata rufaa wala hulipiii
Ndivyo ilivyo mkuu hospitali zote, nimewashangaa hao madaktari badala ya kushikilia msimamo wao eti wanaomba radhi, bure kabisa!! "naomba radhi mkuu" mwingine naye sijui ndiye RMO eti tunaenda kufuta leo hii Mkuu,, pumbavu kabisa yamesoma kama hayajasoma!! Unashindwaje kumwambia huo ndio utaratibu wa serikali sehemu zote! Maana mkiruhusu haki ya nani hospitali zingine watu watakuwa wanaziruka!!
 
Write your reply...Mbona awamu hii hadi vichaa na watoto wanalopia dawa na vipimo Muhimbili.Yeye anashaanga nini?Hana habari kwamba kuna kuchangia?
 
Kosa la huyu kijana ni kulichukulia kibinafsi chuki" kuwa nilikuwa nakutafuta umeingia kwenye 18", sasa wewe ulikuwa unashaka naye na ulimwita kwanini usiweke mambo sawa huko kwamba hapa umekosea ukija kwenye mkutano kama huu unasema mlichokubaliana ili kumlindia heshima kama Dr bingwa maana pamoja na mapungufu utakuta huyu kaokoa watu wengi tu. Hata ukiwa na cheo basi usimtukane mtu mkubwa sio tamaduni zetu.
kumtukana mkubwa hata kujibizana nae sio utamaduni wetu ila Hawa jamaa naona ni utamaduni kwenye familia yao maana kaka yake alimchapa Kofi yule kibabu mwenye wajihi wa heshima kwenye inji hii ya babu🙅🙅🙅
 
Creep ndo nini? Hata kuandika hujui.utaweza kureason kweli?

Happy hana kosa hata kidogo ukiangalia creep nzima na ukaisikiliza kwa makin maamzi aliyoyachukua kwa mtu yoyote mwenye uchungu angeyafanya isitoshe Huyo Dk kapewa muda wa kutosha sana wa kujieleza kashindwa yaani happy hajakurupuka kusema ukwel tu bila kuegemea upande
 
We acha kuona wengine wanaojadili hawajui pengine wewe ndo huelewi, we jiulize presidaa katumbua hadi kachoka kaamua kuacha hujui ni kwann? Kuna vitu serikalini havitatuliwi kwa maneno bali sheria na miongozo usimwone Dr kama mtu asiyejua wajibu wake.
 
Nafikiri huu sio utaratibu mahususi wa kuadabisha viongozi siamini ktk kumsema mtu mbele za watu zaidi ni kumwondolea uaminifu na kumpunguzia morali wa kiutendaji, nahata huko mnakotaka apelekwe hawatakuwa na imani na yeye daima
 
Mwanzo nilipomwona Dr. Kaniki (DMO) akiwa na mic nikadhani yale yale yaliyomtokea akiwa mganga mkuu wa hospitali ya Mwananyamala kwa kuvuliwa koti la udaktari na mkuu wa mkoa wa Dsm kwa wakati huo mzee Makamba yanataka kujirudia tena. Ningesikitika sana.

Kitu kingine namwona mkuu wa wilaya Bw. Kasesela kama mtu wa kuchombezea chombezea kama mtu asiyejiamini kila mara mkuu wa mkoa anapokuwa anaongea. Nafikiri angeacha hiyo tabia.
 
Back
Top Bottom