Mwanahabari Huria
JF-Expert Member
- Jan 29, 2025
- 297
- 172
|||Chini ya uongozi wa Rais Samia Kuanzia mwaka 2021 hadi 2025, Mkoa umepokea Shilingi bilioni 155.24 kwa ajili ya kuboresha Elimu kwa kujenga na kukarabati Shule, kuongeza walimu na kuimarisha miundombinu ya Shule za msingi, Sekondari na vyuo vya kati. Mabadiliko haya yamesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga Shule, kuinua ufaulu na kupunguza umbali wanaotembea kufuata Elimu.
Kwa kipindi hicho, Shule za msingi zimeongezeka kutoka 682 hadi 711, na Sekondari kutoka 186 hadi 200, huku vyuo vya kati vikiongezeka kutoka chuo kimoja hadi vitatu.Pia, kumekuwa na ongezeko la vyumba vya madarasa, madawati, meza na viti kwa Shule zote, pamoja na ujenzi wa nyumba za walimu, mabweni, maabara na maktaba. Kwa mfano, madarasa ya Shule za msingi yameongezeka kwa 946 na ya Sekondari kwa 1,282. Madawati yameongezeka kwa 35,919, na walimu wapya 1,215 wameajiriwa.
Rais Samia Kwa kutumia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR), madarasa 101 yamejengwa, meza na viti 4,813 vimetengenezwa, na chuo cha VETA Bugarama kimejengwa kusaidia mafunzo ya ufundi kwa vijana|||.