RC Rose: Mkoa wa Chato utakuwa na wilaya 5 Kakonko, Biharamulo, Ngara, Bukombe na Chato yenyewe

Maswa ni Simiyu, Lohumbo ni kijiji tu siyo wiaya. Kwa hiyo hoja yako ni dhaifu sana
Shinyanga si itabaki na wasukuma wa Maswa, Kishapu, Lohumbo na Shinyanga yenyewe: zenye utajiri wa almasi na ng'ombe. Kahama iungane na wanyamwezi wenzao kuunda mkoa wao wa mahama, zao linalopatikana kahama pekee hapa duniani lakini halitambuliki na sasa hivi karibu litapotea kwenye uso wa dunia.
 
Wachukue na wilaya zote zinazovuka maji za Mwanza zihamie huko, Sengerema na Ukerewe, Mwanza ni kubwa sana, waendelee kugawa na mikoa mingine hata dar waigawe mara mbili maana kwa Tanzania maendeleo yanafika vijijini haraka kwa njia hiyo mikoa mipya na kuipa maendeleo ya mikoa.
Hahaha bila shaka hii ni post ya hasira
 
objectively, kuimega Chato kutoka Geita (ilikuwa Kagera kabla), Ngara-kutoka Kagera, Kakonko kutoka Kigoma, Bukombe na Biharamulo kuwa mkoa ni jambo jema. Kwa sasa wanaofaidi matunda ya mkoa Kagera ni Bukoba, Muleba na Karagwe. waiache Ngara iondoke tuu. mfano Ngara ilichangia sana kujenga miundo mbinu ya shule za Bukoba miaka ya nyuma....mda si mrefu wakaambiwa kila wilaya ijitegemee kwa kujenga miundombinu yake. Mpaka leo Ngara haija recover. ni miaka ya juzi tuu imeanza kupata shule zake. Ndo maana hata wana ngara waliopata elimu kupitia shule za bukoba ni wachache. Pia kutoka Ngara kwenda Bukoba ni mbali.

Chato utakuwa mkoa wenye coherence. Ngara na Kakonko lugha yao ni almost ile ile. Biharamulo na Chato zamani ilikuwa wilaya moja. imagine mtu kutoka Kakonko kwenda Kigoma kutafuta huduma. kwa raslimali walizonazo...utakuwa mkoa wenye potential sana. Ngara kuna madini ya kutosha...Chato uvuvi nk....Hata kikanisa..Ngara, Chato, baadhi ya sehemu za Kakonko, na Biharamulo ziko chini ya Jimbo moja la Rulenge-Ngara......(ingawa hili kiuhalisia halina uzito-maana imani za kidini na serikali ni tofauti)

Sema, kurahisisha maisha na huduma kwa wananchi....huu mkoa ungewekwa katikati pale Biharamulo. Ila hata makao makuu yakiwekwa Chato sioni shida...

Changamoto hapa ni kwamba wengi wanamchukia Hayati kwa hiyo hata swala la huu mkoa wanaliangalia kwa miwani ya mwendazake. ila kiukweli Chato na hizo wilaya tajwa.. unastahili kuwa mkoa.

Ingawa nashauri kuondoa au kupunguza hizi chuki dhidi ya mwendazake....tunaweza kuuita jina lingine ila isiwe Chato. Mf. mkoa wa Rubondo au mkoa wa Nyabugombe...au Burigi....nawaza tuu.

Ingawa nimalizie kwa kusema kwamba ingawa Hayati alikuwa anatokea Chato, Chato na hizo wilaya kuna watanzania wengine pia. Wathaminiwe na kuheshimiwa pia. sioni kwa nini mwananchi wa Ngara au Kakonko awe penalized kwa sababu tuu hizi wilaya ziko karibu na Chato.
Umetamka vizuri sana. Kwa waliowahi kukaa hayo maeneo watakubali kabisa kwamba kutokana na jiografia ya eneo husika Chato au Rubondo unastahili kuwa mkoa

Sent from Vivo V 19 using Jamiiforums
 
Mkuu nadhani uko sahihi. Lakini pia ukiangalia hizi wilaya tajwa ni sehemu ambazo zimesahaulika kiukweli. Mf. Ingawa Ngara ni wilaya yenye mipaka na nchi mbili, tena strategic kwa uchumi wa taifa letu..bado hata barabara ya kufika huko ni mbovu. Maybe mkiwapa mkoa, mtazinduka mjenge miundo mbinu ya kusadia hawa watu. Naamini wanaweza hata kujenga Universities, vyuo vya ufundi nk. Ndo ajira zenyewe.
Kujenga University hapana kabisa. Tuboreshe vyuo vikuu vilivyopo
 
Endapo hitaji lipo Basi Biharamlo ama Nyakanazi panaweza kuwa Kati . Ngara Hadi Chato ni km 257;Kakonko Hadi Chato km 193;Bukombe Hadi Chato km 137;Biharamlo Hadi Chato km 123; Endapo kigezo ni kuabudu mzimu Basi sawa Ila Kama ni jiografia na kusogeza huduma kwa wananchi kuifanya Chato makao makuu huo mkoa mpya ni uendawazimu, udikiteta,ushamba,ulimbukeni....
Duuh . . . Huu ni ukweli mchungu sana ila kulingana na mambo yalivyopangiliwa tangu mwanzo nahisi Chato itakuwa makao makuu ya mkoa husika
 
Makao makuu hayaangalii ukatikati wa eneo, Kuna factor nyingi ikiwemo miundombinu ya ku accommodate huduma na hadhi ya mkoa. Wilaya zingine walikua wanajipanga wakati Biharamulo inapiga porojo. Yaani hata kama B'mulo ingekua ina miundombinu ya kupokea makao makuu sawa tu, hata Kakonko au Ngara ingekua inajitosheleza ingekua vema tu lakini katika wilaya zote pendekezwa,

Wenzenu walikua wanafanya mapokeo kuanzia majengo ya mahakama, vyuo, hospital zenye level ya kanda ukiacha ya wilaya ambayo ipo siku mingi, mahotels, traffic lights, international airport (sio airstrip kama ya katoke) miradi chungu mzima yenye levels ya kikanda na wala si ya kitaifa halafu leo unasema makao makuu yapelekwe Biharamulo ambako hata hospital ya wilaya tu haipo mnang'ang'ana kuijenga pale barabarani like serious mnaomba makao makuu wilaya kongwe Afrika Mashariki tangu enzi za Mjeruman lakini bado unasema ni ya pili kwa umaskini. Kwanini watoto wenu Chato waliendelea kwa kasi hata baada ya kujikata kuliko Biharamulo ?!

Hii Chenga ya mwili ilishapigwa kitambo hakuna namna ni kuwa wapole tu.
Hahahahaha . . .yaani nimechoka mpaka Basi. Eti chenga ya mwili tangu kitambo like serious ? Ni kweli Biharamulo imekuwa nyuma sana kuliko hata Chato. Nilishangaa sana ile siku nilipofika Biharamulo. Yaani wilaya ya zamani ila miundombinu Sasa daaah
 
Na ikiwa mtu wa Ngara ana kesi Dodoma inakuwaje?
Basi ni vyema tujiulize kama mfumo wetu wa utawala kiserikali uko sawa. Hii dhana ya kuanzisha mikoa kwa lengo la “kusogeza” huduma au maendeleo kwa wananchi haina mantiki katika zama hizi. Ni kutaka kuongeza wigo wa ukiritimba na ulaji kwa wateule wa wanasiasa.
Tunahangaika kutanua serikali kuu mikoani huku tukidhoofisha serikali za mitaa ambazo ndizo zingekuwa zikiongoza utoaji huduma na kuchochea maendeleo ya maeneo yao kama ilivyo kwenye nchi zilizoendelea.
Mkuu mimi naongea kitu ambacho kipo mpaka sasa hivi watu wamesafiri kwenda Bukoba, sasa wewe unaleta imagination hebu tuwahurumie nao ni watanzania wenzetu
 
Hakuna umbali huo kati ya Ngara na Bukoba. Ukipita Karagwe ni KM 270 na ukipita Biharamulo ni KM 300. Pili KM haziwezi kuwa sababu ya kugawa kwa sasa, dunia inaelekea kuwa ya kidijitali na umbali wa kimawasiliano unazidi kupungua siku hadi siku.

Tunatumia sababu zisizo na mashiko kuongeza gharama za uendeshaji.

Na mimi nilikuwa nimeshangaa km 400
 
Mkuu wa mkoa wa Geita mh Rose amesema ombi la kuunda mkoa wa Chato likipita basu mkoa wa Geita utabakiwa na wilaya za Busanda, Nyang'wale na Geita yenyewe na Mbogwe

RC Rose amesema mkoa mpya wa Chato utapokea wilaya 1 kutoka Kigoma na 2 kutoka Kagera.

Kwa maana hiyo mkoa mpya wa Chato unaopendekezwa utakuwa na wilaya 5 ambazo ni Kakonko kutoka Kigoma, Bihalamuro na Ngara kutoka Kagera na Bukombe na Chato yenyewe kutoka Geita.

Chanzo: ITV habari!

Kazi Iendeleebda
Badala ya kuchukua wilaya ya ngara bora wachukue muleba ndio iende chato, pia mkoa wa Geita utakuwa na Kabila moja washubi hii sio nzuri kwa umoja wa kitaifa
 
PhD yake haikuwa na utata, alipewa na Dr. Akwilapo, School mate wake wakiwa Mkwawa (Single combi ya CM) ambaye alizawadiwa Ukatibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Taifa
Ila marehemu nilichompendea wale wote waliomtendea mema alikuwa anawapa vyeo ila waliomtukana kama kina Manji aliwabatiza kwa ubatizo wa moto tena wa makaa ya mawe
 
Maswa ni Simiyu, Lohumbo ni kijiji tu siyo wiaya. Kwa hiyo hoja yako ni dhaifu sana
Maswa inaweza kurudishwa mkoa wa Shinyanga na tarafa ya Lohumbo inaweza kufanya wilaya mpya kama ilivyofanywa tarafa ya Ushetu kuwa wilaya. Yote haya yanawekana. Iacheni Kahama ijinafasi.
 
Badala ya kuchukua wilaya ya ngara bora wachukue muleba ndio iende chato, pia mkoa wa Geita utakuwa na Kabila moja washubi hii sio nzuri kwa umoja wa kitaifa
Bila shaka hujawahi fika kagera kabisa.

Hiv unajua jiografia ya muleba na ngara?



Hebu kasome vzr ramani vzr halafu uje kucomment tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom