RC Paul Makonda: Mbowe ameahirisha mikutano ya CHADEMA baada ya mwanaye kuambukizwa Corona

Juzi rais katangaza mamalaka za kutangaza wagonjwa na habari za Corona ni Waziri mkuu na waziri wa afya. Leo namwangalia Makonda anautangazia umma kuwa mtoto wa Mbowe ni mgonjwa wa corona. Sijui kama nae kapewa mamlaka hayo ama amekuwa waziri wa afya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Eti mtu mropokaji hivi, ana dhamana kubwa kwa wananchi. Kwa jinsi alivyoongea kwa kejeli si kweli kuwa anamuombea huyo mtoto apone.Why this jmn? Kila kukicha kuna chuki inapandikizwa. Huwashangaa wapiga makofi.
 
Mkoa wa DSM kwa kweli umekosa hadhi kabisa.....

Jiji la watu makini...wasomi wabobezi, jiji ambalo ndiyo kiini cha uchumi waTanzania kuongozwa na la saba...hii katiba yetu ina mapungufu mengi mno.
 
Nani amempa ruhusa ya kutangaza magonjwa ya watu. Hana ethics za kazi, mambo mengine ukiyajua kupitia ofisi yako,unaomba ushauri kwa wataalam.

Paul Makonda kama mkuu wa mkoa,angetaka ushauri kwa RMO wake kabla ya kutaja magonjwa ya watu hadharani
Au katumwa na mamlaka za juu?
 
Mkoa wa DSM kwa kweli umekosa hadhi kabisa.....

Jiji la watu makini...wasomi wabonezi, jiji ambalo ndiyo kiini cha Tanzania kuongozwa na la saba...hii katiba yetu ina mapungufu mengi mno.
eti kwa vile anajua kusoma inatosha!!!yaaani?
 
Kwa hiyo yeye ndo mtangazaji wa waliougua Corona ?Huyu kwenye kichwa chake kuna fulushi la mavi.
 
Mara Corona ni sawa na wapinzani, mara mtoto wa mpinzani anaumwa Corona...kuna siku mtasema Isabela na mwana FA ni wapinzani.
 
Juzi Rais kakupa jukumu wewe na Waziri wa Afya na Msemaji wa Serikali kuzungumzia Korona na taarifa za maendeleo yake.

Lakini Leo RC Makonda kakusanya umati wa watu Stand kuu ya mabasi ili atangaze kuwa mtoto wa Mbowe ameambukizwa Korona na Zitto Kabwe ni mshirikina hivyo asisikilizwe.

Waziri mkuu, kama hiyo kazi uliyopewa na Rais kutoa habari za ugonjwa huo (sio kutaja majina) imekushinda sii ungeripoti kwa Rais ili amteue mwingine sio wewe kumpa Makonda kinyemela?

Ona style afanyayo, kwanza anakusanya watu ili waambukizane kisha wapande mabasi na kusambaza nchi nzima kisha ndio anatumia nafasi hiyo kuisakama familia ya Mbowe kwa ugonjwa ambao pia hakuna mwenye ushahidi kwani hesabu iliyotolewa na Ummy Mwalimu ni tofauti na hiyo mwakilishi wako.

Please, kemea hadharani matendo aliyofanya Makonda kabla wengine hawajaiga.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namuonea huruma sana waziri mkuu, hiki alichofanya bashite ni ukiukaji wa maagizo ya waziri mkuu na dharau kubwa kwa mamlaka za juu yake. Ila nahisi amepata baraka kutoka kwa aliyemteua.
 
Je, ndiko tumefikia kwa wagonjwa wa Korona kutajwa kwa majina? Kwamba makonda ni mwenye dhamana yakutoa taarifa kuhusu wagonjwa?

Hakika nachelea kusema uteuzi was vijana wengi awamu hii umeonesha kiasi gani vijana hatuna uwezo wakuongoza kwa weledi, I hope next term turudishe wazee tu tujifunze toka kwao.
Kateua vijana ili awatawale. Wasiwe na say kwaje
 
Akili hizi za kina Makonda ndio zitupeleke uchumi wa kati!!? Inasikitisha jana niliona post ya Haji S Manara akisifia Magufuli kupiga picha kwenye mawe akisema hiki ni chuma.

Hii nchi kuna sehemu imekwama.
Kuna dhambi gani rais kupiga picha juu ya jiwe?. Kikwete alikwenda kubembea kule Jamaica licha ya nchi nzima kuwa gizani!.

Wanasiasa ni wanadamu kama mimi na wewe, uchumi wa kati unapatikana kwa kutumia maarifa yote uliyonayo na kutokuwa mvivu katika kufanya unalolifanya.
 
Kuna dhambi gani rais kupiga picha juu ya jiwe?. Kikwete alikwenda kubembea kule Jamaica licha ya nchi nzima kuwa gizani!.

Wanasiasa ni wanadamu kama mimi na wewe, uchumi wa kati unapatikana kwa kutumia maarifa yote uliyonayo na kutokuwa mvivu katika kufanya unalolifanya.
Hakuna tatizo.. ila shida ni MATAGA kusifia kana kwamba ni jambo moja la kishujaa na la kimkakati kitaifa, kumbe just person.
 
Back
Top Bottom