Wana JF,
Naomba kupewa haki ya kikatiba kwa kupewa habari za huyu Bwana ambae kwasasa ni mkuu wa mkoa wa Mtwara Joseph Simbakalia
Juu ya ;
Uwezo wake kiutendaji kwa wale waliowahi kufanya nae kazi
Imani yake kwa MUNGU na watu wake kwa wale waliowahi/ wanaeishi nae kwenye pwani ile ya Mtwara
Wakubwa wa Magogoni wanamuonaje kuwa ni mtetezi wao ama ni mtetezi wa Taifa zima ?
ANGALIZO;
Alishawahi kuwaita wana Mtwara Wahaini na Wahuni juu ya namna wanavyodai haki zao.
The Fixer,
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Hilo jina la kuitwa wahuni ni sahihi wewe unafikili unafanya fujo za kijinga unataka uitweje,wewe mtu mzima hovyo umekaa kiuchochezi hata huna aibu jifunze kutoa elimu kwa watu kwa lengo la kuisaidia jamii na wala siyo kuchochea vurugu.
Hilo jina la kuitwa wahuni ni sahihi wewe unafikili unafanya fujo za kijinga unataka uitweje,wewe mtu mzima hovyo umekaa kiuchochezi hata huna aibu jifunze kutoa elimu kwa watu kwa lengo la kuisaidia jamii na wala siyo kuchochea vurugu.
kwa kuwa nyumba yake inalindwa na polisi wenye silaha kali, viongozi wa ccm ndio walivyo usalama ni kwao sio kwa watu wengineLicha ya vurugu na patashika iliyotokea leo na inayoendelea katika viunga mbalimbali vya mji wa Mtwara, Mkuu wa Mkoa huo Bw.Joseph Simbakalia amezungumza na Wapo Radio jioni ya leo akisema kwamba kwa siku nzima ya leo Mtwara hali ilikuwa,
shwari kabisa na changamoto zilizotokea ni za kawaida tu.
SOURCE: Wapo Radio.
Mkuu,
Maelezo yako yana nusu ukweli na nusu uwongo kabisa.
Ni kweli kwamba Simbakalia alipewa nishani na Papa Benedict wa 16 mwaka jana. Sababu ya kupewa nishani haikuwa kwaajili ya kustawisha kanisa Mkoani kwake, huu ni upotoshaji miongoni mwa wanajamvi.
Ni hatari sana kuandikia au kuelezea kitu usichojua kabisa, ambapo ni sawa na kumwaga sumu kwenye reservoir-tank la mji, maana utaua watu wengi kama si wote.
Kanali Simbakalia alitunukiwa nishani na Papa kutokana na kuwa Mlei Bora wa Mwaka.
Mlei ni Mkristo Mkatoliki ambaye hayuko kwenye daraja la Utume au upakwa mafuta, au kwa maana ingine si Padri au Sista na madaraja mengine ya juu...ni Mkatoliki wa kawaida kabisa.
Vatican ina utaratibu wa kutoa nishani kwa Mlei popote duniani endapo ataonekana kuishi maisha yanayompasa mlei, ikiwa ni pamoja kujitoa kwa ziada katika huduma kwa kanisa. Simbakalia alichaguliwa kwa vigezo hivyo, na si kwa kustawisha kanisa Mkoani Kigoma kama ambavyo post ya hapo juu inavyotaka kuwapeleka watu chakani.
Nadhani nimeeleweka!
Akiwa Col. Jeshini ,Pia ni mtaalam wa mambo ya Private Public Partnership.
Mtu amekalia simba unatarajia pana kitu hapo?
Huna tofauti na mazoea mitomingi,mambo ya kwenu mi yananihusu nini baki nayo huko kwenu sitaki uhusiano na makabila ya ajabu yanayochochea vurugu watu wafe.We kweli kibwete, ki kwetu kibwete ni kabaang
RC pengine angesema kuwa serikali inafanya kila jitihada ili Mtwara irudi kwenye hali yake ya kawaida. Lakini kusema kuwa hali ni shwari ni sawa na kuifanya Tanzania ionekane kama nchi ya 'Comical Ali'. Karibu Balozi za nchi zote za Magharibi zimeshatoa security warninga kwa wananchi wao wasitembelee Mtawara, na sababu kubwa waliyotoa ni vurugu. Sasa bwana RC kwanini anajitahidi kidogo kudodosa huku na huko kabla ya kutoa hizi habari za kimagumashi?
Kuna namna ya kufunika mambo lakini sio kwa mtindo huu. Walau taarifa iwe na chembe chembe za uhalisia na sio huu utani.
Kumbe Mdau ni Full Col. Mtaalamu pia wa katika medani za kuwa partner ??
Sasa yeye kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa yaaani ameshindwa kabisa kukaa na hawa jamaa / Wadau wooote wa Mtwara na KUMSHAURI MKUU WA NCHI ( RAIS ) namna bora zaidi ya kusonga mbele bila kumwaga damu kwenye Uvunaji na Unufaikaji wa RASILIMALI ZETU wenyewee...??
Kweli ameshindwaa ??
Kimbunga anawahusudu sana wajeshi wenzake!
Siamini kama suala ni kwa Col. Joseph Simbakalia kushindwa kutatua hili tatizo. Hili tatizo lina mambo mengi ndani yake. Kama kushindwa si kwa Simbakalia peke yake watakuwa wameshindwa wengi. Col. Simbakalia alienda Mtwara wakati mipango yote ya uchimbaji na usafirishaji gas imeishakuwa tayari. Hapa nadhani wanasiasa wetu wameshindwa kuwaandaa wana Mtwara kwa ajili ya Mradi huu na kuna majungu na uchochezi mwingi kuhusu mradi. Hivi ni kweli kabisa kwamba watu wa Mtwara hawataki gas itoke Mtwara? Mita zote hizo za ujazo watazifanyia nini? Wanatakiwa waelimishwe lakini kuna watu badala ya kuwaelimisha wanawachochea wafanye vurugu. Vurugu haina tija kwa Mtwara wala Tanzania. Haiwezekani kwamba gas iwe Mtwara tu wakati sehemu zingine za nchi zinaiihitaji. Barabara na Daraja la Mkapa ambalo ni kiuongo muhimu cha watu wa kusini na mikoa mingine havikujengwa kwa gas bali kwa rasilimali toka sehemu zingine za nchi.
Tanzania ni yetu sote na gas ni ya Tanzania.