RC Mtwara: Hali ya Mtwara ni shwari kabisa!

RC Mtwara: Hali ya Mtwara ni shwari kabisa!

hapa ndipo ninapomkubuka Dr Njau enzi hizo akiwa CPE akatufundisha EIA.
jamani labda tujiulize huu mradi ulifanyiwa EIA?? je waliofanya stake holders analysis walifanya kimakini?? manake nilitegemea jambo kama hili liwe lilishajulikana kabla mradi haujawa implemented na hapo lazima wangekuwa na project alternative.

natamani sana Dr Njau kama upo kwenye jamii forum utuambie jambo hapa kama ni kweli mraadi mkubwa kama huu uliwashirikisha stake holders wote. no wonder waliuliza mashirika ya tanesco na songas basi wakawaacha wananchi pasi kujua wanataka mradi uweje na sasa hii ndio pay back time.
gfsonwin
Nakuelewa sana ila u have to put into consideration kwamba Tanzania haipo Dar es salaam pekee, zipo sehemu nyingi sana ambazo zimesahaulika, zinahitaji kukumbukwa. Wanamtwara wanahitaji maendeleo kama mlivyo watu wa Dar, mikoa ya kusini imekuwa chanzo kikubwa cha vyakula hapa nchini, madini na hasa gas, the gov't has to solve this, sio kulifumbia macho.

Dar yenyewe iko congested sasa hivi, hembu angalia mitambo ya Songas ilipo, kisheria ni hatari sana, ile ni gas, huwa mitambo kama ile hulipuka sana, sasa je likitokea la kutokea pale ubungo, atapona mtu?

All in all, mikoa yote inahitaji maendeleo, na kwa vile source ya rasilimali inatoka kwao, basi wasisahauliwe. Wapatiwe huduma za msingi ili nao wajione watu kama sisi tunaoishi sehemu kama Dar.
 
Last edited by a moderator:
Hapa tatizo liko kwenye mitakaba inayohusiana na hili bomba, inawezekana mkopo uliotolewa kwa ajiri hii umeishagawanywa kila mtu kaishakula chake, sasa hapo bomba lisijengwe kivipi?

Mkuu Sangarara,

You have said it all, lakini kabla ya kusaini hiyo mikataba hawakujua kwamba Wanamtwara ni wadau wakubwa wa huo mradi hivyo walipashwa kushirikishwa na kuwa sensatized? Hapo ndipo serikali ilipokosa busara, labda kwa kusukumwa na 10%?

Tiba
 
Kama tatizo ni wana-ntwara kutopewa elimu ya kutosha bado serikali haiwezi kukwepa lawama. Mbona digitali na analojia zilikuwa publicized mpaka kutungiwa nyimbo na akina Mrisho Mpoto? Hii mega project ya gas na kuhamia digitali ni kipi hasa kingestahili elimu kubwa zaidi kwa umma?

Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu..wahenga walisema! Nani asiyekumbuka Netgroup Solution walivyolindwa na dola kuingia ofisini na tambo nyingi eti matatizo ya umeme yatakuwa historia, yako wapi sasa?

Kuna kitu haijakaa sawa kwenye hili suala la gesi, ushabiki pembeni, kama wameweza kuvunja daraja je bomba la gesi litakuwa salama kweli??
 
gfsonwin
Nakuelewa sana ila u have to put into consideration kwamba Tanzania haipo Dar es salaam pekee, zipo sehemu nyingi sana ambazo zimesahaulika, zinahitaji kukumbukwa. Wanamtwara wanahitaji maendeleo kama mlivyo watu wa Dar, mikoa ya kusini imekuwa chanzo kikubwa cha vyakula hapa nchini, madini na hasa gas, the gov't has to solve this, sio kulifumbia macho.

Dar yenyewe iko congested sasa hivi, hembu angalia mitambo ya Songas ilipo, kisheria ni hatari sana, ile ni gas, huwa mitambo kama ile hulipuka sana, sasa je likitokea la kutokea pale ubungo, atapona mtu?

All in all, mikoa yote inahitaji maendeleo, na kwa vile source ya rasilimali inatoka kwao, basi wasisahauliwe. Wapatiwe huduma za msingi ili nao wajione watu kama sisi tunaoishi sehemu kama Dar.

sasa Eli79 ndipo ule mchezo mbaya uliofanywa na serikali na watendaji wake wakati wa EIA unaaza kuonekana. kimsingi kabisa wananchi walitakiwa wapewe elimu kabla mradi haujaanza kutekelezwa kisha washirikishwe kwamba wao wanataka wabenefit vipi, na mradi uwe implemented vipi naamini leo hii wasingekiuka makubaliano ambayo wangeyaweka kati ya project owner na key stake holders.

hili ni kosa la pili ambalo linafanyaika ndani ya hii wizara ambalo linaigharimu serikali pesa na muda, unakumbuka mradi wa umeme kwa kakobe?? je unafikiri key stake holders walishirikishwa ona jinsi unavyofanana na huu kwamba miradi yote inasilika nishati na madini, ugomvi unatokea baada ya project implementation jambo ambalo kwa mtu wa kawaida anashindwa kaulielewa.

hii inatupa picha kwamba serikali huwa inalazimisha na kudharau watu hasa ambao wanaona hawajui vitu wakasahau kwamba watu wanajaifunza.
 
Last edited by a moderator:
Mentality ya akina kagasheki (Mwenye ardhi (kwa maana ya rais na kwenye hili mwenye gesi) kaamua sijui ni mjinga gani alimweleza kagasheki kwamba ardhi na resources zingine zote ni mali ya rais) ndio iliyotufikisha hapa. Dar es Salaam kwa maana ya central government kwa makosa inadhani kwamba ndio inajua kila kitu, ndio yenye akili kuliko wote na ndio inaweza kufikiri na kuamua lolote vile inavyotaka pasipo kuulizwa na yeyote why imeamua hivyo. This is completely unacceptable, hata mtoto ana haki ya kusikilizwa kama kweli unataka kuwa na mtu mzima aliyekamilika baadaye sembuse wananchi kwa ujumla wao? Ifike mahali serikali itambue kuwa inapaswa kutuongoza na si kutuburuza inavyotaka yenyewe hizo zama zimepita muda mrefu sana.
mkuu nakubaliana na wewe 100% kwamba mradi kama huu haukutakiwa wakurupuke tu. kwanza tayari serikali walikuwa na mfano kwa ilichovuna kwenye mradi wa umeme ulopita kwa KAKOBE FGC. kutokana na huu mradi walishajua ni kosa kiasi gani kutomshirikisha key stake holder hata kama ni mmoja.

sikuwah kuwaza kwamba wangerudia kosa kubwa kama hili tena kwenye mradi mkubwa kama huu. wadhani ingekuwa rahisi kwa wananchi wa mtwara kukataa makubaliano kama yangekuwepo?? sasa je kwann hawakuaona umuhimu wa kuwashirikisha wananchi hawa?? je kwann kila siku watuache na notion kwamba EIA huwa haifanywi ipasavyo?? manake ukweli ukifuata steps za EIA ni wazi kabisa hata ungeyaona na ungeshatafutia suluhu kabla hata ya mradi kuanza.
 
Jamani Mungu atusaidie sana, tuombe Mungu atuepushe na balaa hili, poleni sana watanzania na wana Mtwara woote kwa ujumla kwa maafa haya
 
sasa Eli79 ndipo ule mchezo mbaya uliofanywa na serikali na watendaji wake wakati wa EIA unaaza kuonekana. kimsingi kabisa wananchi walitakiwa wapewe elimu kabla mradi haujaanza kutekelezwa kisha washirikishwe kwamba wao wanataka wabenefit vipi, na mradi uwe implemented vipi naamini leo hii wasingekiuka makubaliano ambayo wangeyaweka kati ya project owner na key stake holders.

hili ni kosa la pili ambalo linafanyaika ndani ya hii wizara ambalo linaigharimu serikali pesa na muda, unakumbuka mradi wa umeme kwa kakobe?? je unafikiri key stake holders walishirikishwa ona jinsi unavyofanana na huu kwamba miradi yote inasilika nishati na madini, ugomvi unatokea baada ya project implementation jambo ambalo kwa mtu wa kawaida anashindwa kaulielewa.

hii inatupa picha kwamba serikali huwa inalazimisha na kudharau watu hasa ambao wanaona hawajui vitu wakasahau kwamba watu wanajaifunza.

Tuanuona udhaifu wa serikali kwa kurudia kosa mara mbili, na nadhani hili litawacost dearly.

Lakini pia tujiuluze, kwa nini wanaMtwara wanataka mitambo ijengwe huko na sio kusafirisha raw gas kuja Dar? Wanahisi kuna manufaa yoyote kuwa na mitambo katika mkoa wo?
 
Wamezoea propaganda wanadhani zinaweza kutumika wakati wote. Utandawazi unawaumbua. Unaweza kusema kuko shwari wakati wengine wanapiga picha na kuzipeleka duniani kwa kila tukio linalotokea nyuma ya nyumba ulipo wewe mtoa taarifa feki.
 
Mkuu Sangarara,

You have said it all, lakini kabla ya kusaini hiyo mikataba hawakujua kwamba Wanamtwara ni wadau wakubwa wa huo mradi hivyo walipashwa kushirikishwa na kuwa sensatized? Hapo ndipo serikali ilipokosa busara, labda kwa kusukumwa na 10%?

Tiba

Rushwa ni Mbaya sana ndugu yangu.
Kitu kingine cha hatari zaidi kinachoweza kuwa kinaendelea chini ya kapeti ni kwamba, wanasiasa (mafisadi) ndani ya CCM ambao wamekuwa sidelined katika mchakato wa uwekezaji katika mafuta na gas ndio wanaweza wakawa key financiers wa hizo fujo ili mradi tu kama itawezekana mchakato ucheleweshwe kidogo au mabadiriko fulani yafanyike kwa namna ambayo wao wanaamini kwamba watapata fursa ya kushiriki na kutimiza tamaa zao wa magunia ya fedha.
 
Mkuu Sangarara, kumbuka mabilioni yaliyofichwa Uswizi tuliambiwa sehemu kubwa ni kutoka kwenye makampuni ya nje ya gesi na mafuta, 10% hizo watu waliishatia kibindoni halafu mtu aje aseme bomba la gesi lisijengwe, watachinjwa kama kuku hata asipobaki mtu ni sawa tu.

Tiba
 
Tuanuona udhaifu wa serikali kwa kurudia kosa mara mbili, na nadhani hili litawacost dearly.

Lakini pia tujiuluze, kwa nini wanaMtwara wanataka mitambo ijengwe huko na sio kusafirisha raw gas kuja Dar? Wanahisi kuna manufaa yoyote kuwa na mitambo katika mkoa wo?
Eli79 wafikiri wamakonde wa mwaka 1947 ndio wa leo?? wafikiri hawaoani jinsi ambavyo hata korosho wanayovuna na kuprocess wao isivyowastawisha wao?? wafikiri hawaoni jinsi ambavyo hata bandari iliyopo kwao isivyowastawisha wao?? wafikiri watakuwa radhi kuacha gesi ghafi isafirishwe halafu warudishiwe kuuziwa kwa bei kubwa??

ndio maana nasema haya walitakiwa wawe wameongea nao kabla ya kuimplement mradi na hapo wangejua hawa wadau wanataka nini na wao watafanya nini. imagine gesi ikiwa processed hapo kwao ujue watapesa kwa kuwa vinu/,mitambo ya kuprocess, ule mwingiliano wa watu utatoa ajira kwa wazawa wa pale, achilia mbali foreign exchange. yumkini hawa wataoana hivyo kuboresha tamaduni zao sasa leo unawaambia waitoe hii kisha uwaletee kuwauzia mali iliyotoka kwao tena kwa bei kubwa??
 
Last edited by a moderator:
Matarajio ya serikali yalikuwa ni kuwaangamiza raia wote walioko Mtwara; kwa kuwa wameangamiza wachache ndo maana Mkuu huyo anasema hali ni ya kawaida.
 
among smart people i met him at AED and his paper was super... its a pity that this came from him wrong person at the wrong place and the wrong time.....he can do better than this.....

Shida siyo yeye ila ni system anayoifanyia kazi. Mpangilio mzima ni mbovu toka kwa wakubwa zake hivyo lazima aseme alichokisema au kazi inapotea. Upo hapo mkuu?
 
Mkuu,
Maelezo yako yana nusu ukweli na nusu uwongo kabisa.

Ni kweli kwamba Simbakalia alipewa nishani na Papa Benedict wa 16 mwaka jana. Sababu ya kupewa nishani haikuwa kwaajili ya kustawisha kanisa Mkoani kwake, huu ni upotoshaji miongoni mwa wanajamvi.
Ni hatari sana kuandikia au kuelezea kitu usichojua kabisa, ambapo ni sawa na kumwaga sumu kwenye reservoir-tank la mji, maana utaua watu wengi kama si wote.

Kanali Simbakalia alitunukiwa nishani na Papa kutokana na kuwa Mlei Bora wa Mwaka.
Mlei ni Mkristo Mkatoliki ambaye hayuko kwenye daraja la Utume au upakwa mafuta, au kwa maana ingine si Padri au Sista na madaraja mengine ya juu...ni Mkatoliki wa kawaida kabisa.
Vatican ina utaratibu wa kutoa nishani kwa Mlei popote duniani endapo ataonekana kuishi maisha yanayompasa mlei, ikiwa ni pamoja kujitoa kwa ziada katika huduma kwa kanisa. Simbakalia alichaguliwa kwa vigezo hivyo, na si kwa kustawisha kanisa Mkoani Kigoma kama ambavyo post ya hapo juu inavyotaka kuwapeleka watu chakani.

Nadhani nimeeleweka!

Kumbe Wakatoliki wana daraja la 'Utume' ??!
Sasa Mtume na Papa nani yuko juu !?
 
Huyu RC nadhani ana mtindio ya ubongo kwani hata kufikiri kwake ni kwa shida sana historia haifichi kitu!
 
Back
Top Bottom