RC Mtwara: Hali ya Mtwara ni shwari kabisa!

RC Mtwara: Hali ya Mtwara ni shwari kabisa!

mficha maradhi kifo humuumbua.kama wanaweza wanunue majivu na vifo vyote kama walivyofanya kununua gazeti la jamhuri
 
Unakumbuka yule msemaji wa Iraki alipokua anaambiwa wanajeshi wa marekani wapo airport, akawa anabisha na kusema wakikanyaga mto Tikrit basi hapo ndo patakua makaburi yao. Akaonyeshwa video wamevuka, akawa anabisha kabisa.

Ha ha ha umenichekesha sana jamaa akawa anaambiwa wazee wako airpot yeye anabisha ha ha ha nimecheka sana ndo hayo ya simba sasa jamani hii dunia ina vituko sana
 
Yangu macho..The movie is now in action...lets wait and see who is the steling!!:embarassed2:
 
Radio wapo inashika Mtwara? Acha ubabaishaji

ukiambiwa radio Kwizera ya Ngara inasikaka Dar utabisha ulivyo analogia ww -----,
Radio wapo, Kwizera, Ibony fm na zingine zinasikika kwenye internet hata kama simu yako ina GPRS na Radio search sasa hivi usikilize.
 
babalao 2 nikikipata nitakujulisha kinapopatikana maana hata mimi nakitafuta. Hata Mazon.com wameishiwa, hawana tena
 
Last edited by a moderator:
ni kweli atakuwa amechanganyikiwa, maana yeye ndiye alichangia sana kuhusu hii issue, pale aliposema wananchi wa Mtwara ni mahaini. na achanginyikiwe tuu
 
Mkuu, usimshangae huyu mkuu wa mkoa. Magamba wote walishafumbwa macho na masikio. Ukiona matukio kadhaa yaliyopita (hasa mauaji) na jinsi walivyo yakanusha ndo utajua ninalo lisema hapa.

Lakini pia tuwalaumu kidogo maana mfumo wa siasa wsliyomo ni ule '47 ambapo bado wanafikiri dunia si kijiji.
 
mkuu, mwache aropoke hivyo. brig gen mohamed said al sahaf alikuwa anasema hivyo hvyo majeshi ya marekani yalipokuwa yanaikaribia ikulu ya sadam
 
Hatuna rais na wala wakuu wamikoa so ni kama tuko sokoni
 
hebu anayejua anijuze neno simbakalia maana yake nn?

ukisikia simba kalia jua huyo amejeruhiwa sababu huku kwetu simba huwa wanaunguruma,hawalii kama huyo wenu wa ntwara inewezekana ni paka eti mnamuita simba!
 
Licha ya vurugu na patashika iliyotokea leo na inayoendelea katika viunga mbalimbali vya mji wa Mtwara, Mkuu wa Mkoa huo Bw.Joseph Simbakalia amezungumza na Wapo Radio jioni ya leo akisema kwamba kwa siku nzima ya leo Mtwara hali ilikuwa, shwari kabisa na changamoto zilizotokea ni za kawaida tu.

SOURCE: Wapo Radio.
 
Wenye akili tulijua angesema hivyo...
Anamdanganya nani ? Jf ni zaidi ya
kauli yake.

Huo ndiyo woga aliosema Lema.
 
RC pengine angesema kuwa serikali inafanya kila jitihada ili Mtwara irudi kwenye hali yake ya kawaida. Lakini kusema kuwa hali ni shwari ni sawa na kuifanya Tanzania ionekane kama nchi ya 'Comical Ali'. Karibu Balozi za nchi zote za Magharibi zimeshatoa security warninga kwa wananchi wao wasitembelee Mtawara, na sababu kubwa waliyotoa ni vurugu. Sasa bwana RC kwanini anajitahidi kidogo kudodosa huku na huko kabla ya kutoa hizi habari za kimagumashi?

Kuna namna ya kufunika mambo lakini sio kwa mtindo huu. Walau taarifa iwe na chembe chembe za uhalisia na sio huu utani.
 
Aseme ukweli aondolewe huo ukuu wa mkoa? Ndo tz yetu kila kitu ni kusifia tuu nae et mwanaume na ana familia, hiv unaogopa nini kusema ukweli kama kumenuka si unasema? Mi nawachukia watu kama hao watu wanakufa unasema hakuna akiyekufa, lema kasema dhambi kubwa kuliko zote ni uoga, magamba wakamuona mwongo leo tunayaina live. Polen watu wa mtwara na lindi tuko pamoja sana katika hili
 
Hahahaaa! 'Hali ni tulivu kabisa ukiondoa maeneo machache sana yenye Changamoto za Kiusalama na shughuli zinaendelea kama kawaida'- Al Sahaf wa Mtwara.
 
Huu ndiyo UJINGA wa Serikali yetu.
Sasa huyu RC bado anajua kuna watu wa kudanganywa leo hii?
 
Back
Top Bottom