Upuuzi ndo huu.
Wakati wa kulima walikuwa wapi hadi waje kuwapangia watu jinsi ya kutumia mazao yao?
Nyie Vitoto mlikuwa mnadanganywa
Kuwa Awamu ya kwanza ilikuwa ni Awamu ya Asali na Maziwa!
Enzi hizo hata kitu au zao gani ulime ni uamuzi wa Serikal sio Wewe Binafsi!
Ikiamriwa ulime zao la Biashara Wewe ukalima la Chakula unakutana na Serikal ya Tanu
Moja ya vitu anavyonifurahisha sana JPM ni kurudisha zile Nginja nginja za Nyerere tulizokuwa tunazililia kinafki
Jomba hueleweki unasimamia nini, watu wanapinga hiyo tabia ya mkuu wa mkoa kupangia wauzeje mazao yao. Huyo Nyerere unayemtaja ndio watu waliochangia wakulima wa nchi hii kuwa masikini. Sasa hivi tumetoka kwenye kilimo cha biblia(mvua) tumehamia kwenye drip irrigation na umwagiliaji mwingine. Kabla ya kulima tunaangalia soko linataka nini na sio mkuu wa mkoa anataka apateje sifa. Akitaka kulima hayo ya unga hata yeye anaweza ili ajipatie sifa zaidi badala ya kupangia ya wanaume wenzake kwa hela zao. Hatulimi kama wakulima wa zamani tunalima kibiashara tena kwa kupima udongo kwanza.
Nyie Vitoto mlikuwa mnadanganywa
Kuwa Awamu ya kwanza ilikuwa ni Awamu ya Asali na Maziwa!
Enzi hizo hata kitu au zao gani ulime ni uamuzi wa Serikal sio Wewe Binafsi!
Ikiamriwa ulime zao la Biashara Wewe ukalima la Chakula unakutana na Serikal ya Tanu
Moja ya vitu anavyonifurahisha sana JPM ni kurudisha zile Nginja nginja za Nyerere tulizokuwa tunazililia kinafki
Nyerere alikuwa "socialist" mjaaa asiejitambua na ndio maana Tanzania imefiia hapa ilipofikia,Nyerere nchi limshinda hilo alikubali mwenyewe....
Je unakumbuka yalemashimo ya barabarani ilikuwa inachukua simku mbili kufika Morogoro kwa gali,inachukua mwiki kutoka Daresalam mapka mwanza dereva alikuwa apitie Uganda ndio ageuze aje halafu aje Mwanza, Don't glorify Nyerere,sasa wewe unaona kitu cha busara baada ya mkulima kuimiza mgongo halafu uankuja kumpandia nini afanye kwa alichokivuna....
IQ ya mtanzania halisi ni kama zako ndio maana nchi haiendi mbele
Pamoja na Mbwembwe zote za kufikirika ulizotaja ikitokea Mvua kuchelewa, Ukame mnailaumu Serikali!
Serikali inalaumiwa kwasababu imeshindwa kuweka miundombinu ya umwagiliaji wakati nchi ni ya pili kwa kuwa na maji mengi Africa.Pamoja na Mbwembwe zote za kufikirika ulizotaja ikitokea Mvua kuchelewa, Ukame mnailaumu Serikali!
Huu ni ujinga wa wawaafrika,hivi mahindi mabichi yanatumika kurembea harusi au yanaliwa,kama yanaliwa hasara iko wapi?makavu yanaliwa na mabichi yanaliwa,huyu akapimwe akili,mahindi nilime mimi ili nikayauze mabichi halafu useme nisiyavune,basi na maharage mbichi yasiuzwe yataleta njaa,au zuia watu wasikoboe mahindi wasile makande,mkulima siyo mtumwa wa mtu anastahili uhuru wa kuuza mahindi yake anapoona yanafaida,nyie na kiongozi wenu simlisema hamtatoa chakula cha bure? leo kinacho wakera ni nini?Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe amepiga marufuku uuzaji wa mahindi mabichi akidai kuwa unaweza kusababisha njaa.
Dk Kebwe amesema kama hakutakuwa na udhibiti wa biashara ya mahindi mabichi kiasi cha chakula kinachotarajia kuvunwa hakitafika na hivyo mkoa unaweza kuingia kwenye aibu ya kuomba chakula kutokana na kukumbwa na njaa.
Kutokana na hilo amewataka wakuu wa wilaya pamoja na watendaji wa kata na vijiji kusimamia biashara hiyo ya mahindi mabichi inayofanywa na wakulima kwa tamaa ya kupata pesa haraka bila ya kuweka akiba ya chakula.
Katika hatua nyingine Dk Kebwe amepiga marufuku matumizi ya nafaka kwa ajili ya kutengeneza pombe kwa sababu zimekuwa zikichangia upotevu wa chakula usiokuwa wa lazima.
Amewataka wenyeji wa mkoa wa Morogoro kuuza kiasi kidogo cha chakula kwa ajili ya kufanya maendeleo na si kucheza ngoma za ‘vigodoro’.
Amesema kuwa wakulima mkoa wa Morogoro ndio pekee wenye ardhi inayostawi mazao yote ya chakula na ni miongoni mwa mikoa inayotegemewa kulisha Taifa hivyo lazima kuwe na mikakati ya pamoja ya kuhakikisha inazalisha chakula kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na ziada ya kulisha mikoa mingine.
Kwahiyo siku ukiibiwa simu watu wapigwe marufuku kuwa na simu?Bora tu apige marufuku maana wezi wanatuibia sana maindi mabichi shambani........,!