RC Morogoro: Marufuku kuuza mahindi mabichi

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe amepiga marufuku uuzaji wa mahindi mabichi akidai kuwa unaweza kusababisha njaa.

Dk Kebwe amesema kama hakutakuwa na udhibiti wa biashara ya mahindi mabichi kiasi cha chakula kinachotarajia kuvunwa hakitafika na hivyo mkoa unaweza kuingia kwenye aibu ya kuomba chakula kutokana na kukumbwa na njaa.

Kutokana na hilo amewataka wakuu wa wilaya pamoja na watendaji wa kata na vijiji kusimamia biashara hiyo ya mahindi mabichi inayofanywa na wakulima kwa tamaa ya kupata pesa haraka bila ya kuweka akiba ya chakula.
Katika hatua nyingine Dk Kebwe amepiga marufuku matumizi ya nafaka kwa ajili ya kutengeneza pombe kwa sababu zimekuwa zikichangia upotevu wa chakula usiokuwa wa lazima.

Amewataka wenyeji wa mkoa wa Morogoro kuuza kiasi kidogo cha chakula kwa ajili ya kufanya maendeleo na si kucheza ngoma za ‘vigodoro’.

Amesema kuwa wakulima mkoa wa Morogoro ndio pekee wenye ardhi inayostawi mazao yote ya chakula na ni miongoni mwa mikoa inayotegemewa kulisha Taifa hivyo lazima kuwe na mikakati ya pamoja ya kuhakikisha inazalisha chakula kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na ziada ya kulisha mikoa mingine.
 
kwahiyo anataka watu wote wale bisi ?
upload_2017-6-25_13-14-11.jpeg

kama hataki mahaindi ya kuchoma.
upload_2017-6-25_13-13-59.jpeg

images
IMG-20160321-WA0045.jpg
 
Wrngine tunalima mahindi ili tuuze mabichi kwa ajili ya kuchoma na si makavu,maana mabichi yanalipa zaidi,ndio maana tunalima kilimo cha kumwagilia asituzingue aisee
 
Yeye anafikiri kila mtu analima mahindi ya kutengenezea unga? Hajui kwamba mahindi mabichi ni ya muda mfupi na yanalipa kuliko yakishakauka? Mbona wasipangie wafanyakazi jinsi ya kutumia mishahara yao? Yeye ajipange na serekali walime hayo ya kuzuia njaa. Sio unakaa ofisini wenzio wanaumia wala hujui mipango yao kisha ulazimishe wauze kwa utashi wako. Wengine tunakopa ili tulime na kurejesha mikopo kwa wakati.
 
Kwani hayo mabichi wanakula ng'ombe?? Mahindi yangu tusipangiane matumizi maana mlishasema serikali haigawi chakula kwahiyo ninavyo yatumia haiwahusu. Pimbi kweli hawa makinikia
 
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe amepiga marufuku uuzaji wa mahindi mabichi akidai kuwa unaweza kusababisha njaa.

Dk Kebwe amesema kama hakutakuwa na udhibiti wa biashara ya mahindi mabichi kiasi cha chakula kinachotarajia kuvunwa hakitafika na hivyo mkoa unaweza kuingia kwenye aibu ya kuomba chakula kutokana na kukumbwa na njaa.

Kutokana na hilo amewataka wakuu wa wilaya pamoja na watendaji wa kata na vijiji kusimamia biashara hiyo ya mahindi mabichi inayofanywa na wakulima kwa tamaa ya kupata pesa haraka bila ya kuweka akiba ya chakula.
Katika hatua nyingine Dk Kebwe amepiga marufuku matumizi ya nafaka kwa ajili ya kutengeneza pombe kwa sababu zimekuwa zikichangia upotevu wa chakula usiokuwa wa lazima.

Amewataka wenyeji wa mkoa wa Morogoro kuuza kiasi kidogo cha chakula kwa ajili ya kufanya maendeleo na si kucheza ngoma za ‘vigodoro’.

Amesema kuwa wakulima mkoa wa Morogoro ndio pekee wenye ardhi inayostawi mazao yote ya chakula na ni miongoni mwa mikoa inayotegemewa kulisha Taifa hivyo lazima kuwe na mikakati ya pamoja ya kuhakikisha inazalisha chakula kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na ziada ya kulisha mikoa mingine.
Hii sio sawa
 
Mtu analima, anapalilia, anamwagilia serikali iko mbali kabisa na wala hijui nini kinaendelea ila ilifika muda wa mavuno tu seeikali hii hapa inapanga jinsi utakavyotumia mavuno yako.
Sahihi mkuu
 
Hii ya kupangiana vya kufanya siyo nzuri. Yeye afanye kama ametoa ushauri tu basi utekelezaji amwachie mtu mwenyewe.
 
Bora tu apige marufuku maana wezi wanatuibia sana maindi mabichi shambani........,!
 
The words of wisdom: "KNOWLEDGE is knowing what to say but WISDOM is knowing how and when to say it'
 
Yeye anafikiri kila mtu analima mahindi ya kutengenezea unga? Hajui kwamba mahindi mabichi ni ya muda mfupi na yanalipa kuliko yakishakauka? Mbona wasipangie wafanyakazi jinsi ya kutumia mishahara yao? Yeye ajipange na serekali walime hayo ya kuzuia njaa. Sio unakaa ofisini wenzio wanaumia wala hujui mipango yao kisha ulazimishe wauze kwa utashi wako. Wengine tunakopa ili tulime na kurejesha mikopo kwa wakati.
Kakurupuka
 
Upuuzi ndo huu.

Wakati wa kulima walikuwa wapi hadi waje kuwapangia watu jinsi ya kutumia mazao yao?
 
Kwani mahindi mabichi sio chakula, au hayo mahindi mabichi tunayouziwa wanakula? mbuzi?
Wakulima wadogo wadogo na walima bustani wafaidike vipi?

Yeye ni RC mvua inyeshe isinyeshe mwisho wa mwezi mifuko inatuna,

Haya mambo ya kupangiana na kulazimishana tule ugali au uji na tusile mahindi ya kuchoma yameamza lini?
 
Wanapenda kuwapangia watu tu utafikiri wanawawezesha wakulima kwenye pembejeo

Ova
 
Mambo ya
Mtu analima, anapalilia, anamwagilia serikali iko mbali kabisa na wala hijui nini kinaendelea ila ilifika muda wa mavuno tu seeikali hii hapa inapanga jinsi utakavyotumia mavuno yako.

Ajabu kabisa hii!!!!!
 
Mtu analima, anapalilia, anamwagilia serikali iko mbali kabisa na wala hijui nini kinaendelea ila ilifika muda wa mavuno tu seeikali hii hapa inapanga jinsi utakavyotumia mavuno yako.

Kwa kuwa ikitokea Njaa ni Nyinyi Wapinzani Uchwara huwa mnailaumu Serikal wakati haina shamba
 
Back
Top Bottom