RC Makalla: Nitaongea na Wadau ili daladala zinazoishia Kariakoo ziwe zinaishia Machinga Complex kesho ni mwisho wa kuhama!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,961
141,956
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema wamachinga waliogoma kuhama wataondolewa kwa lazima na vibanda vyao kuhamishwa. Kesho 30/10/2021 ndio siku ya mwisho kwa wamachinga wote kuhamia maeneo rasmi.

Kadhalika Makalla amesema ataongea na wadau wa Usafiri ili daladala zote zinazoishia Kariakoo ziwe zinaishia Machinga Complex ili kuchangamsha biashara katika eneo hilo.

Chanzo: ITV habari
 
Za tegeta na kawe ingawa zinaoyesha Gerezani

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
Ooohh ok tatizo sizitumii ndiyo maana nilizisahau kabisa, tena na Simu 2000 pia zinaishia pale Msimbazi ila bado mtu akashuke machinga complex!

Kwaiyo asiingilie Kariakoo atoboe mandera road aje aingie uhuru then Karume akunje!

Sawa ila ni kuwasumbua watu maana sidhani naona kuna kaugumu.
 
Kabla hajazipeleka atanue kwanza barabara na ajenge kituo.

Hizo za Kigamboni tu zishajaza eneo na kusababisha msongamano. Tatizo la machinga komplex hakuna nafasi ya kufanyia biashara.

Mitaa yote inayozunguka yale majengo kuna vituo vya daladala na kutoka maeneo karibu yote ya Dar.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema wamachinga waliogoma kuhama wataondolewa kwa lazima na vibanda vyao kuhamishwa. Kesho 30/10/2021 ndio siku ya mwisho kwa wamachinga wite kuhamia maeneo rasmi.

Kadhalika Makalla amesema ataongea na wadau wa Usafiri ili daladala zote zinazoishia Kariakoo ziwe zinaishia Machinga Complex ili kuchangamsha biashara katika eneo hilo.

Source: ITV habari
Mkuu wa mkoa ndio atahama...................wait for the sarcasm to be staged by the confused animals
 
Back
Top Bottom