RC Makalla: Nitaongea na Wadau ili daladala zinazoishia Kariakoo ziwe zinaishia Machinga Complex kesho ni mwisho wa kuhama!

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema wamachinga waliogoma kuhama wataondolewa kwa lazima na vibanda vyao kuhamishwa. Kesho 30/10/2021 ndio siku ya mwisho kwa wamachinga wite kuhamia maeneo rasmi.

Kadhalika Makalla amesema ataongea na wadau wa Usafiri ili daladala zote zinazoishia Kariakoo ziwe zinaishia Machinga Complex ili kuchangamsha biashara katika eneo hilo.

Source: ITV habari
Akili za mlipuko zezeta, poor management, failure to manage the unexpected, failure to think expansively, traggedy of the commons and common of the traggedy. Mentally decomposing leaders at work.
 
Akili za mlipuko zezeta, poor management, failure to manage the unexpected, failure to think expansively, traggedy of the commons and common of the traggedy. Mentally decomposing leaders at work.
Mzee Amos makala ni mtendaji mzuri sana shida yupo na chama ambacho si sahihi.

Unajua ili uweze kung'aa na uwezo au kipaji chako ni lazima uwe sehemu sahihi. Mtendaji mzuri sifa yake ya kwanza ni kusimamia utaratibu regardless watu mtamuonaje. Akitumika vibaya mtamchukia, akitumika vizuri mtampenda.
 
Ukweli ni kwamba hakuna daladala terminal kariakoo, ile terminal ambayo ilikuwepo gerezani imechukuliwa na Udart mwendokasi.
Shehena ya mabasi mapya ya Mwendokasi ikiingia daladala zitaishia huko huko pembezoni!
 
Mbezi Beach huku bado kwenye residential plots bado wamejaa!! Makalla usipowaondoa hao utakuwa umelikoroga na hapo lazima awajibike diwani wa Kawe na wenyeviti wa mitaa husika kwani wao ni wadau wa hizi biashara ndio maana wana hujumu zoezi!.

Sasa Makalla usikae ofisini na kuitisha press conference tu, njo mtaani uone live!
Roho mbaya ya mwafrika
 
Hivi hao Machinga wana lipi la maana hadi wawe kama wanabembelezwa wakati raia walipa kodi hawana upendeleo wowote kama hao wakepa kodi
La maana sana ni walikuwa wapiga kura wa mwendazake akawatengenezea vitambusho akawauzia akapiga pesa za kutosha baada ya hapo machinga wakawa hawatawaliki hata kwenye mifereji ya barabarani waliweka vibanda vyao
 
30 October 2021

ARUSHA WAWAPANGA MACHINGA KUFUATANA NA AINA YA BIDHAA NA HUDUMA WANAZOUZA


  • Gereji na vifaa vya kuchomelea wapewa eneo,
  • wauza mbogamboga matunda na chakula wapangiwa eneo,
  • wauza mitumba wapatiwa eneo
  • pia wauza vifaa vya eletroniki simu umeme redio vyombo vya nyumbani,
  • Fenicha na useremala nao wagaiwa eneo lao...
Source : Millard Ayo
 
Yaani Nia yangu ninkwenda Kariakoo, wewe unipeleke Machinga complex. Huyu ni Makala au Sakala?

Ajifunze kuheshimu haki za raia, sio kutupelekesha kiboya atakavyo
Hata hivyo hakuna kibali kinachotolewa sasa kwa daladala kuishia kariakoo ila zote zinaishia gerezani au machinga complex, ukiona daladala inaishi either kariakoo elewa sheria haija simamiwa ipasavyo.

Mfano, daladala za tegeta, makumbusho, kawe au msasani zote zinaishia pale lilipo soko but kwa route yake ni kuishia gerezani.
 
Eenhee! Mnataka kila mtu awe shoeshiner mjini!? Au ndio yale ya kupunguza msongamano magerezani kwa kuondoa wezi wa kuku na kujaza machinga!? Huyo anayejiita makala hata mbeya alitusumbua sana sisi machinga. Machinga wa dsm tafuteni namna ya kupambana naye, kwa kuwa akili hana huyo jamaa.

Watapigwa tu hakuna namna.
 
Back
Top Bottom