Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameingia Kariakoo kwa kutumia basi la Mwendokasi (haijulikani alikotokea) na kutoa Maagizo kwamba baada ya siku 7 njia zote za watembea kwa miguu kwenye eneo hilo ambazo zimejaa wamachinga, mama lishe, wachoma mihogo na wauza Alikasusi ziwe wazi.
Haijulikani ni wapi wamachinga hao watapelekwa.
=======
RC MAKALLA: MARUFUKU MACHINGA KUFANYA BIASHARA KWENYE NJIA ZA WATEMBEA KWA MIGUU.
- Asema
agizo hilo ni kwa Wafanyabiashara Mkoa mzima.
- Amtaka
DC Ilala na Uongozi wa Machinga kuweka utaratibu mzuri kuwapanga Machinga Kariakoo.
- Awapo mbinu ya
kufunga baadhi ya Mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya Biashara.
-
Wamachinga wakiri kuingilia maeneo ya watembea kwa miguu na kuahidi kuhama.
- Aeleza
dhamira yake ya kuboresha mandhari ya Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mhe. Amos Makalla amepiga marufuku
ufanyaji wa Biashara Kwenye maeneo hifadhi ya barabara zote za Mkoa huo baada ya utaratibu huo kuwa
chanzo cha uvunjifu wa amani na ongezeko la ajali.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipotembelea
Soko la Kariakoo na kujionea Kero ya
Ufanyaji biashara holela Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.
Kutokana na hilo
RC Makalla amewaelekeza
Mkuu wa Wilaya ya Ilala kufanya kikao na Wafanyabiashara hao Jumatatu ya *September 13 na kuainisha maeneo ya kuwapeleka wote waliovamia hifadhi ya Barabara.
Aidha RC Makalla amewaelekeza Kuangalia utaratibu mzuri wa kufunga na kufungua baadhi ya Mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya biashara Kutokana na ufinyu wa maeneo ili Waweze kupata riziki.
Hata hivyo RC Makalla amesema kwa tathimini aliyofanya amebaini Hali ya Ufanyaji biashara holela Dar es salaam ipo kwa kiwango kikubwa na kuwanyima watembea miguu haki zao za msingi.
Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Manispaa zote za Mkoa huo kuweka Vibao vya kuzuia biashara Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.