Kijue kisiwa cha Ukerewe kwa undani. Kisiwa cha kifahari kilichopo pembezoni mwa jiji la Mwanza

MwanaUkerewe

Member
May 28, 2020
14
75
Salaam kwenu wote wana jamvi

Haya ni mambo machache kuhusu wilaya/kisiwa cha Ukerewe.

Maelezo mafupi
UKEREWE ni moja wapo ya wilaya zinazounda mkoa wa Mwanza. Pia ni miongoni mwa wilaya za mwanzo mwanzo (kongwe) kuanzishwa nchini Tanzania. Wilaya ya Ukerewe ina ukubwa wa eneo wa kilometa za mraba zipatazo 530.

Idadi ya watu

Wilaya ya ukerewe ina jumla ya wakazi wapatao 345,147. Kata 25, tarafa 4 na vijiji 76.

Ukerewe ni kisiwa
Mbali na kuwa wilaya, Ukerewe ni kisiwa. Ndicho kisiwa kinachoongoza kwa ukubwa barani Afrika na kisiwa cha tano kwa ukubwa duniani. Pia Ukerewe ndicho kisiwa pekee kisichokuwa ndani ya bahari kwa ukanda mzima wa Afrika.

Kisiwa hiki kinapatikana kusini mashariki mwa Ziwa Viktoria nje kidogo ya jiji la Mwanza ambacho kwa ujumla wake kinaundwa na visiwa vidogo dogo vipatavyo 38 huku kisiwa kikubwa kikiwa ni kisiwa cha Ukara huku vingine vikiwa havikaliwi na watu.

Makabila yanayopatikana
Wilaya ya Ukerewe inakaliwa na watu wa makabila mbali mbali kutoka kila pembe ya nchi na nje ya nchi. Lakini makabila makuu ni matatu ambayo ni Wakerewe(wenyeji), Wajita na Wakara. Mbali na kuzungumza lugha tofauti, haya makabila wanasikilizana kwa ukaribu kabisa. Pia Kikerewe kinarandana na kihaya kutokana na ufanano wa baadhi ya maneno.

Hali ya hewa na vivutio vya asili vinavyopatikana
Ukerewe ni wilaya iliyobarikiwa kuwa na hali ya hewa safi ya wastani na uoto wa asili pia ni kitovu cha utalii wa ndani. Miongoni mwa vivutio vya utalii vinavyopatikana ni pamoja na mapango ya Handebezyo, jiwe linalocheza "dancing stone" la Nyaburebeka.

Mbali na vivutio hivyo uwapo ukerewe utapata fursa ya kulitazama ghorofa la kwanza kumilikiwa na mtu mweusi. Vile vile utapata fursa ya kutembelea na kuitazama shule kongwe ya Kagunguri ambapo profesa wa kwanza nchini Tanzania alipata kusomea hapo pamoja na viongozi mbali mbali waliowahi kushika nyadhifa mbali mbali za juu serikalini kama vile Pius Msekwa na wengineo.

Mji mkuu
Mji mkuu wa ukerewe ni NANSIO (Kiswahili) au NANSYO (Kilugha). Ni mji mzuri wenye mandhari ya kupendeza na unaokua kwa kasi sana. Hali ya kimaisha katika mji huu ni ya kawaida sana kwa mtu yeyote mwenye kipato ama mtafutaji kuweza kuishi na kuendesha maisha yake.

Shughuli za kiuchumi
Shughuli kubwa ya kiuchumi inayotegemewa ni uvuvi japo kilimo na ufugaji vinafanyika lakini kwa kiwango kidogo sana. Pia ni kisiwa kizuri kwa kufanyia shughuri za biashara, usafirishaji na utalii wa ndani.

Huduma ya elimu
suala la elimu wilayani Ukerewe limepewa kipaumbele. Katika jitihada za kutokomeza adui 'ujinga' wilayani Ukerewe kuna jumla ya shule za msingi 125 na shule za sekondari 25.

Huduma za afya
wilaya inatambua umuhimu wa afya bora kama nguzo muhimu katika kuchochea suala la maendeleo ya mtu binafsi, familia na Taifa kwa ujumla katika kuleta maisha bora na kupunguza umaskini. Kwa kulitambua hilo, wilaya imejenga jumla ya vituo ya afya 4, zahanati 28( sawa na uwiano wa zahanati moja kwa kila kata) na hospitali moja ya wilaya kwa lengo la kutoa huduma za afya kwa wananchi.

Huduma zingine za kijamii
Huduma zote za kijamii kama vile usafiri, maji na umeme vinapatikana. Pia uwepo wa benki mbili na mawakala mbali mbali wa kifedha na huduma za simu waliotapakaa kila sehemu umerahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha uwapo kisiwani ukerewe.

Gharama za usafiri
Gharama za usafiri kutoka mwanza kufika ukerewe zinatofautiana kutokana na chombo cha usafiri ulichotumia. Mchanganuo wa gharama za usafiri ni kama ifuatavyo,
kivuko cha Nyehunge
nauli ni Tsh 6,000/= ( kawaida) na Tsh 7,000/=( seat za juu)
Umbali wa safari: masaa 3

Kivuko cha serikali(Mv clarias na butiama)
nauli ni Tsh 6,000/=
Umbali wa safari: masaa 2 na nusu

Kivuko cha serikali(Mv ilemela)
nauli ni Tsh 2,000/= Hiki kivuko kipo pembezoni kidogo mwa mji kinafanya safari zake kati ya ukerewe na kayenze kupitia kisiwa cha bezi.

Kivuko cha Mv Rafiki(fast boat)
nauli ni Tsh 10,000/= (kawaida) na Tsh 15,000/= VIP(seat za juu)
Umbali wa safari: Saa moja na nusu

Nauli za mabasi ni Tsh 10,000/=
Umbali wa safari: masaa 8-9

Hitimisho
Haya ni machache kati ya mengi yanayopatikana katika kisiwa hiki adhimu kabisa. Wenyeji wa hiki kisiwa ni watu wakarimu na wapenda wageni hivyo msisite kukitembelea na kujionea mengi yanayopatikana kwenye hiki kisiwa cha Ukerewe kilichopo pembezoni mwa jiji la Mwanza.

Viambatanisho

BlurCamera-EasyFocus_20200528_140329.jpg
Monarch beach resort
BlurCamera-EasyFocus_20200528_104944.jpg
Nansio tower

2052243_Screenshot_20191010-0900002.jpeg
Nansio port

BlurCamera-EasyFocus_20200528_085001.jpg
Some landscape

BlurCamera-EasyFocus_20200528_090143.jpg
Mwiboma-hamuyebe
IMG_20200625_173406_4.jpg

Mv Rafiki( fast boat)

images (4).jpeg
Jiwe linalocheza(dancing stone)

images (12).jpeg
Handebezyo

images (13).jpeg
Mapango ya handebezyo

images (11).jpeg
Mv ilemela( ukerewe to kayenze-mwanza via bezi island)

images (10).jpeg
Nyehunge ferry

images (7).jpeg
Mv clarias
EWC-9pDWsAMxvdQ.jpg

Mv Butiama( kuanza kazi karibuni)

BlurCamera-EasyFocus_20200528_085526.jpg
Lake Victoria view

images (8).jpeg
Shughuli za uvuvi(fishing activities) zikiendelea

images (5).jpeg
Kitoweo cha samaki aina ya sato

images (6).jpeg
Kitoweo cha samaki aina ya sangara

2052195_images202.jpeg
Monarch beach

Karibu Nansio, karibu kisiwa cha Ukerewe
 
Msuluhishi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
247
250
MwanaUkerewe,

Nimesikia watu wengi wakisifia sana uzuri wa kisiwa cha Ukerewe na jinsi Wakerewe walivyo watu wapole na wakarimu. Hata hivyo kuna wengine wanasema kwamba kwa kiasi fulani bado kuna imani za kishirikina katika jamii.

Mleta mada hili hukuligusia lakini je, ni kweli au wanasingiziwa tu? Hebu tupe maoni yako kuhusu hili.
 
Igombe fisherman

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
965
1,000
Hapo kwenye nauli ya Basi,,mabasi yanapita wapi kuingia nansio,au Yana muundo wa hovercraft?,
Pili,kisiwani Cha kome kilichoungua juzi nacho kipo ukerewe au bukoba?
Ngoja hapa nijaribu kumjibia mtoa mada. Basi zinazotoka mwanza kwenda ukerewe zinapitia barabara ya msoma likifika bunda linaacha barabara kuu ya msoma linaelekea magharibi wanapaita kisorya. Kisha litavushwa na panton na kuendelea na safari kwenda nansio
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
35,317
2,000
Ngoja hapa nijaribu kumjibia mtoa mada. Basi zinazotoka mwanza kwenda ukerewe zinapitia barabara ya msoma likifika bunda linaacha barabara kuu ya msoma linaelekea magharibi wanapaita kisorya. Kisha litavushwa na panton na kuendelea na safari kwenda nansio
Ndo kusema kisorya na ukerewe sio mbali kivile?
 
MwanaUkerewe

Member
May 28, 2020
14
75
Nimesikia watu wengi wakisifia sana uzuri wa kisiwa cha Ukerewe na jinsi Wakerewe walivyo watu wapole na wakarimu. Hata hivyo kuna wengine wanasema kwamba kwa kiasi fulani bado kuna imani za kishirikina katika jamii. Mleta mada hili hukuligusia lakini je, ni kweli au wanasingiziwa tu? Hebu tupe maoni yako kuhusu hili.
Kwanza nashukuru kwa swali zuri ulilouliza na hili swali limekuwa likiulizwa mara kwa mara
Nimesikia watu wengi wakisifia sana uzuri wa kisiwa cha Ukerewe na jinsi Wakerewe walivyo watu wapole na wakarimu. Hata hivyo kuna wengine wanasema kwamba kwa kiasi fulani bado kuna imani za kishirikina katika jamii. Mleta mada hili hukuligusia lakini je, ni kweli au wanasingiziwa tu? Hebu tupe maoni yako kuhusu hili.
Kwanza nakushukuru kwa swali zuri na hili swali limekuwa likiulizwa mara kwa mara na sisi kama wanaukerewe bila kuchoka tumekuwa tukilijibu na tutaendelea kulijibu mpaka pale watu watakapopata uelewa wa kutosha kuhusiana na uvumi huu.

Imani za kishirikina kiujumla ni imani potofu ambazo zinatakiwa kupingwa si tu ukerewe peke yake bali na jamii zote za kitanzania kwa sababu ni miongoni mwa mambo yanayokwamisha maendeleo katika jamii.

Katika wilaya ya Ukerewe,Ni kweli nakiri wazi kwamba hizo imani zilikuwepo lakini baada ya muingiliano wa watu kutoka makabila tofauti tofauti, imani hizo zimepungua kwa asilimia kubwa kama siyo kutokomea kabisa. Nikuhakikishie tu kwamba kwa sasa hali ni shwari, watu wako bize zaidi kuchapa kazi kwa lengo la kujiletea maendeleo. kwahiyo ukisikia mtu bado anaishutumu hii wilaya kwa imani za kishirikina ujue anatumia historia ya zamani ya miaka mingi iliyopita(ambayo haipo kwa sasa) kuchafua sifa na taswira nzima ya uzuri wa kisiwa hiki.
 
jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
6,828
2,000
Salaam kwenu wote wana jamvi

Haya ni mambo machache kuhusu wilaya/kisiwa cha Ukerewe.

Maelezo mafupi
UKEREWE ni moja wapo ya wilaya zinazounda mkoa wa Mwanza. Pia ni miongoni mwa wilaya za mwanzo mwanzo (kongwe) kuanzishwa nchini Tanzania.

Idadi ya watu

Wilaya ya ukerewe ina jumla ya wakazi wapatao 345,147. Kata 25, tarafa 4 na vijiji 76.

Ukerewe ni kisiwa
Mbali na kuwa wilaya, Ukerewe ni kisiwa kikubwa kinachopatikana ndani ya Ziwa Viktoria pembezoni kidogo mwa jiji la Mwanza ambacho kwa ujumla wake kinaundwa na visiwa vidogo dogo vipatavyo 38 huku kisiwa kikubwa kikiwa ni kisiwa cha Ukara huku vingine vikiwa havikaliwi na watu.

Makabila yanayopatikana

Wilaya ya Ukerewe inakaliwa na watu wa makabila mbali mbali kutoka kila pembe ya nchi na nje ya nchi. Lakini makabila makuu ni matatu ambayo ni Wakerewe(wenyeji), Wajita na Wakara. Mbali na kuzungumza lugha tofauti, haya makabila wanasikilizana kwa ukaribu kabisa. Pia Kikerewe kinarandana na kihaya kutokana na ufanano wa baadhi ya maneno.

Hali ya hewa na vivutio vya asili vinavyopatikana

Ukerewe ni wilaya iliyobarikiwa kuwa na hali ya hewa safi ya wastani na uoto wa asili pia ni kitovu cha utalii wa ndani. Miongoni mwa vivutio vya utalii vinavyopatikana ni pamoja na mapango ya Handebezyo, jiwe linalocheza "dancing stone" la Nyaburebeka.

Mbali na vivutio hivyo uwapo ukerewe utapata fursa ya kulitazama ghorofa la kwanza kumilikiwa na mtu mweusi. Vile vile utapata fursa ya kutembelea na kuitazama shule kongwe ya Kagunguri ambapo profesa wa kwanza nchini Tanzania alipata kusomea hapo pamoja na viongozi mbali mbali waliowahi kushika nyadhifa mbali mbali za juu serikalini kama vile Pius Msekwa na wengineo.

Mji mkuu
Mji mkuu wa ukerewe ni NANSIO (Kiswahili) au NANSYO (Kilugha). Ni mji mzuri wenye mandhari ya kupendeza na unaokua kwa kasi sana. Hali ya kimaisha katika mji huu ni ya kawaida sana kwa mtu yeyote mwenye kipato ama mtafutaji kuweza kuishi na kuendesha maisha yake.

Shughuli za kiuchumi
Shughuli kubwa ya kiuchumi inayotegemewa ni uvuvi japo kilimo na ufugaji vinafanyika lakini kwa kiwango kidogo sana. Pia ni kisiwa kizuri kwa kufanyia biashara na utalii wa ndani.

Huduma ya elimu
suala la elimu wilayani Ukerewe limepewa kipaumbele. Katika jitihada za kutokomeza adui 'ujinga' wilayani Ukerewe kuna jumla ya shule za msingi 125 na shule za sekondari 25.

Huduma za afya
wilaya inatambua umuhimu wa afya bora kama nguzo muhimu katika kuchochea suala la maendeleo ya mtu binafsi, familia na Taifa kwa ujumla katika kuleta maisha bora na kupunguza umaskini. Kwa kulitambua hilo, wilaya imejenga jumla ya vituo ya afya 4, zahanati 28( sawa na uwiano wa zahanati moja kwa kila kata) na hospitali moja ya wilaya kwa lengo la kutoa huduma za afya kwa wananchi.

Huduma zingine za kijamii
Huduma zote za kijamii kama vile usafiri, maji na umeme vinapatikana. Pia uwepo wa benki mbili na mawakala mbali mbali wa kifedha na huduma za simu waliotapakaa kila sehemu umerahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha uwapo kisiwani ukerewe.

Gharama za usafiri
Gharama za usafiri kutoka mwanza kufika ukerewe zinatofautiana kutokana na chombo cha usafiri ulichotumia. Mchanganuo wa gharama za usafiri ni kama ifuatavyo,
kivuko cha Nyehunge
nauli ni Tsh 6,000/= ( kawaida) na Tsh 7,000/=( seat za juu)
Umbali wa safari: masaa 3

Kivuko cha serikali(Mv clarias na butiama)
nauli ni Tsh 6,000/=
Umbali wa safari: masaa 2 na nusu

Kcha serikali(Mv ilemela)
nauli ni Tsh 2,000/= Hiki kivuko kipo pembezoni kidogo mwa mji kinafanya safari zake kati ya ukerewe na kayenze kupitia kisiwa cha bezi.

Kivuko cha Mv Rafiki(fast boat)
nauli ni Tsh 10,000/= (kawaida) na Tsh 15,000/= (seat za juu)
Umbali wa safari: Saa moja na nusu

Nauli za mabasi ni Tsh 10,000/=

Hitimisho

Haya ni machache kati ya mengi yanayopatikana katika kisiwa hiki adhimu kabisa. Wenyeji wa hiki kisiwa ni watu wakarimu na wapenda wageni hivyo msisite kukitembelea na kujionea mengi yanayopatikana kwenye hiki kisiwa cha Ukerewe kilichopo pembezoni mwa jiji la Mwanza.

Viambatanisho

View attachment 1461593
Monarch beach resort
View attachment 1461599
Nansio tower

View attachment 1461601
Nansio port

View attachment 1461602
Some landscape

View attachment 1461605
Mwiboma-hamuyebe

View attachment 1461606
Mv Rafiki( fast boat)

View attachment 1461612
Jiwe linalocheza(dancing stone)

View attachment 1461613
Handebezyo

View attachment 1461614
Mapango ya handebezyo

View attachment 1461615
Mv ilemela( ukerewe to kayenze-mwanza via bezi island)

View attachment 1461616
Nyehunge ferry

View attachment 1461617
Mv clarias

View attachment 1461619
Mv Butiama( kuanza kazi karibuni)

View attachment 1461621
Lake Victoria view

View attachment 1461623
Shughuli za uvuvi(fishing activities) zikiendelea

View attachment 1461624
Kitoweo cha samaki aina ya sato

View attachment 1461625
Kitoweo cha samaki aina ya sangara

View attachment 1461627
Monarch beach

Karibu Nansio, karibu kisiwa cha Ukerewe
Wajita oyee...
 
mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
24,327
2,000
MwanaUkerewe,

Nimesikia watu wengi wakisifia sana uzuri wa kisiwa cha Ukerewe na jinsi Wakerewe walivyo watu wapole na wakarimu. Hata hivyo kuna wengine wanasema kwamba kwa kiasi fulani bado kuna imani za kishirikina katika jamii.

Mleta mada hili hukuligusia lakini je, ni kweli au wanasingiziwa tu? Hebu tupe maoni yako kuhusu hili.
Huyu bwana ana sifa zote za kua kiongozi lkn tatizo lake ni moja tu ni MKARA,hahahahhahah-Nyerere
 
MwanaUkerewe

Member
May 28, 2020
14
75
Ngoja hapa nijaribu kumjibia mtoa mada. Basi zinazotoka mwanza kwenda ukerewe zinapitia barabara ya msoma likifika bunda linaacha barabara kuu ya msoma linaelekea magharibi wanapaita kisorya. Kisha litavushwa na panton na kuendelea na safari kwenda nansio
Asante sana kwa majibu ya kina bila shaka muulizaji atakuwa ameelewa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom