Jiwe linalocheza na upotoshaji wa simulizi

Kishimbe wa Kishimbe

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
5,024
4,831
JIWE LINALOCHEZA NA UPOTOSHAJI WA SIMULIZI!

Mara nyingi sana simulizi huwa zinapotosha sana uhalisia wa habari, hasahasa kama tukio likiwa mbali sana na msimuliwaji au kama ni jambo lililotokea zamani! Lakini cha ajabu zaidi ni pale mtu anapoelezea kitu ambacho kipo na unawezapelekwa na kukiona, lakini bado mtu anatia chumvi simulizi mpaka unaesimuliwa ukaona labda ni uchawi, mizimu au ujumbe 'live' kutoka kwa Bwana Mungu.
Nisiwachoshe, kuna kile kinachoitwa JIWE LINALOCHEZA LA NYABUREKEKA, KISIWA CHA UKARA, WILAYA YA UKEREWE, MWANZA. Masimulizi ya waliofika lilipo na wenyeji wa maeneo husika huwa yanaashiria kana kwamba labda jiwe hilo hupigiwa ngoma likacheza, hali kiukweli kabisa mimi ninaweza kuliita jiwe hilo 'NYABUREBEKA SEESAW ROCK' kwani si zaidi ya jiwe kubwa kidogo ambalo kwa umbile lake na sehemu liliyopo linaweza kuwa kama mzani wa kiaina na mtu aweza kulichezesha kwa kulisukumasukuma! HIVI MUUJIZA HAPO UPO WAPI ZAIDI YA UHABA WA UPATIKANAJI WA KITU CHA AINA YAKE?

TAZAMA HII VIDEO!



Kweli kabisa jiwe hilo ni la ajabu kwa kuwa sio kitu unachoweza kukiona kila sehemu duniani, japo, nina imani kabisa, kwamba halipo peke yake duniani! Cha msingi tunapolitangaza kama kivutio cha utalii basi tulieleze jinsi lilivyo kiuhalisia!

MY TAKE: Hata kama tunataka kuvutia vivutio vyetu vya utalii ni vizuri sana tukawa wakweli tunapovitangaza maana tunawezasutwa na watalii halafu wakaona kila tunachowaambia ni longolongo tuuu!
 
labda usiku nitafanya hiyo kazi
172460.jpg

Kweli ngosha mwanaume, yaani unategeshea ifike saa tano usiku utumie zile GB zilizobaki za kifurushi cha usiku ulichonunua jana usiku! Anyway kwa wewe sishangai sana, maana ni hulka yenu wa Kaskazini!
 
Back
Top Bottom